Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 491
- 781
Serikali imewaeleza wakazi wa Sinza kuwa Mpango wa Uendelezaji Upya wa Eneo la Sinza wa mwaka 2026-2046 haulengi kuwaondoa wananchi katika maeneo yao, bali kuboresha matumizi ya ardhi, kuongeza thamani ya mali zao na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika eneo hilo.
Akifungua mkutano wa wadau wa kukusanya maoni kuhusu Rasimu ya Mpango wa Uendelezaji Upya wa Sinza jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Leonard Akwilapo, amesema mpango huo unalenga kuongeza thamani ya ardhi, kuboresha mazingira ya makazi, kuimarisha miundombinu, kuongeza ajira, kuvutia uwekezaji na kuifanya Sinza kuwa eneo la kisasa lenye ushindani mkubwa wa kiuchumi.
Dkt. Akwilapo amesisitiza kuwa utekelezaji wa mpango huo utaongozwa na sheria, sera na taratibu za nchi huku haki za wamiliki wa ardhi zikiheshimiwa kikamilifu.
Kupitia mpango huo, ameeleza kuwa wamiliki wa ardhi wataendelea kuwa sehemu ya maendeleo ya maeneo yao kwa kuchangia ardhi kwa pamoja ili kuwezesha upatikanaji wa miundombinu, huduma za jamii na maeneo ya maegesho.
"Lengo la Serikali si kuchukua ardhi za wananchi, bali kuweka mazingira yatakayowezesha matumizi bora zaidi ya ardhi, kuongeza thamani ya mali za wananchi" amefafanua Dkt. Akwilapo.
Pia soma
~ Mazungumzo ya kuhamisha Wananchi wa Sinza yasifanyike kwa mafungu hotelini, tushirikishwe na uwazi uwepo
~ Mpango wa Serikali kuendeleza upya maeneo ya Sinza unahitaji uwazi na uwajibikaji