Malisa Godlisten: Nape akae kimya, hana locus ya kuilaumu CCM wakati bado yupo humo

Malisa nae anasumbuliwa na mihemko ya kichama, kwa hiyo waliopo nje ya ccm ndio wana haki ya kuikosoa serikali!?
 
Nape hana akili

hakumuona Kilango au wengine ambao wako cool!!

kosa lake lilikuwa so obvious na la kitoto kabisa kutaka sifa kwa watu na hautimizi lengo la kumuondoa muhusika

vita ingine unajifanya umepigwa huku unajipanga kumuondoa mtu kiaina
Hakujua kama anafurahisha genge fulani lenye maslahi yake, na sio lina uchangu na nchi hii.!
 
Ccm mtamkumbuka Nape. Ukitaka kujua umuhimu wa Nape mruhusuni Kinana aongee, kwann mnamtuma kutibiwa India?
 
ya MUNGU mpe MUNGU na ya KAISALI mpe KAISALI

kunasomo nalipata ukiwa kibashite kazi ako ni kusifia hata kama unaemsifia kakosea

NAPE kinachompatia kushindwa kusimamia haki na kweli pasipo kuagalia masilahi ya lumumba

ushauri kwa NAPE aendelee kusimamia kweli daima hata akiteuliwa tena uwazr

na wanalumumba mwengine akinyolewa zako tia maji kazi kwenu

yaliyompata NAPE kwa awamu hii yatakuwa ndo habari ya mjini
 
Nape alishaambiwa mara elfu lele ulela anyamaze lakini ilishashindikana. Siku ya kwanza tu baada ya kutenguliwa uwaziri aliamua kuitisha press conference ili aseme. Alikataliwa asiitishe hiyo press conferense lakini alikataa kutii amri ya kukaa kimya. Ilibidi nguvu kiasi itumike kumfanya anyamaze lakini wapi. Hadi ikafikia kuonyeshwa ka mguu ka kuku lakini bado alikataa kunyamaza.

Kwa hiyo hata humu Jf hata tumsihi vipi Nape hawezi kunyamaza. Yeye anasema ni mmakonde, yaani ukisimama nchale, ukikaa nchale, ukilala nchale hata ukifanyaje nchale tu utapigwa. Hatuna cha kufanya. Nape ataendelea tu kutupiga nchale mpaka tukome.
 
Kutoka kwa Malisa Godlisten
Kwanini Nape anaweweseka? Naona tangu ametimuliwa uwaziri hayupo sawa kichwani. Namshauri ni vema angekaa kimya kuliko kuongea ongea vitu vinavyozidi kumpunguzia credits. Nape ameanza kuilaumu na kuikosoa serikali kwa mambo ambayo yalifanyika yeye akiwa serikalini.

Kwa mfano suala hili la wananchi kunywa maji taka, Nape anailaumu serikali leo, kana kwamba wameanza kunywa maji haya baada ya Nape kufukuzwa uwaziri. Haya maji wananchi wamekunywa kabla Nape hajawa waziri na hata akiwa waziri. Lakini jambo hili halikumgusa akiwa waziri, leo amefukuzwa ndio anajifanya kuguswa?
Mi nadhani Nape alikua ana nafasi nzuri ya kuwasaidia watu hawa akiwa waziri kuliko sasa akiwa Mbunge. Hizi kelele anazopiga kwa sasa angepiga akiwa Waziri pengine wananchi hawa wangesaidika.

Jambo jingine ni kuhusu miezi 38 anayoitaja Nape kuwa aliishi maisha magumu. Intention yake ni kutafuta sympathy?? Kama ni hivyo amekosea sana. Wa kuhurumiwa si yeye aliyeishi hayo maisha kwa miezi 38 tu, bali wa kuhurumiwa ni wananchi walioishi hayo maisha kwa kipindi chote tangu kuzaliwa.

Pia Nape hapaswi kulalamika kwa kuwa alikua anatekeleza sehemu ya JD yake ya ajira kama Katibu Uenezi. Mimi nikienda vijijini kikazi siwezi kulalamika kwa sababu natekeleza wajibu wangu. Sasa Nape analia nini wakati kwenda kwake huko vijijini alilipwa mshahara, posho, mafuta ya gari, dereva, na marupurupu mengine. Kwanini analia kwa jambo ambalo lilikua sehemu ya ajira yake? Angeenda kwa kujitolea ningeona mantiki ya yeye kulalamika. Lakini kama alikua anatekeleza sehemu ya ajira yake, kulalamika itz non sense.

Mwisho nimshauri Nape AKAE KIMYA kwa sababu hana locus ya kuilaumu CCM wakati bado yupo humo. Kama anaona hawezi kukaa kimya basi ajiondoe CCM ajiunge na chama kingine ili apate moral authority ya kuipiga CCM. Huwezi kulalamika kuugua kipindupindu wakati unaishi karibu na dampo na hutaki kuhama. So its either Nape aondoke CCM, au abaki lakini AKAE KIMYA MILELE.!
kwani wakati aliposema kuna mawaziri mzigo alikuwa chama gani ?
 
