Malighafi ya Nyuklia kuzalishwa Pangani

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuwezesha upatikanaji wa leseni kubwa ya uchimbaji madini (Special Mining License - SML) kwa Kampuni ya Nyati Mineral Sand inayomilikiwa na kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Strandline ambayo itapelekea kuanza kwa mradi mkubwa wa uchimbaji madini Tembo katika Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema hayo leo alipofanya ziara ya kutembelea sehemu ya eneo la mradi huo iliyopo katika Kijiji cha Stahabu, Kata ya Mikinguni Wilayani Pangani-Tanga.

"Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza Wizara ya Madini kuhakikisha tunawezesha uanzishwaji wa miradi hii mikubwa na ya kimkakati ambayo itapelekea sio tu ustawi wa uchumi wa Nchi yetu, bali kuwa kichocheo cha maendeleo na ustawi wa Wilaya ya Pangani na Wananchi wanaozunguka mradi huu.

Mradi huu unatarajiwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 125 ambao unakadiriwa kuishi kwa miaka 20 hadi 25 utatekelezwa katika Vijiji 8 vilivyopo katika Kata za Mikinguni, Mwera, Tungamaa na Bweni-Wilaya ya Handeni,Mkoani Tanga.

Akiongea kwa niaba ya Mwekezaji, Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyati Mineral Sand Ltd ambaye anawakilisha Hisa za Serikali, Heri Gombera alieleza kwamba mradi huo unatarajiwa kuanza mwaka 2026 na unatarajiwa kuzalisha tani milioni 8 kwa mwaka ya madini mbalimbali yakiwemo titanium, ilmenite, rutile, zircon na monazite ambayo pamoja na matumizi mengine hutumika pia kuzalisha malighafi za injini za ndege, nyuklia, vifaa vya Hospitali na viwanda vya marumaru na rangi.

Credit - AyoTv
 
Back
Top Bottom