Malipo ya madaktari wa majuu - tujilinganishe

Malipo ya madaktari wa majuu - tujilinganishe

Mabishano ni mazuri lakini biased to money wakati madaktari hawalalamikii pesa kihivyo bali kwa ujumla kuhuisha huduma za afya nchini. Pesa wanayoomba kwenye budget watu wa wizara ya afya nyingi ni ya kufanyia vikao na safari za watu wa wizarani, kisha kununulia panadol MSD. Ungemsikiliza vizuri Mama SITTA kuhusu kuikata budget ya MoHSW alipoongelea matokeo ya kazi ya kamati yake ya Bunge, wala usingeweka uzito kwenye pesa za madaktari, ingawa bado alikuwa na swali - wapi budget kuhusu madai ya madaktari?
 
Naona mnafananisha Simba na Paka.

1. Daktari wa majuu anasoma kwa mkopo (mfano OSAP) akimaliza masomo analipa mkpo wake
2. Daktari wa majuu yupo dedicated hata saa saba usiku anakurupuka kwenda kutibia akihitajika.
3. Daktari wa majuu haweki tamaa mbele na haruhusiwi kugoma.
4. Daktari wa majuu anapenda kazi yake hatibii kama kazi anakuwa na passion, kama anamtibia mtoto mdogo basi ata m handle huyo mtoto kama ni wakumzaa mwenyewe.

Kule kwa wenzetu kazi ya udaktari ni wito kweli kweli na hata hizo pesa wanazolipwa ni ndogo sana kulinganisha na utendaji wao, na wao wamefundishwa kuokoa maisha popote pale walipo hata asipokuwa kazini akiona sehemu ujuzi wake unahitajika hata barabarani atatoa huduma bila kuuliza kwanza malipo au daftari la kusaini.

Acheni kufananisha Simba na Paka.
Hawa madaktari wetu wengefikia hata nusu ya utendaji kazi wa madaktari wa majuu, hakuna mtu angelalamika wao kudai 3.5m. Mimi nilimpeleka mgonjwa wangu MOI aliumia kwenye Basi, alikaa pale mwezi mzima bila huduma, mwishowe wakataka wamkate miguu yake eti haiwekani kuunga tena!!! Nilipomhamishia BURERE hospital Kibaha, miguu iliyoshindikana kuungwa MOI, imeunga na jamaa sasa anatembelea bila matatizo.
 
Ni ukweli usiofichika kuwa katika kada zote za wafanyakazi wa umma (sijumuishi waliopo kwenye Govt Agencies kama TRA,TFDA,TMAA nk maana hata kwa madaktari waliopo kwenye govt agencies kama NIMR mishahara yao ni mikubwa kuliko daktari wa kawaida) madaktari ndiyo wanaoongoza kwa malipo makubwa kuliko yeyote,pia ni ukweli kwamba mazingira ya kazi kwa madaktari hayaridhishi kama yalivyo kwa Polisi,walimu,engineers na wengio wote isipokuwa wanasiasa.Unyeti wa madai wanayoyataka hauwezi kutimizwa kwa muda mfupi sana sana mgomo wao utaendelea kutuumiza tu raia wanyonge tusio na hatia.
Jamani mwalimu anapangiwa shule kijijini hakuna nyumba ya kukaa,mshahara mwisho wa mwezi anaufuata km kadhaa,maji na umeme hakuna na watoto wanakalia mawe lakini anafanyakazi hagomi kwa kusema kuwa hawezi kuendelea kushuhudia watoto wakifeli kwa kukosa vitendea kazi muhimu kwa ufanisi wake kazini.Utasikia wanasema utalinganishaje daktari na mwalimu hii kauli huwa siipendi sana,ina chembechembe ya kujikwaza juu ya kada nyingine za watumishi wa umma ambao hata kwa sasa still madaktari wanawazidi hizo kada nyingine,kada nyingine pamoja na mishshara midogo kila mwisho wa mwezi bodi ya mikopo wanakinga bakuli uwarudishie hela zao kutoka kwenye mshahara lakini daktari alisoma bure hadaiwi hata senti toka loan's board.

