Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Kutoka kwa Malisa Godlisten
Kwanini Nape anaweweseka? Naona tangu ametimuliwa uwaziri hayupo sawa kichwani. Namshauri ni vema angekaa kimya kuliko kuongea ongea vitu vinavyozidi kumpunguzia credits. Nape ameanza kuilaumu na kuikosoa serikali kwa mambo ambayo yalifanyika yeye akiwa serikalini.
Kwa mfano suala hili la wananchi kunywa maji taka, Nape anailaumu serikali leo, kana kwamba wameanza kunywa maji haya baada ya Nape kufukuzwa uwaziri. Haya maji wananchi wamekunywa kabla Nape hajawa waziri na hata akiwa waziri. Lakini jambo hili halikumgusa akiwa waziri, leo amefukuzwa ndio anajifanya kuguswa?
Mi nadhani Nape alikua ana nafasi nzuri ya kuwasaidia watu hawa akiwa waziri kuliko sasa akiwa Mbunge. Hizi kelele anazopiga kwa sasa angepiga akiwa Waziri pengine wananchi hawa wangesaidika.
Jambo jingine ni kuhusu miezi 38 anayoitaja Nape kuwa aliishi maisha magumu. Intention yake ni kutafuta sympathy?? Kama ni hivyo amekosea sana. Wa kuhurumiwa si yeye aliyeishi hayo maisha kwa miezi 38 tu, bali wa kuhurumiwa ni wananchi walioishi hayo maisha kwa kipindi chote tangu kuzaliwa.
Pia Nape hapaswi kulalamika kwa kuwa alikua anatekeleza sehemu ya JD yake ya ajira kama Katibu Uenezi. Mimi nikienda vijijini kikazi siwezi kulalamika kwa sababu natekeleza wajibu wangu. Sasa Nape analia nini wakati kwenda kwake huko vijijini alilipwa mshahara, posho, mafuta ya gari, dereva, na marupurupu mengine. Kwanini analia kwa jambo ambalo lilikua sehemu ya ajira yake? Angeenda kwa kujitolea ningeona mantiki ya yeye kulalamika. Lakini kama alikua anatekeleza sehemu ya ajira yake, kulalamika itz non sense.
Mwisho nimshauri Nape AKAE KIMYA kwa sababu hana locus ya kuilaumu CCM wakati bado yupo humo. Kama anaona hawezi kukaa kimya basi ajiondoe CCM ajiunge na chama kingine ili apate moral authority ya kuipiga CCM. Huwezi kulalamika kuugua kipindupindu wakati unaishi karibu na dampo na hutaki kuhama. So its either Nape aondoke CCM, au abaki lakini AKAE KIMYA MILELE.!