Malisa na Mikopo ya Elimu ya Juu

Malisa na Mikopo ya Elimu ya Juu

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
Wengi waliosoma nje ya nchi kwa kulipiwa na bodi ya mikopo (HESLB) wanadaiwa fedha nyingi kulinganisha na waliosoma nchini. Nimeona jamaa ana mshahara 900K but anadaiwa 47M. Kwa mwezi atakatwa 143K, kwa mwaka 1.7M. Under "ceteris paribus" mwamba atahitji miaka 28 kumaliza deni lake. Lakini ukiongeza "rention fee" atahitaji miaka 35 kumaliza deni.

Assume ana mika 30 kwa sasa. Jumlisha 35 ya kulipa deni atakua na miaka 65. Umri wa kustaafu ni miaka 60. Maana yake atastaafu bila kumaliza kulipa deni. Ikitokea hivyo Bodi itaenda kukomba kiinua mgongo chake kumalizia deni (kama sheria inavyosema). Sasa jiulize je huku ni kumsaidia mtanzania au kumkomoa?

Kunapaswa kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu mikopo ya elimu ya juu. Wazazi wanaoweza kusomesha watoto wao kwa kuwalipia ni vizuri wafanye hivyo, badala ya kuwaingiza kwenye mikopo hii inayoumiza. Pili, wazazi wasio na uwezo serikali iwape watoto wao ruzuku (bursary) si mikopo (loan)

Awamu ya kwanza na ya pili serikali iliwapa ruzuku wanafunzi wote wa elimu ya juu. Awamu zilizofuata zikaondoa ruzuku na kuleta mikopo. Nyerere na Mwinyi waliweza nini ambacho kimewashinda waliofuata?

Wakati wa Nyerere na Mwinyi wanafunzi wa vyuo vikuu walikula bure, kusoma bure, na kulala bure. Na bado walipewa pesa ya kujikimu. Kuna kipindi nchi ilipita kwenye hali ngumu kiuchumi Nyerere akapunguza bajeti ya mayai kwenye breakfast ya wanafunzi wa UDSM. Wakafanya mgomo. Akawaita Ikulu na kuwatia bakora

Wakati ule mwanafunzi hana pressure ya ada, kula wala kulala. Anapewa pesa ya stationeries, field na research. Asubuhi anapewa breakfast yenye mapochopocho kibao (maziwa, mkate, mandazi, pancacke, chees, jam, mayai, juice, sambusa, sosage etc). Halafu wanapunguziwa mayai wanaamua kugoma. Nyerere akawatia bakora. Akawaambia msijifanye nyie ni muhimu kuliko watanzania wengine.

Sasa wale waliosomeshwa kwa ruzuku na kupata fursa zote hizo, ndio wameleta kitanzi kinaitwa mikopo ya elimu ya juu. Kitanzi hiki kimewatesa sana watoto wengi wa maskini. Hivi Nyerere nae angeweka mikopo hawa viongozi wa leo wangesoma? Nashauri MIKOPO ifutwe wanafunzi wapewe RUZUKU kama zamani. Rasilimali tulizonazo kama taifa zinatosha.!

Malisa GJ
 
Walipe tu hakuna namna maana walipo vyuoni wanataka mikopo wasilete siasa uchwara kwenye mikopo
Kumbuka kuwa hata hao unaowatetea kuwa wapate nao watatakiwa kuja kulipa hiyo mikopo. Masuala nyeti kama haya tusiingize itikadi za kisiasa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkopo wa Bodi umegeuka na kuwa tatizo jingine kwa Watanzania wa kawaida...

Halafu pia bodi wamegeuza wadaiwa kama chanzo cha mapato, maana ukifikiria mantiki ya hicho kitu wanaita retention, hakuna!
Wamekopeshwa wengi... Na wanazidi kukopeshwa wengi... Hivyo obviously hili ni tatizo kubwa sana linatengenezwa bila kujua... Litakuja kuleta shida baadae kama halitarekebishwa
 
Aliyeshiba hakumbuki mwenye njaa, hivi hata bwana mkubwa si kasomeshwa bure...
Anyway ngoja nimwache ale mema nchi for now.
 
Wamekopeshwa wengi... Na wanazidi kukopeshwa wengi... Hivyo obviously hili ni tatizo kubwa sana linatengenezwa bila kujua... Litakuja kuleta shida baadae kama halitarekebishwa
Basi serkali isitishe kutoa mikopo kila mtoto ajilipie kuepusha kelele
 
Basi serkali isitishe kutoa mikopo kila mtoto ajilipie kuepusha kelele
Kuna watu wanafanya kejeli katika hili labda ni kwasababu tu ya ushabiki au hana mtoto ambaye anamsomesha au yeye mwenyewe nk.
Hapa hakuna mtu aliyekataa au hataki kulipa deni la serikali.

Hakuna mtu anapinga kuwa mkopo ule haukuwa au hauna manufaa kwa watoto wetu au mnufaika. Kinacholalamikiwa hapa ni ile sheria mpya ya mwaka 2016.Jamani kiuhalisia sheria ile imegeuza dhana ya ule mkopo kuwa mateso kwa mnufaika.

