Malisa GJ: Rais Samia anawakaanga MATAGA

Malisa GJ: Rais Samia anawakaanga MATAGA

Hapa Dj Mbowe ameumia sana kuona Mama Samia hayuko tayari kumsaliti Magufuli.
Mbowe amefoka Twita kwa uchungu sana.
Sidhani kama ataenda kwenye hicho kikao atakachoitwa ikulu.

Nyumbu ni nyumbu kwa akili ya Malisa anqdhqni Samia ni rais anayetokana na Chadema!!!

Key point: Samia si Magufuli.

Kwa Watanzania haijalishi chama gani kiko madarakani almuradi Rais aliyepo ana kiwango kikubwa cha ustaarabu.
 
Vijana wa CHADEMA sometimes inasikitisha tu.

CHADEMA ya kina Zitto, Slaa, Mnyika, haitakuja kujirudia

Kweli kila awamu na kitabu chake.

Ukitaka kurudi huko usisahau kuwa hatimaye Slaa na Zitto wamedhihirika kuwa “wengine” tofauti na vile walivyokuwa wakati ule.

Sasa fikiria, itokee warejee CHADEMA leo na kupewa fursa zile zile kama watatenda vile vile.

Mimi binafsi sijawa nostalgic na Slaa na Zitto.

Nikikumbuka kauli aliyotoa Slaa kama KM alipomfukuza Zitto halafu mwenendo wake mwenyewe alipokuwa akiondoka CHADEMA, najiuliza sana malengo waliyokuwa/waliyo nayo nayo hawa waheshimiwa kwenye siasa za upinzani.
 
Ha

L

Halafu huyu Malisa uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana.Anachojua ni kuandika maandishi mengi yaliyojaa pumba tupu.Upupu wa Malisa ni pale anapojaribu kutuhaminisha kwa kujifariji kuwa,sasa mama SSH ,yupo pamoja na wapinzani sio mwana CCM .Huu ni ujinga na upumbavu ,mkubwa.Ni uchambuzi hewa wa ndotoni.Huyu atakuja ten,miaka minne ijayo ,akimponda mama Samia.
Nadhani badala ya kuandika PUMBA hizi, wewe ungejielekeza kupangua hoja za Malisa, moja baada ya nginne, ungeeleweka zaidi vinginevyo inaonekana unademka tu bila hoja.
 
Hapo ndo huwa nashindwa kuwaelewa CHADEMA.
U-CHADEMA unakujaje kwenye hoja hii mkuu? Kama huna cha kuandika ni bora tu ukakaa kimya badala ya kujiaibisha mbele ya great thinkers.
 
Kwa jinsi nchi inavyoongozwa kwa misinhi ya sheria, ifikapo 2025 MATAGA yatakuwa yamenyooka vizuri sana. Yatulie tu sindano ziingie kwa kuwa hakuna namna.
 
Dig Deeper-Hotuba ya Mama

Na Malisa GJ

Kimsingi mama anaisuka Tanzania mpya, lakini hataki sindano iwaume sana wale chawa wa mwendazake, hivyo anachoma halafu anawapuliza kwa kuwaambia kuwa yeye na mwendazake ni kitu kimoja.

Wakishangilia anaongeza sindano nyingine. Wakishtuka anapuliza tena anawaambia mwendo ni uleule alioacha mwendazake. Wanabwatuka tena kushangilia, anaongeza sindano nyingine. Yani mama ana akili sana.

#Mosi; Ameahidi kuimarisha uhusiano wa kimataifa na kufungua balozi mpya kwenye nchi mbalimbali. Uhusiano wetu kimataifa uliingia doa kwa miaka 6 ya mwendazake. Tulifeli ktk diplomasia. Yeyote aliyekua na mawazo tofauti na sisi tulimuita beberu. Hatukutaka kuchangamana na dunia hata vikao vikubwa kama WEF au UN hatukutaka kushiriki. Tulikosa exposure nyingi ambazo zingetusaidia kupiga hatua.