Binafsi naona madaktari wanamalalamiko yao ya msingi (isipokuwa la mshahara wa mil3.5 kwa kuanzia) lakini kutumia jamii kama ndiyo nyenzo yao kuu ya kuonyesha dissatisfaction yao kwa serikali mimi sijaridhika nayo kabisa na siiungi mkono.Watafute namna ya kuiwajibisha serikali (ikiwamo kususia services wanazopata toka serikalini hata mshahara) bila kutujuisha sisi walalahoi tuliokatwa kodi ili wao wasome bure ili watuhudumie afya zetu za kuungaunga.

Swali? Kwa daktari aliyepo kwenye mgomo anastahili kulipwa mshahara na marupurupu mengine kama mfanyakazi halali wa serikali?
 
Naona mnafananisha Simba na Paka.

1. Daktari wa majuu anasoma kwa mkopo (mfano OSAP) akimaliza masomo analipa mkpo wake
2. Daktari wa majuu yupo dedicated hata saa saba usiku anakurupuka kwenda kutibia akihitajika.
3. Daktari wa majuu haweki tamaa mbele na haruhusiwi kugoma.
4. Daktari wa majuu anapenda kazi yake hatibii kama kazi anakuwa na passion, kama anamtibia mtoto mdogo basi ata m handle huyo mtoto kama ni wakumzaa mwenyewe.

Kule kwa wenzetu kazi ya udaktari ni wito kweli kweli na hata hizo pesa wanazolipwa ni ndogo sana kulinganisha na utendaji wao, na wao wamefundishwa kuokoa maisha popote pale walipo hata asipokuwa kazini akiona sehemu ujuzi wake unahitajika hata barabarani atatoa huduma bila kuuliza kwanza malipo au daftari la kusaini.

Acheni kufananisha Simba na Paka.

Lakin bila motivation hakuna utendaji mzuri sehem yoyte. ikiwa ni pamoja na mishahara mizuri, mazingira mazuri ya kazi na vitendea kazi bora na vinavyoenda na wakati, pia facility.. madawa nk... bila hivyo ni abusive ya professional. Watu kwenda INDIA sio kwamba wahindi ndio wanajua sana... hapana. Tatizo ni vifaa vya kisasa na madawa yanayofaa sio feki kama hapa kwetu.
 
Kama swala ni maslahi basi tuongelee maslahi ya watumishi wote wa umma na jinsi ya kuyaboresha sio madaktari peke yao.

Just imagine afisa masijala wa serikali nae agome kwamba mazingira magumu kule kwenye ma file kuna vumbi hawezi kwenda na mshahara mdogo. Askari nae agome vitendea kaiz hamna na hana allowance za mazingira magumu kwakuwa anashika bunduki. Bwana shamba nae agome kwamba hana usafiri na mazingira anayoishi vijijini hatarishi anatembea umbali mrefu. Bwana mipango miji agome anaingia maporini kupima viwanja anaweza kugongwa na nyoka huko. Mbunge nae agome kwamba bunge la Kenya linalipa pesa nyingi kwa wabunge na wao wanataka walipwe kama Kenya.
 
WADAU WAKATI KILA MTU ANAONGEA KIVYAKE KUHUSU MADAI YA MADAKTARI HEBU TUANGALIE JINSI KAZI ZINAZOLIPA MNO HUKO MAREKANI KUWA NI ZA MADAKTARI WENGINE WANAFUATA. NAFIKIRI HUKU KWETU - TZ MAMBO NI KINYUME. WATU WANAWEZA CHANGIA KWA KULINGANISHA NA UCHUMI NA FINANCIAL RESOURCE LAKINI POINT HAPA NI KWAMBA INATAKIWA KWA RESOURCE TULIZONAZO TUTOE VIPAUMBELE KWA KADA MUHIMU

