Malisa: Kuhusu Hardtalk sikutaka kusema lolote kwa sababu alichokifanya Lissu hakuna mwanaCCM yeyote anayeweza kufanya

Hivi haya maneno yote haya mleta mada angeyachapa kwenye kanga angefanikiwa kutoa doti ngapi?
 
Kwa taarifa yako rais anayo mamlaka ya kuamua ni kipi kipelekwe kwanza bungeni kabla hakijaagizwa.

JPM aliamua kukwepa urasimu wa kisiasa kwenye manunuzi ya hizi ndege, aliamua kukwepa mijadala isiyo na tija.

Akaamua kutumia utaratibu kama ule wa manunuzi ya silaha na ndege za kivita, angesema alihusishe bunge basi mpaka leo kusingekuwa na ndege hata moja iliyokwisha nunuliwa.
Sikatai analo jukumu la kupeleka lipi bungeni lijadiliwe lakini ni makosa kuliruka bunge kufanya manunuzi moja kwa moja. Ni kuipuuza katiba.
Acha kulamba viatu hata pasipo faa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaha, we jamaa bwana, kama ningelikuwa kitengo cha kugawa buku 7 sidhani kama ningekupa hata senti. Sasa ndo umeandika shudu gani hapa, ulitakiwa kuja na facts ku-support maelezo yako badala yake unakuja na maneno ya kwenye khanga.
Teteeni mtakavyo tetea. Hata mkimpiga deki, Lisu kajiaibisha. Kathibitisha ni mkurupukaji.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unaongelea hizi za ATC ama za kijeshi.
Kama za kijeshi sawa kuna utaratibu wake

Ila mimi nazungumzia manunuzi haya ya hizi za kawaida.
Kama ni hizi za kawaida si dhani kama ni sawa.
You behaves like a manipulator any way.
Hueleweki

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sio ndege tu, rais anao uwezo wa kuidhinisha manunuzi yoyote yale anayoona inafaa pasipo kushauriwa na bunge. Inampasa tu aidhinishiwe fedha na usalama wa taifa.
 
Utampeleka nani wa CCM kwenye HARDtalk?

Niggaz pliiz.

CCM ina watu wengi sana walio capable na kufanya mahojiano na vyombo vya habari vya kimataifa.

Msitake kuniambia kuwa waziri wetu wa mambo ya nje hana uwezo. Hivi mmeshawahi kumwona akihojiwa na vyomvo vya nje?

Kabisa unaweza kusema with a straight face kwamba Mahiga hana uwezo wa kufanya mahojiano na HARDtalk?

Ben Mkapa je?

Mark Mwandosya je?

Abdulrahman Kinana je?

Asha-Rose Migiro je?

CCM ina hazina ya kutosha ya watu wenye uwezo. Acheni siasa za kijinga.

On the other hand, upinzani wana nani? Huyo Lissu mwenyewe alibanwa mbavu na hakujibu vizuri maswali.
Mkapa aliqualify kwenda HARDTALK baada ya kuua CUF kule Pemba enzi zile, na alipanick sana chini ya Sebastian. Lissu amequalify baada ya kumiminiwa risasi 16 mwilini na CV yake kali. Hao wengine uliowataja sidhani kama HARDTALK watakuwa na haja nao. Siyo tu ishu ya kufiti pale HARDTALK, swali ni je, watakuwa tayari kuwahosti? Discussion iliyofuatia HARDTALK ya Lissu ilikuwa kali kiasi Sackur akaona naye atie neno. Hiyo inakupa idea ya umuhimu na umaarufu wa Lissu. Japo umaarufu huo kapewa na CCM bila wao kujua, au kwa kutojua kwao.

JPM anaweza kwenda kutokana na UMAGUFULI wake, lakini nadhani itakuwa kichekesho cha karne na burudani ya nguvu. na sidhani kama CCM watamruhusu. Mahiga alionekana kama mtu wa maana alipokuwa umoja wa mataifa. Lakini kila tukimwangalia na kumsikiliza, haoneshi weledi wowote wa pekee. so boring kiasi kwamba hata HARDTALK hawawezi kumhitaji.
 