Mama kasema uhusiano utaimarishwa. Hakuna tena "blahblah" za mabeberu. Tutashirikiana na mataifa mengine kwa maslahi mapana ya Tanzania yetu. Dunia inasogea sisi hatuwezi kubaki nyuma. Kwa hiyo lazima tushirikiane na dunia lakini kwa kulinda maslahi yetu, bila kukubali masharti yatakayoharibu utu wetu. Yeyote anayetaka kushirikiana na sisi aheshimu misingi yetu ya utaifa.

Hiki ni kitu ambacho tumeshauri kwa muda mrefu lakini mwendazake hakutaka kabisa kushauriwa. Leo mama amefanya yaleyale ambayo tulishauri, lakini ili kuwapooza "chawa" akasema yeye na mwendazake ni kitu kimoja. Wakashangilia.

#Pili; Mama ameahidi kuukuza demokrasia na utawala wa sheria. Na katika kuonesha anamaanisha AMEOMBA WATANZANIA WAIKOSOE SERIKALI. Hili ni jambo kubwa sana. Yani Rais wa nchi anawaomba wananchi mkosoe serikali. Haijawahi kutokea. Mama kaweka rekodi. Mwendazake hajawahi kukubali kukosolewa, achilia mbali kuomba wananchi wamkosoe. Hiyo kwake ilikua "future imposible tense".

Ukosoaji ulikua ni dhambi kubwa hata kama unakosoa kwa nia njema. Muulize mdogo wangu Kumbusho Dawson alipokosoa ujenzi wa mabweni baada ya kupata nyufa nini kilimtokea? Kuna watu wamefungwa wengine wamepigwa, na kufanyiwa vitendo vya kikatili kwa sababu tu ya kukosoa serikali.

Leo Mama kasema kukosoa ruksa. Hii ni ishara kwamba anapenda mawazo mbadala. Kwahiyo wakosoaji tumepewa ruksa ya kujiachia ili mradi tusivunje sheria za nchi. Tukosoe kwa misingi ya kujenga (constructive critisism). Hii ni sindano kali kwa chawa lakini ili kuwapooza akawaambia mimi na mwendazake ni kitu kimoja. Wakashangilia.

#Tatu; Mama kaonesha nia ya maridhiano kwa kukubali ombi la viongozi wa upinzani kukutana nae. Amesema atakutana nao muda mfupi kuanzia sasa. Hii ni habari njema maana nchi hii ni yetu sote na inahitaji mawazo ya kila upande ili kupiga hatua. Wakati wa mwendazake kuna watu walijimilikisha nchi. Wakajiona wao ni wenye nchi na wengine ni wapangaji. Wakaamini wao ndio wenye haki ya kutoa maoni, na si mtu mwingine yeyote.

Sasa Mama kasema atakutana na viongozi wa upinzani kwa ajili ya maridhiano, ili tusonge mbele tukiwa wqmoja. Nachowashauri kwenye meza ya maridhiano wasisahau Katiba mpya. Mchakato uendelee pale kwenye rasimu ya Warioba. Akifanya hivyo ataacha legacy kubwa sana kwa taifa hili. Katiba mpya pia itatupa Tume huru ya uchaguzi na mengine mengi kwa maslahi ya taifa letu.

Mwendazake hakutaka maridhiano kabisa na hata viongozi wa upinzani walipomuomba kukutana nae aliwapuuza. Chawa wakatukana upinzani eti mlizoea kuitwa Ikulu kwenda kunywa juice wakati wa JK lakini JPM hana muda huo, yuko busy kujenga SGR. Sasa mama kasema SGR itajengwa na Ikulu tutaitwa. Na safari hii hatutakunywa juice tu, hadi futari tutakula. Na tukitoka tutawaambia mama na mwendazake ni kitu kimoja ili mpige nduru 🤣.