Na mimi niwaambie ukweli kama watu wangejua ingekuja tungwa sheria hii mtu nadhani angeacha kusoma.Hata hawa watoto wetu basi tu hawajui kitakachokuja kuwakuta.

Nadhani iko siku kila mmoja atakuja aamini hiki watu wanacholalamika. Yaani haingii akilini wewe kwenye salary slip uliwekewa labda milion 6.

Halafu ukapigwa sijui penalty ikaw2a mil.9 kwenye salary slip.Badae salary slip ikasoma nil halafu baadae unaambiwa deni liloko kwenye salary slip si HALISI,deni lako halisi wanajua Bodi,ukitaka kujua wasiliana nao,UNAPEWA deni jingine upya.

Swali unajiuliza,penalty ya mil 3iliyongezeka kutoka 6 hadi 9 ili cover vitu gani? kwanini deni lako lote lisiwekwe kwenye salary slip?.

Jamani kama kweli hawa wabunge wetu kwadhati kabisa walipitisha sheria hii kwa matakwa yao kabisa na kwa moyo radhi na hawakuona dosari kabisa na sheria yenyewe waliielewa kabisa, basi kwa wale tunae amini uwepo wa mungu,basi mungu atasikia kilio chetu hiki na atulipia.
 
Basi serkali isitishe kutoa mikopo kila mtoto ajilipie kuepusha kelele
Suala lililopo si kuacha kutoa mikopo... Sababu Serikali ndio tegemeo.. yawepo marekebisho katika baadhi ya mambo juu ya sheria ya urejeshaji wa mikopo
 
Soon kodi ya kichwa itarudi kwa style hii,Mi nimeelewa tu huo mstari....waliosoma bure ndiyo wameleta huo utumwa kwa wengine......mchawi wa muafrica ni muafrica mwenyewe hao wanaoitwa mabeberu hata hawana shida.....shida ipo kwa hii ngozi ya masizi
 
Kinachofanyika ni unyonyaji kwa watoto wa wanyonge, hivi inakuwaje mtu aliyesoma chuo kikuu cha umma kama UDSM, SUA, Mzumbe arejeshe kiasi kile kile kama waliosoma vyuo vikuu vya binafsi wakati mishahara na bajeti za kuendesha vyuo vikuu vya umma inatolewa na serikali.

Niliwahi kusema serikali iendelee na utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wanachuo waliochaguliwa kujiunga vyuo vikuu vya umma na nafasi za kujiunga zitolewe kulingana na bajeti na uhitaji, jambo la kwanza ni kuvunja bodi ya mikopo na hilo swala lisimamiwe na wizara yenyewe...
 
Nilipokuwa nafuta ujinga katika elimu ya juu, kuna wakati nilijikuta najikunyata pale ambapo wanafunzi wenzangu walipokuwa wanatangaziwa kwenda kusaini "bumu". Kuna wakati ilinibidi nijichanganye na marafiki zangu ili na mimi nionekane wa maana, yaani mnufaika wa mkopo wa elimu ya juu, kulikuwepo kama kaunyanyapaa kiaina hivi "huna mkopo"?

Maisha ya chuo yaliendelea mpaka tukamaliza japo sikufanikiwa kumaliza Ada yote lakini namshukuru sana mkuu wa chuo alinielewa na baada ya miezi minane hivi ya kuhitimu chuo nilifanikiwa kulipa deni lote nikapewa cheti changu.

Nataka kusema nini hapa, wale waliopata mkopo wa elimu ya juu hawaoni kama mkopo ulikuwa na unafuu katika elimu yao bali lilikuwa bomu linalo walipukia sasa. Nashauri mamlaka husika zirekebishe sheria hii ili kuleta unafuu wa mkopo unaolipika bila kuweka ongezeka lolote. Kama mwanachuo alikopeshwa 6m.alipe 6m. Mkopo wa elimu siyo biashara.

Nawatakia kheri ya mwaka mpya 2021.
 
Hapo awali dhamira ilikua njema tu but later turned into parastatal. So watu wanahitaji faida, magawio nk. Ni mtego km mitego mingine akili kumkichwa. Elimu ya tz siyo mtaji huwa hairudishi hela.
 
Kinachofanyika ni unyonyaji kwa watoto wa wanyonge, hivi inakuwaje mtu aliyesoma chuo kikuu cha umma kama UDSM, SUA, Mzumbe arejeshe kiasi kile kile kama waliosoma vyuo vikuu vya binafsi wakati mishahara na bajeti za kuendesha vyuo vikuu vya umma inatolewa na serikali. Niliwahi kusema serikali iendelee na utaratibu wa kutoa ufadhili kwa wanachuo waliochaguliwa kujiunga vyuo vikuu vya umma na nafasi za kujiunga zitolewe kulingana na bajeti na uhitaji, jambo la kwanza ni kuvunja bodi ya mikopo na hilo swala lisimamiwe na wizara yenyewe...
Rahisi wa wanyonge Mungu anamuona
 
Back
Top Bottom