Mkapa aliqualify kwenda HARDTALK baada ya kuua CUF kule Pemba enzi zile, na alipanick sana chini ya Sebastian. Lissu amequalify baada ya kumiminiwa risasi 16 mwilini na CV yake kali. Hao wengine uliowataja sidhani kama HARDTALK watakuwa na haja nao. Siyo tu ishu ya kufiti pale HARDTALK, swali ni je, watakuwa tayari kuwahosti? Discussion iliyofuatia HARDTALK ya Lissu ilikuwa kali kiasi Sackur akaona naye atie neno. Hiyo inakupa idea ya umuhimu na umaarufu wa Lissu. Japo umaarufu huo kapewa na CCM bila wao kujua, au kwa kutojua kwao.

JPM anaweza kwenda kutokana na UMAGUFULI wake, lakini nadhani itakuwa kichekesho cha karne na burudani ya nguvu. na sidhani kama CCM watamruhusu. Mahiga alionekana kama mtu wa maana alipokuwa umoja wa mataifa. Lakini kila tukimwangalia na kumsikiliza, haoneshi weledi wowote wa pekee. so boring kiasi kwamba hata HARDTALK hawawezi kumhitaji.

Okay, ni maoni yako.
 
Kwa aina ya mabandiko niyaonayo hapa kutoka kwa wafuasi wa lissu,baada ya yale mahojiano kwenye kipindi cha HARD TALK,ni dhahiri kabisa kuwa jamaa hawaamini kilichotokea.kwa mtu ambaye wao walikuwa wakiamini kwamba ni 'best of the best'kupoteana kiasi kile kwenye kujibu maswali,bado inakuwa ngumu kumeza kwao.
Sasa wanajaribu kuhalalisha kuvurunda kwa mtu wao kwa hoja kama.....
Ooooh flani naye aende akahojiwe tuone.....
Oooh sijui watanzania wangapi wameshawahi kuhojiwa pale.....
Mara sijui kipindi cha lissu kimepata watazamaji zaidi ya Million 35o....
Na blah blah blah nyingine kibao.......
Ni hivi..........
Jamaa sio smart kama mnavyojidanganya,ila ni vile tu watu wengi wamezoea kushikiwa akili zao.
I'm sure you didn't grasp the context of that conversation, just as it happened to the abrupter bashite
 
Kuhusu Hardtalk sikutaka kusema lolote kwa sababu alichokifanya Lissu hakuna mwanaCCM yeyote anayeweza kufanya. Hakuna. Si JPM, si Bashiru, si Kibajaj wala Fuso. Hakuna. Si kiongozi mstaarabu kama mama Samia, au mropokaki kama Chakubanga. Hakuna. Narudia hakuna kiongozi yoyote wa CCM (kwa nyakati hizi) anayeweza kukaa kwenye Hardtalk walau kwa dakika 5 tu bila kuzirai, au kupanick. Hakuna.

The program called HARDTALK, and only Hard brains takes chance. Sasa utampeleka nani wa CCM kwenye Hardtalk? Akaseme nini? Fonti fedi badala ya front page? Au conjogate badala ya congratulate? Hebu kuweni serious kidogo.

Only hard brains, and global brains can take chance to Hardtalk. Lissu ni Global brain ndio maana ameshiriki Hardtalk na amejibu kwa utashi na weledi maswali yote kwa muda wote wa kipindi. Muulizeni Kagame kilichomtokea alipoalikwa kwenye hicho kiti. 🤣🤣. Hakuweza kustahimili kabisa. Panicking za kutosha utadhani anahojiwa na waasi wa FNL Palipehutu.

Kwahiyo kile kiti sio chepesi. Ni cha moto kwelikweli. Ndio maana Hardtalk ni moja ya vipindi vinavyoheshimika sana duniani. Watu wanaichukulia Hardtalk kirahisi utadhali Lissu aliitwa kwenye 'Dakika 45' za ITV au kwenye 'Kapu la TBC'. Ile ni HardTalk ya BBC. Kuweni serious.!