No. 1 Best-Paying Job: Anesthesiologists
Average Annual Pay: $234,950
Employees in Field: 33,310

No. 2 Best-Paying Job: Surgeons

Average Annual Pay: $231,550
Employees in Field: 42,340

No. 3 Best-Paying Job: Obstetricians and Gynecologists

Average Annual Pay: $218,610
Employees in Field: 20,540

No. 4 Best-Paying Job: Oral and Maxillofacial Surgeons

Average Annual Pay: $217,380
Employees in Field: 5,800

No. 5 Best-Paying Job: Orthodontists

Average Annual Pay: $204,670
Employees in Field: 5,040

Tatizo kubwa ninalo liona ni kwamba Serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwaadaa WANANCHI kuwa mgomo wa madaktari ni kudai posho ama nyongeza ya mishahara wakaji jambo la msingi ni VIFAA NA MAZINGIRA BORA YA KAZI!

ZINDUKA KWENYE USINGIZ ULIOLALA
 
Madaktari wafahamu kwamba hamna haki bila wajibu.

Inabidi wakae wajitafakari wabadilike. Hata wakiongezewa pesa sidhani kama kutakuwa na impact kubwa kwenye utendaji wao maana hata huko kwenye hospitali za private ukienda kutibiwa tofauti kubwa ni majengo na facilities otherwise udaktari ni ule ule tu.

Madaktari wetu hawa wewe mgonjwa hujamaliza kumuelezea magonjwa yako yeye ameshaandika dawa bila hata kukuangalia hapo ambapo wewe unamwambia pana maumivu wala kuuliza maswali zaidi ya historia yako na hayo maumivu, ndio maana watu wengi wakiumwa hawaendi hospitali wanaanza kwa kujimezea madonge ya Malaria kama kipimo cha kuangalia kama ipo haipo.
 
Kulinganisha mishahara ya madaktari wa USA na Tanzania ni sawa na kulinganisha Paka na Tembo. Ingawa najua madai ya madaktari sio mishahara tu, lakini pia kama ungetaka kufanya ulinganifu wa mishahara ungelinganisha na nchi za ukanda wa kwetu ambazo relativelu tunafanana kiiuchumi na kijiografia mathalani, Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana, etc.

Ulinganifu wake huu POGO!
You have a point..lakini ukilinganisha mshahara wa Kikwete na Obama nani ana mshahara mkubwa?
 
Madaktari wafahamu kwamba hamna haki bila wajibu.

Inabidi wakae wajitafakari wabadilike. Hata wakiongezewa pesa sidhani kama kutakuwa na impact kubwa kwenye utendaji wao maana hata huko kwenye hospitali za private ukienda kutibiwa tofauti kubwa ni majengo na facilities otherwise udaktari ni ule ule tu.

Madaktari wetu hawa wewe mgonjwa hujamaliza kumuelezea magonjwa yako yeye ameshaandika dawa bila hata kukuangalia hapo ambapo wewe unamwambia pana maumivu wala kuuliza maswali zaidi ya historia yako na hayo maumivu, ndio maana watu wengi wakiumwa hawaendi hospitali wanaanza kwa kujimezea madonge ya Malaria kama kipimo cha kuangalia kama ipo haipo.
Je wewe kwenye kazi yako unayofanya unatimiza wajibu kama inavotakiwa?
 
Kulinganisha mishahara ya madaktari wa USA na Tanzania ni sawa na kulinganisha Paka na Tembo. Ingawa najua madai ya madaktari sio mishahara tu, lakini pia kama ungetaka kufanya ulinganifu wa mishahara ungelinganisha na nchi za ukanda wa kwetu ambazo relativelu tunafanana kiiuchumi na kijiografia mathalani, Kenya, Uganda, Rwanda, Botswana, etc.