Kwanini Nape anaweweseka? Naona tangu ametimuliwa uwaziri hayupo sawa kichwani. Namshauri ni vema angekaa kimya kuliko kuongea ongea vitu vinavyozidi kumpunguzia credits. Nape ameanza kuilaumu na kuikosoa serikali kwa mambo ambayo yalifanyika yeye akiwa serikalini.
point
 
Jambo jingine ni kuhusu miezi 38 anayoitaja Nape kuwa aliishi maisha magumu. Intention yake ni kutafuta sympathy?? Kama ni hivyo amekosea sana. Wa kuhurumiwa si yeye aliyeishi hayo maisha kwa miezi 38 tu, bali wa kuhurumiwa ni wananchi walioishi hayo maisha kwa kipindi chote tangu kuzaliw
mkuu nime like lkn nikaona haitoshi...jamaa analia kwassbbu ya 38days?????ss tunaliaga mpaka tunaona ni haki yetu kuteswa na polisi,kulala njaa , kulala nje kwenye mabaki ya nyumba zetu zilizobomolewa , kwenda shule uniform imechanika kwenye tako...inasikikitisha sanaa kweli ccm madaraka ya kulevya
 
Mahali pekee palipo salama siku zote ni kwenye ajira ya kudumu (serikalini / mashirika /asasi mbalimbali,nk). Ajira ya kuchaguliwa au kuteuliwa (ajira kwenye siasa), siku zote sio salama na wakati wowote huweza kukuacha solemba!
Aidha huwa nawashangaa wasomi wanaoacha kazi za taaluma zao na kukimbilia siasa. Au ni kwa sababu ya matumaini waliyokuwa nayo juu ya posho za safari za ndani na nje na nyinginezo kabla huyu mheshimiwa hajashika hatamu na kuvizuia?
Jiulize!
 
Jambo jingine ni kuhusu miezi 38 anayoitaja Nape kuwa aliishi maisha magumu. Intention yake ni kutafuta sympathy?? Kama ni hivyo amekosea sana. Wa kuhurumiwa si yeye aliyeishi hayo maisha kwa miezi 38 tu, bali wa kuhurumiwa ni wananchi walioishi hayo maisha kwa kipindi chote tangu kuzaliw
Wabongo...mna"mchenjia" tena, wakati mlimjaza upepo wa kutosha asigane na wenzake!
 
Wabongo...mna"mchenjia" tena, wakati mlimjaza upepo wa kutosha asigane na wenzake!
na akiendelea kuandika andika chuki zake kwenye social media ndo atachenjiwa mpaka ashangae,wenzake waliokaa kimya ni wajinga eeeh?yy ndo anajifanya mjuaji eeeh,washauri wake muelezeni yy bado kijana mdogo sana bora akae kimya.
 
ANAYEVURUGA NCHI NI BASHITE, AKITOKA MAENEO MENGI YATATULIA.

Sio kwa aina ya wtz kama nyie hata Harmorapa maarufu. Mtz sio mtu wa kazi ni majungu. Mitandao imeonyesha ni aina gani ya watu. Sisi. Ona wakina Zitto nk. Watz. Hatujui tunataka nini na nani. So wala usitudanganye. Sisi na wakinadada wa ngomani hatuna tofauti. So kama wewe ni kiongozi fuata Ilani yenu. Na bahati mbaya hakuna maendeleo yatakayoonekama kwa miaka 5 sembuse 2. tushukuru tu kwanza tuna Rais Hana deal. Mkali. Ana msimamo. Na anajua anachotaka. Hayumbishwi na wapiga debe kama nyie. Wabunge hawana ajenda wanamatukio. Nchi gani hii.
 
Kutoka kwa Malisa Godlisten
Kwanini Nape anaweweseka? Naona tangu ametimuliwa uwaziri hayupo sawa kichwani. Namshauri ni vema angekaa kimya kuliko kuongea ongea vitu vinavyozidi kumpunguzia credits. Nape ameanza kuilaumu na kuikosoa serikali kwa mambo ambayo yalifanyika yeye akiwa serikalini.

Kwa mfano suala hili la wananchi kunywa maji taka, Nape anailaumu serikali leo, kana kwamba wameanza kunywa maji haya baada ya Nape kufukuzwa uwaziri. Haya maji wananchi wamekunywa kabla Nape hajawa waziri na hata akiwa waziri. Lakini jambo hili halikumgusa akiwa waziri, leo amefukuzwa ndio anajifanya kuguswa?
Mi nadhani Nape alikua ana nafasi nzuri ya kuwasaidia watu hawa akiwa waziri kuliko sasa akiwa Mbunge. Hizi kelele anazopiga kwa sasa angepiga akiwa Waziri pengine wananchi hawa wangesaidika.