Kuonesha kuwa Lissu ni global brand kipindi chake kimetazamwa na watu milioni 350 duniani kote hadi sasa. Na wengine wanaendelea kutazama. Milioni 350 ni sawa na watanzania wote mara 7. Hii ni heshima kubwa kwa mtu ambaye ni Mbunge tu kufuatiliwa kwa wingi kiasi hiki duniani pote. Mpelekeni JPM akitizamwa na watu laki mbili na nusu, mniambie nianze kutafuta uraia wa nchi nyingine.

Lissu alijibu maswali yote kwa hoja na weledi mkubwa. Kuna vitu vitatu ambavyo nimeona CCM wakipiga navyo kelele. Cha kwanza ni grammar ya Lissu. Wanadai Lissu alipanick hadi akasahau kiingereza. Eti kuna mahali alitumia 'are' badala ya 'is' na akatumia primary auxiliaries badala ya modal auxiliaries. Yani CCM leo wamegeuka walimu wa English paper 1 form five HKL? Hiki ni kichekesho. CCM hawahawa ambao JPM akiboronga wanasema kujua kingereza sio kipimo cha akili, ndio wanaomfundisha Lissu kingereza leo? Wgat a shame?

Yani Lissu kutumia 'are' badala ya 'is' nayo ni hoja ya kujadili? Kwahiyo tuseme Lissu ameharibu grammar kuliko mzee wa Fenti fodi sio? Hebu acheni utani. Bora Lissu amekosea grammar kidogo akiwa kwenye 'kiti moto cha dunia' kuliko mzee wenu anayekosea grammar hata akiwa anasalimia wananzengo. Jiulize siku akipelekwa kwenye Hardtalk itakuaje? Kiingereza chote cha kemia kitaevaporate kwenye intaprinyuaa.

Hoja ya pili ambayo wanaCCM wameibeba ni kuhusu ushoga. Kwamba eti Lissu alidai akiwa Rais ataruhusu ushoga. Uongo wa mchana kweupe. Hapa ndipo napohisi huenda hawakutazama kipindi, na kama walitazama hawakuelewa, na aliyewatafsiria aliwapotosha.

Lissu alichosema ni kwamba sheria za nchi yetu (ambazo zimetungwa na wabunge wengi wa CCM) haziruhusu serikali kuingilia masuala ya faragha ya wananchi wake. Yani dola haina mamlaka kisheria kuchunguza watu wanafanya nini katika vitanda vyao. Kwahiyo akiwa Rais na sheria zikabaki kama zilivyo atakachofanya ni kuzingatia utawala wa sheria. Unless otherwise yafanyike marekebisho ya sheria ya kuruhusu serikali kuingilia mambo ya faragha ya wananchi wake.

Kwa lugha rahisi ni kwamba majibu ya Lissu yaliivua nguo serikali ya CCM, ambayo inajidai kupinga ushoga lakini serikali hiyohiyo imetunga sheria za kulinda faragha. Lissu alichomaanisha kama tunataka kupingana na ushoga tubadili sheria zetu, sio kupinga kwa mihemko. Haiwezekani serikali ya CCM inatunga sheria zinazo entertain ushoga na haitaki kuzibadilisha, halafu akina Bashite wakipata mihemko wanajitokeza hadharani kujifanya wanapinga ushoga. Hiki ni kichekesho.

Lissu anachosema badilisheni sheria kwanza. Kumbuka Lissu ni mwanasheria na ni mtu wa principles. Hata kwenye madini alisema kwa logic ileile aliyosemea ushoga. Kwamba kama tunataka kufaidi rasilimali za madini tubadili sheria kwanza, sio kwa mihemko. Serikali ya CCM ilitunga sheria ya kuwaruhusu wawekezaji wa madini kuchukua 96% ya gross income na watanzania kuambulia 4% tu. Halafu JPM anatoka hadharani na kusema tumeibiwa sana, wakati nae alikuwa sehemu ya wabunge wa CCM waliopitisha sheria hiyo kwa kura nyingi za ndioo. Maajabu.!