Ulinganifu wake huu POGO!
Wewe hujaelewa nadhani. Amesema pamoja na kuwa marekani uchumi wake huwezi kulinganisha naTZ, lakini doctors should be given priority payment in TZ with available small we have. Sio mbunge amzidi daktari, no!!! Basi mshahara wao uwe ndio mkubwa kwa scale za TZ, kwa sasa hauko hivyo!!
 
WADAU WAKATI KILA MTU ANAONGEA KIVYAKE KUHUSU MADAI YA MADAKTARI HEBU TUANGALIE JINSI KAZI ZINAZOLIPA MNO HUKO MAREKANI KUWA NI ZA MADAKTARI WENGINE WANAFUATA. NAFIKIRI HUKU KWETU - TZ MAMBO NI KINYUME. WATU WANAWEZA CHANGIA KWA KULINGANISHA NA UCHUMI NA FINANCIAL RESOURCE LAKINI POINT HAPA NI KWAMBA INATAKIWA KWA RESOURCE TULIZONAZO TUTOE VIPAUMBELE KWA KADA MUHIMU

No. 1 Best-Paying Job: Anesthesiologists
Average Annual Pay: $234,950
Employees in Field: 33,310

No. 2 Best-Paying Job: Surgeons

Average Annual Pay: $231,550
Employees in Field: 42,340

No. 3 Best-Paying Job: Obstetricians and Gynecologists

Average Annual Pay: $218,610
Employees in Field: 20,540

No. 4 Best-Paying Job: Oral and Maxillofacial Surgeons

Average Annual Pay: $217,380
Employees in Field: 5,800

No. 5 Best-Paying Job: Orthodontists

Average Annual Pay: $204,670
Employees in Field: 5,040

Statistics! Statistics! Statistics!!!!!

Ukitumia takwimu vibaya unaweza kujiponza! hata kam utalinganisha na majirani zetu angalia GDP ya nchi hizo, angalia ukubwa wa Private sector, angalia historia ya sekta ya afya. Private Practices kwenye sekta ya afya inaukubwa na ushindani kiasi gani? vinginevyo tutakuwa tunalinganisha oranges and apples!

Tatizo la Tanzania siyo madai ya madaktari, au mfumo uliopo ni uwezo wa ukubwa wa uchumi kukidhi mahitaji yote ya kitaifa, kuanzia ulinzi, usalama, Public service na udogo wa wigo wa kodi kutokana na kuwepo kwa uwembamba wa sekta binafsi ya utabibu ambayo haitowi mbadala wa mishahara mikubwa kwa madaktari, na wanataaluma wengine. kwasababu nchi yetu siku si nyingi ilitoka katika ujamaa ambapo kila kitu kinafanywa na serikali, na kwa bahati mbaya sana mentality hii bado inaendelea na kila kukicha wanacnachi wanaamini kuwa matatozo yao yote yatatatuliwa na serikali. Ujamaa Legacy!

Kinachotakiwa kufanyika ni kubadilisha mtazamo, na wanasiasa wote CCM na hata hao CHADEMA waache kuwadanganya Watanzania kuwaambia kuwa mkinichaguwa matatizo yenu yatakuwa yamekwisha. WIGO wa UCHUMI NA KODI iliyopo Tanzania ya leo hawezeshi kuondoa matatizo yetu hata kam nia ipo.

Marekani wamekuwa huru tangu July 04 1776, lakini mpaka leo bado wanabishana kuhusu bima ya afya kwa wananchi wote. Ugua leo ukiwa Marekani, au Mungu apishe mbali yakukute yaliyomkuta Dkt. Ulimboka na upo Marekani na hauna Bima, Ukubwa wa Mshahara wa Dakatari wa Marekani hautakusaidia, kitakachokuokoa ni Bima yako ya Afya.

Serikali yetu inapaswa kutupia macho sekta hii na kuhakikisha kuwa vitendea kazi na kupanua wigo wa private practice kwa madaktari, lakini pia kuhakikisha hawa waliopo na hospitali zilizopo zinakidhi mahitaji ya sekta hii.

