Malipo ya Upimaji Viwanja ni Halali au Rushwa?


Mrimi

Mrimi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Messages
1,703
Likes
103
Points
160
Mrimi

Mrimi

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2011
1,703 103 160
Nimekuwa nikikwazwa sana na malipo kwa ajili ya kupimiwa kiwanja cha kujenga nyumba ya kuishi. Nimekuwa sielewi mantiki ya malipo haya
kwani ninavyoelewa mimi ni kwamba hii ndio kazi waliyoajiriwa kufanya,kama ambavyo traffic police kazi yake ilivyo ya kufanya kazi barabarani,
hiyo ndiyo kazi yao.Na hawa watu wa ardhi kazi ya sio ni field work ndiyo ofisi yao. Ninavyoelewa mimi wanalipwa mishahara,(tena mizuri tu) na
kuna bajeti wanapata kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kiofisi za kila siku. Hapa ndio napata shida kuelewa mantiki ya haya malipo tunayotozwa.

Lkn kibaya zaidi, malipo haya sio flat rate, wanatoza kufuatana utashi bianafsi wa muhudumu utakayemkuta ofisini siku hiyo. Hata baada ya kulipia bado utalazimika kuhonga ili kuwawezesha hao maofisa kufika katika eneo la kiwanja. Hii sio haki hata kidogo kwani hata baada ya kujenga bado unalazimika kulipia kodi ya jengo.

Kutokana na kero hii watanzania walio wengi wanashindwa kuhimili gharama kubwa ya ununuaji viwanja,ujenzi na hizo kero za kipuuzi hapo juu,
matokeo yake watu wanajenga katika viwanja visivyopimwa, kisha lawama zinzwaandama kuwa hawajafuata utaratibu,kesho na keshokutwa linakuja tingatinga linabomoa- Eti serikali haijui sababu ya watu hawa kujenga bila kufuata utaratibu,hiki sio kichekesho na kebehi?
 
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,233
Likes
306
Points
180
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,233 306 180
Ndiya maana miji mikubwa hapa tanzania inajengwa kiholela, hao watu ni wahuni sana. Bahati mbaya hatuna serikali ya kuwasimamia
 

Forum statistics

Threads 1,235,629
Members 474,678
Posts 29,229,077