#Nne; Mama amevihakikishia vyombo vya habari uhuru wao. Mambo ya waandishi kukamatwa, kupigwa, kutekwa, yamefika mwisho. Vyombo vipo huru kuandika na kuripoti habari yoyote yenye maslahi kwa taifa ili mradi vinafuata sheria za nchi. Mwendazake alizika kabisa uhuru wa vyombo vya habari, tangu alipowaambia "hamna freedom to that extent". Mama kafungua huo mnyororo rasmi kuanzia leo.

#Tano; Mama ameahidi kuboresha maslahi ya watumishi wa umma, kwa kupandisha vyeo na mishahara. Huu ni mfupa uliomshinda mwendazake. Kwa zaidi ya miaka 6 watumishi hawakupandishwa madaraja wala kuongezewa mshahara. Kila walipolalamika walijibiwa kwa kejeli kama hawataki kazi waache.

RC mmoja akasema eti angewachapa viboko. Unamchapaje viboko mtu anayedai haki yake ya kisheria? Nyongeza ya mshahara sio huruma ya kiongozi ni matakwa ya kisheria. Lakini watumishi wamedhulumiwa haki hiyo kwa miaka 6 bila huruma. Sasa mama amesema imetosha. Ameamua kuwafuta machozi.

Sambamba na hilo mama pia ameahidi ajira mpya. Katika ajira hizo walimu ni 6,000. Hapa ningependa nimshauri kidogo. Kwanini serikali inataka kuajiri walimu 6,000 wakati mahitaji ni 40,000? Idadi ya walimu waliohitimu tangu mwaka 2015 hadi sasa ni 45,000, deficit ya walimu ni 40,000. Sasa kwanini ajira 6,000? Si waajiriwe tu wote?

#Sita; Kuhusu uwezeshaji kwa vijana mama amesisitiza halmashauri ziendelee kutenga 10% ya bajeti yake kwa ajili ya mikopo kwa vijana na wenye ulemavu. Hapa ningemshauri aunde timu ya ufuatiliaji. Je halmashauri ngapi hufanya hivyo? Na je hufanya kwa kiwango kinachotakiwa? Kwa mfano kwa mwaka wa fedha 2019/20 halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilipitisha bajeti ya Bilioni 48, ambapo Bilioni 4.8 zilipaswa kutengwa kwa ajili ya vijana. Lakini kiasi kilichotengwa kwa ajili ya vijana hakifiki hata 500M. Kuna haja ya ufuatiliaji.

#Saba; Kuhusu ATCL mama amekubali kuwa shirika linajiendeaha kwa hasara, sawa na ripoti ya CAG inavyosema. Hii ina maana zile story za mwendazake kwamba ATCL inapata faida hadi inatoa gawio serikalini zilikua drama tu. Mama ameahidi kuliwezesha shirika kwa kuliongezea mtaji, na kulifutia baadhi ya madeni ili lijiendeshe kwa tija.

Hii ndio sifa ya kiongozi bora. Unakubali penye mapungufu na unaweka mipango ya kusolve mapungufu hayo. Sio unatupiga sound kwamba shirika linatoa gawio wakati lipo hoi bin taaban.

#Nane; Mama amezungumzia kifo cha Magufuli. Amesisitiza tena kwamba kilitokana na tatizo la moyo na si vinginevyo. Amesema kuna watu wanaotoa taarifa za uchonganishi mitandaoni kuhusu kifo cha Magufuli. Amewataka watu hao waache mara moja uchonganishi huo.

Wengi tumesikia wachonganishi hao ambao wamejirekodi sauti na kusambaza kwenye mitandao wakitunga "hadithi" kuhusu hicho. Bila shaka watu hao ni wale waliomtumaini JPM kwa moyo na akili zao zote na kudhani hawezi kufa. Wakasahau kwamba nae ni mwanadamu kama sisi.

Watu hao kwa sasa wapo kwenye "denial" na ndio wanahaha kutunga story za kuchonganisha viongozi. Mama amewaomba muache. Kumbukeni ombi la mama ni amri. Sasa kama hamtaki kusikia msije kujilaumu. Achaneni na hizo drama. Ukurasa wa JPM umeshafungwa na sasa ni zamu ya Samia. Tumpe nafasi!
Nafikiri yeye huyo GJ Malisa ndiye aliyepoteza dira badala ya kuelezea falsafa za CDM kwa maandalizi ya kushika dola unajitwisha zigo la CCM usilolijua limebeba kitu gani ukiwa unachumwa kichwani lakini hausemi kama unaumia. Changamoto za Chama tawala, Rais na wanachama wake ni za kwao muda wakipatana utapata aibu ya mwaka.