Na Watanzania kwa ujumla wanapata decent medical service kama civilized human beings.

Na nyie Madaktari hacheni siasa, fanyeni kazi, mkigoma watanzania wanakufa, mchawi wenu siyo serikali iliyopo madarakani au CCM. ni ukubwa wa Uchumi uliopo na hii si kwa Tanzania pekee yake, hata Marekani bado hili linawasumbua. Hata CHADEMA siku wakuja kutawala nchi hii Mungu apishe mbali, hawataweza kuwaongezea mishahara na kukamilisha kila kinachoitajika bila kufinya maeneo mengine ya Tanzania kama Elimu, Ulinzi, au Miundombinu, kwa hiyo tutumie hekima na Uzalenda Uchumi wa Tanzania tuliyonayo sasa hauwezi kubeba madai ya kila mmoja wetu, na kama mtu akija anakwambia hilo linawezekana anakudanganya kwani atakachofanya ni: He will rob Mwita to pay Mushi or vice versa, kumbukam kuwa hawawote ni Watanzania:-(

Msigome fanyeni kazi, siasa waachieni wanasiasa.

Na kwa kwale wanaopenda kujibu hoja kwa matusi na kebehi, uwanja upo wazi🙂)))
 
WADAU WAKATI KILA MTU ANAONGEA KIVYAKE KUHUSU MADAI YA MADAKTARI HEBU TUANGALIE JINSI KAZI ZINAZOLIPA MNO HUKO MAREKANI KUWA NI ZA MADAKTARI WENGINE WANAFUATA. NAFIKIRI HUKU KWETU - TZ MAMBO NI KINYUME. WATU WANAWEZA CHANGIA KWA KULINGANISHA NA UCHUMI NA FINANCIAL RESOURCE LAKINI POINT HAPA NI KWAMBA INATAKIWA KWA RESOURCE TULIZONAZO TUTOE VIPAUMBELE KWA KADA MUHIMU

No. 1 Best-Paying Job: Anesthesiologists
Average Annual Pay: $234,950
Employees in Field: 33,310

No. 2 Best-Paying Job: Surgeons

Average Annual Pay: $231,550
Employees in Field: 42,340

No. 3 Best-Paying Job: Obstetricians and Gynecologists

Average Annual Pay: $218,610
Employees in Field: 20,540

No. 4 Best-Paying Job: Oral and Maxillofacial Surgeons

Average Annual Pay: $217,380
Employees in Field: 5,800

No. 5 Best-Paying Job: Orthodontists

Average Annual Pay: $204,670
Employees in Field: 5,040

Hawa viongozi wetu wanatumia sana emotion katika maamuzi yao. wanajiingiza katika matata makubwa sana
 
Je wewe kwenye kazi yako unayofanya unatimiza wajibu kama inavotakiwa?

reformer,

Mimi natimiza wajibu wangu kwa muajiri wangu baada ya kutimiza nategemea na yeye atimize upande wake.

Kama nikihisi siridhiki na mwenendo wa mwajiri katika kutimiza wajibu wake au mazingira ya kazi ninatoa Resignation naenda kufanya kazi sehemu nyingine kwakuwa nina vigezo vya kutosha na uzoefu katika eneo langu.
 
kulinganisha mishahara ya madaktari wa usa na tanzania ni sawa na kulinganisha paka na tembo. Ingawa najua madai ya madaktari sio mishahara tu, lakini pia kama ungetaka kufanya ulinganifu wa mishahara ungelinganisha na nchi za ukanda wa kwetu ambazo relativelu tunafanana kiiuchumi na kijiografia mathalani, kenya, uganda, rwanda, botswana, etc.

