Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Mimi nafanya kazi Butiama katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere, wakati wa kuajiriwa, Watumishi wengi tulinunua maeneo karibu na eneo ambalo Serikali ilitazamia kujenga chuo.
Bahati nzuri tukawa tumeenda masomoni lakini tuliporudi miaka mitano baadaye tukakuta maeneo yetu yamepimwa bila sisi kushirikishwa. Tukaanzisha mchakato wa kufuatilia ili kujua imekuwaje yamepimwa na kwa jina gani bila sisi kuhusishwa.
Tulipofuatilia suala hilo kwa Afisa Mipango Mji, alitueleza kuwa upimaji ulifanyika kwa kushirikisha watu, wengi wao walikuwa Wanakijiji ingawa sisi hatukujulishwa kwa namna yoyote, hata kwa njia ya simu.
Baada ya kuchunguza, tulibaini walitaka kutumia uelewa mdogo wa Wanakijiji hao ili kurahisisha mchakato kwa maslahi wanayoyajua wao.
Tulimlalamikia Afisa Mipango kuhusu kutoshirikishwa, tukashauri mchakato huo ubatilishwe na sisi pia tuzingatiwe. Ndipo akataka tukubaliane kuwa, baada ya upimaji, tungekuwa na mgao wa Asilimia 60 kwa 40 ambapo kama eneo lilikuwa na heka 3 au 4 ambalo viwanja 10 vilipatikana, Serikali ingechukua vinne na sisi sita.
Hata hivyo, tulipinga kwa kuwa hatukushirikishwa kwenye mchakato wa awali.
Afisa Mipango aliendelea kuleta ubabe na kutueleza kuwa makubaliano yalikuwa yamepita. Akaamua kuendelea na uuzaji viwanja vilivyopimwa kwa madai kwamba walitupa nafasi ya kuchagua, ila hatukutokea.
Baada ya hapo, walitoa tangazo la kuuza viwanja katika Kitongoji cha Ikorokomyio, eneo ambalo chuo kipya kinajengwa, na sisi tuliona tangazo hilo siku moja kabla ya kuuza viwanja.
Tulipomuuliza kwa nini tangazo lilichelewa, alijibu kuwa lilichelewa kwa sababu ya matatizo ya mtandao, jambo ambalo hatukuliridhia.
Hivi sasa, watu wameanza kununua viwanja hivyo, ikiwemo na maeneo ambayo ni mali yetu, hata sisi ambao hatujakubali mchakato huo.
Unaenda pale unaonesha viwanja vyako, lakini kuna wengine ambao ndani ya vile sita pia kuna vingine vimechukuliwa tena, na hivyo kusababisha mtafaruku mzito uliojaa ubabe usio na maana.
Kitu kingine ni kwamba mtu mwenye kiwanja kimoja hachangii gharama nyingine, yeye analipia tu gharama za upimaji, ambazo si zile zinazofahamika na Serikali yaani Tsh. 130,000/-; badala yake, unapigiwa hesabu ya Tsh. 300 kwa kila mita ya mraba.
Mwenye viwanja viwili hana shida, lakini ukiwa na vitatu hadi vinne unalazimika kuachia kimoja na ukiwa na vitano unaachia viwili kwa Serikali. Hii ni sawa kweli?
Tulipendekeza kwamba, kwa kuwa hatukukubaliana na mchakato wa kwanza, tupatiwe nafasi ya kulipia tu gharama za upimaji kwa viwanja vyote sita.
Hata hivyo, waliendelea kushikilia kuwa haiwezekani kwa sababu viwanja hivyo vinachukuliwa kwa ajili ya huduma kama maji, umeme na barabara.
Tukauliza kwa misingi gani, wakati utaratibu wa huduma hizo unaeleweka ikiwa sio kazi yao? Ni ya mamlaka nyingine, bado kukawa na ugumu.