Usifikiri kujipendekeza kutakuleta kwenye himaya hiyo ni hadithi ya alinacha
 
Nafikiri yeye huyo GJ Malisa ndiye aliyepoteza dira badala ya kuelezea falsafa za CDM kwa maandalizi ya kushika dola unajitwisha zigo la CCM usilolijua limebeba kitu gani ukiwa unachumwa kichwani lakini hausemi kama unaumia. Changamoto za Chama tawala, Rais na wanachama wake ni za kwao muda wakipatana utapata aibu ya mwaka.

Usifikiri kujipendekeza kutakuleta kwenye himaya hiyo ni hadithi ya alinacha
Hayo ni yako. Ninachojua ni kwamba Malisa GJ ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii na amekuwa akichambua bila kujali misingi ya itikadi za vyama. Labda humjui vizuri umeamua tu kudemka jinsi unavyojisikia.
 
Hayo ni yako. Ninachojua ni kwamba Malisa GJ ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii na amekuwa akichambua bila kujali misingi ya itikadi za vyama. Labda humjui vizuri umeamua tu kudemka jinsi unavyojisikia.
Eti simjui yeye ni nani, unatishia sio au unajaribishia kina cha maji? Huyo mtu wako unayemjibia kwa niaba yake hana ujuzi wowote wa kuchambua chochote kilichopo hapa duniani.
 
Eti simjui yeye ni nani, unatishia sio au unajaribishia kina cha maji? Huyo mtu wako unayemjibia kwa niaba yake hana ujuzi wowote wa kuchambua chochote kilichopo hapa duniani.
Kwa hiyo unataka kusema kwamba Malisa GJ si mchambuzi wa masuala ya kisiasa mkuu? Anachambua masuala gani? Labda wewe unamfahamu kuliko watanzania wengine. Hebu tuambie tuelewe.
 
naamini ukosoaji ukizidi kuliko uwezo wa kujirekebisha na kuficha makosa ya kukosolewa.

Watu watabinywa tu kwa kuchoma sindano na kupuliza kama awamu za nyuma kabla ya Baba lao.

Hakunaga nchi kila mtu anabwabwaja tu alafu anaangaliwa. Tofauti ni jinsi anavyonyamazishwa tu. Hata snowden na assange walishughulikiwa na baba la demo
Irrelevant story.
 
Vijana wa CHADEMA sometimes inasikitisha tu.

CHADEMA ya kina Zitto, Slaa, Mnyika, haitakuja kujirudia

Kweli kila awamu na kitabu chake.
Sindano imegusa mfupa, Huna wa kumwimbia pambio, ulimtegemea mwanadamu na mwanadamu huyo amefutika. Pole, hizi ni zama za Samia.
 
Rais Samia mara zote anasema anaendeleza yale yaliyofanywa na Hayati Magufuli na katika kukazia hilo akasisistiza kwa kusema kwa Yeye na JPM ni wamoja. Kama ndivyo huyu kijana wa mwenyekiti asiyepingwa anapata wapi ujasiri wa kusema hayakuwepo enzi za Magufuli? Nilichogundua ni kwamba Magufuli alikuwa hapendi siasa za choko choko mchokonoe akikugusa kakuonea akikuacha kakuogopa
Baki, huko kwa mwendazake. Lkn tambua hizi ni zama za Samia na mambo hayatakua yale tena. Endelea kupumbazika na kauli za SSH kwamba yeye ni kitu kimoja na yule bedui huku marekebisho yakifanyika na legacy ya yule ikiyeyuka.

Vipi, ATCL mwaka huu wametoa gawio.
 
Back
Top Bottom