Ulinganifu wake huu pogo!

kweli mkuu hapo kuna kitu tunamiss yaani "purchasing power parity"
 
chizi ww,uwalimu unasomea miaka mingapi?

tofauti ya 2yrs kwa gap iliyopo ni sawa lakini zaidi ya hayo ni ufisadi tu. Juzi bungeni tulisikia wabunge wakitoka mapovu kuwa ratio ya 70:30 ya bajeti haiisuki nchi kiuchumi. Mimi nakubali lakini kwa mshahara wa 3.5 kwa group la madaktari tuu basi itabidi ratio iwe 95:5 sasa hiyo ni akili au matope. Madaktari acheni visingizio. Private wanalipa hiyo hiyo 1m ya serikali acheni utoto
 
WADAU WAKATI KILA MTU ANAONGEA KIVYAKE KUHUSU MADAI YA MADAKTARI HEBU TUANGALIE JINSI KAZI ZINAZOLIPA MNO HUKO MAREKANI KUWA NI ZA MADAKTARI WENGINE WANAFUATA. NAFIKIRI HUKU KWETU - TZ MAMBO NI KINYUME. WATU WANAWEZA CHANGIA KWA KULINGANISHA NA UCHUMI NA FINANCIAL RESOURCE LAKINI POINT HAPA NI KWAMBA INATAKIWA KWA RESOURCE TULIZONAZO TUTOE VIPAUMBELE KWA KADA MUHIMU

No. 1 Best-Paying Job: Anesthesiologists
Average Annual Pay: $234,950
Employees in Field: 33,310

No. 2 Best-Paying Job: Surgeons

Average Annual Pay: $231,550
Employees in Field: 42,340

No. 3 Best-Paying Job: Obstetricians and Gynecologists

Average Annual Pay: $218,610
Employees in Field: 20,540

No. 4 Best-Paying Job: Oral and Maxillofacial Surgeons

Average Annual Pay: $217,380
Employees in Field: 5,800

No. 5 Best-Paying Job: Orthodontists

Average Annual Pay: $204,670
Employees in Field: 5,040

Tutoke ktk mgomo wa madaktari na tuongelee kama ulivyoongelea hapo juu. Nafikiri usichukulie kama ulivyochukulia bali tafuta uwiano ktk nchi hiyo hiyo with reference na fani nyingine.

angalia hapa chini
Hi Guys,
do you know how much is salary rate for a exp. 5+ yrs cisco network CCIE (R/S)?
I am offered $100/hr ..but heard most guys are taking $150/hr ? I am still working with my previous employer and not getting well paid..
in dc salary $200k..
please help me out.

there are only 5125 CCIE in US so far , so they can not even bring on H1B quota ..
I appreciate your suggestion ,
thx
mfano huo hapo juu, huyo engineer jamaa anakoplain analipwa 100 kwa saa. sasa tumpigie mahesabu kwa haraka haraka itakuwa 8*100*30*12=288000usd kwa mwaka.
sasa chukulia uwiano best uliyepost hapo juu yani dokta/eng= 235000/28800 = 0.82.

Njoo kwa mshahara wa madokta wa tanzania/engineer wa tanzania uone na uone kama kuna tofauti kubwa na 0.82. Ama ukiona inakuchanganya sana chukua uwiano wa daktari wa marekani na wa kima cha chini cha marekani upate uwiano. Kisha chukua mshahara wa daktari wa tanzania na wa kima cha chini upate uwiano, na baadae linganisha huo uwiano.
 
reformer,

Mimi natimiza wajibu wangu kwa muajiri wangu baada ya kutimiza nategemea na yeye atimize upande wake.

Kama nikihisi siridhiki na mwenendo wa mwajiri katika kutimiza wajibu wake au mazingira ya kazi ninatoa Resignation naenda kufanya kazi sehemu nyingine kwakuwa nina vigezo vya kutosha na uzoefu katika eneo langu.
Ok kama usemayo ni kweli basi ww ni mmoja ya wazt wachache wanaopaswa kuwa mfano.
Nijuavyo mimi hakuna kada ambayo haina kashfa ya rushwa na ubabaishaji TZ.
Na hii inasababishwa na viongozi wetu ambao baada ya kupewa madaraka miezi sita tu wana nyumba za ajabu na magari ya kifahari.
Unategemea nn toka kwa wafanyakazi wengine kama madokta, walimu, polisi nk?
 
