Malipo ya fidia ya ardhi

abudist

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
850
781
Wakuu nataka kueleweshwa kiasi gani wakazi wa Kiromo, Bagamoyo wanapaswa kulipwa ardhi yao iliyochukuliwa kwa matumizi ya SEZ projects. Eneo hili liko kwenye earmarked ya SEZ (Just behind Kiromo Hotel) na wakazi wamesitishwa kuendeleza chochote toka mwaka 2008. Na mpaka sasa hakuna chochote kilichofanyika kwenye maeneo hayo ambayo walikuwa wanalima. Kuanzia mwaka 2008 mpaka leo wanasumbuliwa kulipwa na serikali inadai haina fedha.
Wakazi hawa wameshaenda kwenye ngazi tofauti kulalamika bila kufanikiwa, wamekuwa wanaahidiwa ahadi za uongo zisizo na mwisho kila mwaka.

Ahadi kubwa ilitolewa na makamu wa rais, mama Samia Suluhu September 2015 wakati CCM inasaka kura. Alipohutubia Zinga, Bagamoyo aliahidi CCM ikishinda italipa wananchi hawa takriban shs 40 billion za fidia kwenye maeneo hayo Ref: Tanzania: CCM to Support Bagamoyo Residents Recover 40 Billion/ - Land Lakini kama kawaida ya wanasiasa wetu wanapopata madaraka, baada CCM ya kupata ushindi ahadi hiyo ahikutimizwa mpaka sasa. Hadi leo watu hawa bado wanahangaika na kibaya zaidi wamesitishwa kufanya maendelezo yeyote kwenye maeneo yao. Mama mkwe wangu ni mmoja wa wahathiriwa.

Swali langu la msingi ni: Kama wakilipwa mwaka huu kiasi gani watapaswa kulipwa kwa kila square metre? Sababu tathmini ya ardhi ya maeneo yao ilifanyika 2008/2009 na sasa tuko 2017.
 
Back
Top Bottom