Jambo jingine ni kuhusu miezi 38 anayoitaja Nape kuwa aliishi maisha magumu. Intention yake ni kutafuta sympathy?? Kama ni hivyo amekosea sana. Wa kuhurumiwa si yeye aliyeishi hayo maisha kwa miezi 38 tu, bali wa kuhurumiwa ni wananchi walioishi hayo maisha kwa kipindi chote tangu kuzaliwa.

Pia Nape hapaswi kulalamika kwa kuwa alikua anatekeleza sehemu ya JD yake ya ajira kama Katibu Uenezi. Mimi nikienda vijijini kikazi siwezi kulalamika kwa sababu natekeleza wajibu wangu. Sasa Nape analia nini wakati kwenda kwake huko vijijini alilipwa mshahara, posho, mafuta ya gari, dereva, na marupurupu mengine. Kwanini analia kwa jambo ambalo lilikua sehemu ya ajira yake? Angeenda kwa kujitolea ningeona mantiki ya yeye kulalamika. Lakini kama alikua anatekeleza sehemu ya ajira yake, kulalamika itz non sense.

Mwisho nimshauri Nape AKAE KIMYA kwa sababu hana locus ya kuilaumu CCM wakati bado yupo humo. Kama anaona hawezi kukaa kimya basi ajiondoe CCM ajiunge na chama kingine ili apate moral authority ya kuipiga CCM. Huwezi kulalamika kuugua kipindupindu wakati unaishi karibu na dampo na hutaki kuhama. So its either Nape aondoke CCM, au abaki lakini AKAE KIMYA MILELE.!

Sasa Hii ndiyo sababu nchi inarudi nyuma kwaajiri ya vitisho na kunyamazisha watu. Nape Ana haki ya kusema bila ya kuhama chama, bora tu anayoyatetea yanaukweli. Ukiwa kwenye chama sio lazima ukubali yote yafanywao. Vitendo vinafanywa na watu, sio chama na kuwalaumu watu hao wanaofanya makosa wanachama wa CCM hiyo ndiyo demokrasia ya kutetea ukweli. Huwezi kumuona mtoto wako anamudhuru mtu na ukakaa kimya kwa kuwa ni mtoto wako huo sio uungwana. Haki itetewe hata kama ni chama chako kinachovunja haki hiyo. Nape hana haja ya kuhama kwa akili hii, tafadhari mpe Nape nafasi yake ya kuzungumza bila ya vitisho. Nchi zilizoendelea huwa sometimes wanachama wana vote kinyume cha chama chao ikiwa hawakubaliani na chama chao, huku wako kwenye chama. Lazima Watanzania tukubali kutofautiana hata kama tuko kwenye chama kimoja, hayo ndiyo maendeleo ya kuinjenga nchi hii, mutindo wa kusema ndiyo muheshimiwa usoni moyoni Unanung'unika ni kuirudisha nchi nyuma.
 
na akiendelea kuandika andika chuki zake kwenye social media ndo atachenjiwa mpaka ashangae,wenzake waliokaa kimya ni wajinga eeeh?yy ndo anajifanya mjuaji eeeh,washauri wake muelezeni yy bado kijana mdogo sana bora akae kimya.
(Red) Mimi simo
 
Hapa kuna mambo mawili. Kwanza, uhuni aliofanyiwa Nape siku alipotaka kuongea na waandishi habari umemuathiri sana kisaikologia kwa sababu hakutarajia kiongozi wa CCM kama yeye angefanyiwa kitu kama hicho. Siku zote Nape amekuwa anaamini kuwa wanasiasa wa upinzan ndio wanastaili kufanyiwa unyama kama huo. Kwa mfano, Lema na Lissu walivyobebwa mzombe-mzombe wakiwa bungeni, kusafirishwa kupelekwa mikoa mingine na kuswekwa lupango Nape aliona hiyo ilikuwa staili yao. Double standards!

Lakini jambo la pili na la kufurahisha ni kwamba hakika sasa Nape ametambua kuwa nchi hii ina mfumo mbovu wa kiutawala ambao mbali na kudumaza maendeleo, pia unaominya demokrasia na haki za raia. This is "one giant leap" for Nape! Kwa vile Nape amelitambua hili na ni mwakilishi wa wananchi, sioni mantiki yoyote ya kumziba mdomo asiongee eti kwa vile bado yuko CCM. Ukiwa CCM ukae kimya unapoona kuna uovu umefanywa na serikali ya CCM? Ukae kimya unapoona serikali haishughullikii matatizo ya wananchi inavyopaswa? No! No! No!

A luta continua Nape!
 
Back
Top Bottom