Kama swala ni maslahi basi tuongelee maslahi ya watumishi wote wa umma na jinsi ya kuyaboresha sio madaktari peke yao.

Just imagine afisa masijala wa serikali nae agome kwamba mazingira magumu kule kwenye ma file kuna vumbi hawezi kwenda na mshahara mdogo. Askari nae agome vitendea kaiz hamna na hana allowance za mazingira magumu kwakuwa anashika bunduki. Bwana shamba nae agome kwamba hana usafiri na mazingira anayoishi vijijini hatarishi anatembea umbali mrefu. Bwana mipango miji agome anaingia maporini kupima viwanja anaweza kugongwa na nyoka huko. Mbunge nae agome kwamba bunge la Kenya linalipa pesa nyingi kwa wabunge na wao wanataka walipwe kama Kenya.
yeyote anayeona anapunjwa, agome tu. Woote uliowataja watagoma kama si leo basi kesho subiri tu kikombe cha hasira kijae, chanzo cha yote haya ni ufisadi ulio kubuhu, leo tunashudia migodi ikilipa kodi kwa wana siasa huku selikali ikilamba mrahaba wa geresha,hakika hatufurahii, mara unasikia upotevu wa mabilion na hapa na pale na selikali ikiwasamehe wahusika!
 
Webondo

Sikutaka kulinganisha magnitude ya mshahara!!! nilitaka kuonesha how serious wenzetu wako katika kurank malipo kwenye public sector

Pamoja na kurank hiyo mishahara kama mmoja ya watanzania waliobahatika kuishi Marekani huko nyuma ukweli ni kwamba madaktari wa Marekani na wafanyakazi wa Marekani wa kada zingine hufanya kazi kuwatumikia wananchi kisha huwa rewarded kwa juhudi zao. Sie Tanzania wafanyakazi haswa madaktari na waalimu hudai mishahara waongezewe ambayo ni haki kabisa kutokana na ughali wa maisha lakini hao hao madaktari na waalimu serikalini hawafanyi kazi ukilinganisha na wenzao wa sekta binafsi.

Kwanza serikali imewapa upendeleo madaktari kufanya kazi serikalini na kwenye sekta binafsi ambapo kada zingine kama wanasheria, wahasibu, wahandisi na marubani hawaruhusiwi kuwa wameajiliwa serikalini na bado wakafanya kazi sekta binafsi kwa uwazi labda kwa kujificha. Cha ajabu pamoja na huo upendeleo madaktari wengi hospitali za serikali hawafanyi kazi wengi wao wanaingia kusaini vitabu na kukaa ofisini au kusubiri muda wa kuondoka kwenda nyumbani au hospitali binafsi wengine wanakuwa mitaani kupiga mishemishe muda wa saa za kazi kama kada nyingine zifanyavyo.

Maana madaktari na manesi wangefanya kazi zao kwa kujituma kwanza ukizingatia kada yao inahusu maisha ya wanadamu moja kwa moja wagonjwa wengi wasingefia mapokezi au kwenye foleni wakisubiri kutibiwa. Siku hizi ukifika hospitali za serikali kama unajuana na daktari utahudumiwa haraka na kuacha watu wengi kwenye foleni huku madaktari wakiwa ofisini wanapiga story. Madaktari mnalipwa pesa nyingi serikalini kwa kuanzia mshahara kuliko kada zingine naomba mfanye kazi kwanza kwa wito na utiifu sio wengi wenu mnavaa majoho meupe wakati hamtoi huduma wagonjwa wanakufa kwa kukosa huduma.
 
Back
Top Bottom