Lissu akamwambia badili kwanza sheria, bila kubadili sheria hatuwezi kupambana na hao wawekezaji. Wakienda mahakamani watatushinda. Akaonekana adui. Matokeo yake sote tunayajua. Hakuna cha Noah 7 tulizoahidiwa kwa kila mtanzania, wala Bajaj moja. Sheria zimebaki zilezile, wawekezaji wanaendelea kupiga 96% ya gross income, na sisi tunaendelea na kiki za kisiasa. Business as usual.

Jambo la 3 ambalo CCM wote wanashangilia kama mazuzu ni namna Stephen Sackur alivyokua akiuliza maswali. CCM wanadhani Steve anamuunga mkono JPM ndio maana akauliza maswali ya kumprovoke Lissu. Hadi kachakubanga kamempost Steve na kusema ni mwanachama mpya wa CCM. Nikacheka sana halafu nikaishia kukaonea huruma, labda kwa sababu ya utapiamlo utotoni huenda kaliathirika sehemu ya ubongo inayosaidia kureason.

Msingi wa kipindi cha HardTalk ni provocation. The Q&A session its a provocative interview. Yani host wa kipindi anatafuta facts zote muhimu za kukuprovoke. Ndio maana viongozi wengi wakienda pale wanaishia tu kupanick na kuondoka.

The host of HardTalk show is always in opposite angle of the interviewee. Yani akienda JPM leo kuhojiwa, Steve atatafuta facts zote za upande wa opposition na atamuuliza maswali very provocative, kiasi kwamba unaweza kuhisi ametumwa na Chadema. The same way akienda kiongozi wa upinzani, atatafuta facts za upande wa serikali akupige nazo hadi uhisi ametumwa na serikali. Hivi ndivyo kipindi kilivyo kwa yeyote anayeenda kuhojiwa. Lengo ni kukufanya uumize kichwa na kutoa majibu yenye weledi. Ndio maana kipindi kinaitwa HardTalk na sio Futuhi.

Kwahiyo Chakubanga kumuita Steve mwanachama mpya wa CCM ni ulimbukeni tu. Leo JPM akiitwa kwenye Hardtalk (japo hana standard ya kuitwa) Chakubanga huyohuyo atasema Steve ni mwanachama wa Chadema tena mjumbe wa kamati kuu. Maana kwa maswali atakayopigwa lazima Chakubanga aseme maswali hayo yaliandaliwa na sekretarieti ya Chadema. Kwahiyo tumuonee tu huruma, huenda hiki ndio kipindi chake cha kwanza cha Hardtalk kukitizama, au huenda aliugua pepopunda utotoni. Tumsamehe.!

Malisa GJ
That courage of supporting homosexuality, is nowhere to be found in this country. Usiseme ndani ya CCM tu, bali Tanzania nzima maana hata walio mashoga, wanajificha.
Aliulizwa aseme Yes or No! Akaulizwa mara ya pili; Yes or NO! mara ya tatu akapewa maelezo kidogo na kutakiwa aseme Yes or No! aah! Maelezo meeengi deductively akamaanisha YES!! We unatuletea tafsiri ya kiswahili kireefu. Kamateni mtu wenu mdomo. ni mrefu bila sababu.
 
Akili za watu wa lumumba
That courage of supporting homosexuality, is nowhere to be found in this country. Usiseme ndani ya CCM tu, bali Tanzania nzima maana hata walio mashoga, wanajificha.
Aliulizwa aseme Yes or No! Akaulizwa mara ya pili; Yes or NO! mara ya tatu akapewa maelezo kidogo na kutakiwa aseme Yes or No! aah! Maelezo meeengi deductively akamaanisha YES!! We unatuletea tafsiri ya kiswahili kireefu. Kamateni mtu wenu mdomo. ni mrefu bila sababu.
 
Lile swali la mtego tena waliliacha mpaka dakika za majeruhi

Kifupi ushindi wa Lissu ulijikita zaidi katika kujibu swali la ushoga binafsi ningekuwa ni mimi hakika ningechemsha sijui ningejibu nini zaidi ya kubabaika na kutokwa na jasho jingi na kumwomba mwendasha kipindi tumalize haraka.

Majibu ya Lissu yalijikita katika sheria zetu wenyewe na si vinginevyo.
 
Back
Top Bottom