Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,194
- 4,115
Kuhusu Mbarikiwa Mwakipesile,
1. Amepinga vikali mkataba wa "kinyonyaji" wa bandari kupitia mahubiri yake. Kufungwa jela kunaweza kutafsiriwa ni kwa sababu ya kupinga mkataba huo kama ilivyokuwa kwa Wakili Mwabukusi, Mdude, Dr.Salaa etc.
2. Hoja ya kuendesha Kanisa ambalo halijasajiliwa ni mufilisi kwa sababu ameendesha kanisa hilo kwa miaka mitatu. Serikali ilikua wapi miaka yote wasimkamate, mpaka alipopinga mkataba wa bandari ndio wakashtuka Kanisa halijasajiliwa?
3. Mbarikiwa amewahi kuwaalika viongozi mbalimbali kushiriki ibada Kanisani kwake wakiwemo maDC, wabunge na viongozi wa taasisi za umma. Je wote hao hawakushtuka kuwa Kanisa halijasajiliwa?
4. Je asingepinga mkataba wa bandari serikali ingeendelea kumvumilia aendeshe kanisa lisilosajiliwa kama ilivyomvumilia kwa miaka mitatu?
5. Mwanae Sarah alitunga wimbo "Mnatuona Manyani" akikosoa vikali mkataba "wa kimangungo" wa bandari. Akakamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi. Je haya aliyofanyiwa baba, sio mwendelezo wa aliyofanyiwa mtoto?
6. Mwenendo wa kesi unatia mashaka. Hakimu ameendesha kesi kwa masaa mawili tu akamtia hatiani na kumtandika mvua ya miaka mitatu jela. Sijawahi kuona kesi ikiendeshwa kwa speed kiasi hiki.
7. Mbarikiwa alikua kwenye process za kusajili Kanisa lake na documents zipo serikalini. Kwa mujibu wa sheria, kama umeshaanza process huwezi kufungwa. Badala yake serikali inaweza kusimamisha huduma mpaka upate vibali ndio uendelee.
8. Suguye amewahi kufungiwa Kanisa lake kwa madai ya kutosajiliwa. Lakini hakukamatwa wala kushtakiwa. Badala yake alishughulikia vibali na alipokamilisha aliruhusiwa kuendelea na huduma. Sasa kwanini imekua tofauti kwa Mbarikiwa?
9. Mtu anayeanzisha Kanisa ana lengo la kupunguza maovu kwenye jamii na kuwafanya watu wamrudie Mungu wao. Mtu mwenye lengo zuri kama hili, unamfungaje jela kisa tu hajasajili? Kwanini usimsaidie aweze kupata vibali? Kanisa sio danguro hadi watu waogope kuanzisha.
10. Mama kwa unyeyekevu nakushauri punguza chawa. Wameanza kukupanda kichwani. Wanaumiza watu wakidhani wanakufurahisha. Kumbe wanakujengea chuki kwa jamii. Ukija kushtuka 2025 hii hapa. Utaomba maji kwa karai my friend.!