Mali inasakwa Makaburini si Mashambani tena

Mali inasakwa Makaburini si Mashambani tena

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
11168407_555876271221192_4275440744529439287_n.jpg
Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamebomoa kaburi la Napegwa Kishaluli (75) mkazi wa Mailimoja Kibaha mkoani Pwani aliyezikwa Aprili 20 mwaka huu na kumvua nguo zote pamoja na kuchukua mikoba aliyokuwa amezikwa nayo.

Tukio hilo lilitokea Aprili 24 mwaka huu katika Kata ya Tangini jirani na soko la Loliondo ambako baada ya mazishi kaburi hilo liliwekewa mlinzi kwa muda wa wiki moja.

Mkataba wa mlinzi huyo ulipomalizika aliondoka na siku iliyofuata kaburi hilo lilivunjwa.

Watu wa karibu na familia ya marehemu wamesema kuwa baada ya mazishi ulikuwapo uvumi kwamba marehemu alizikwa na vitu vya thamani zikiwamo fedha, simu, pete na mikufu ya dhahabu pamoja na nguo zenye thamani kubwa.
 
ya nini kumzika mtu na mikoba, mikufu ya dhahabu/shaba, au vitu vyovyote vya thamani?? atavifanyia nini huko kaburini? anaviona?? mnataka kumuonyesha nani?? waliobaki hawawezi kuvitumia??

na nyie mnaovunja kaburi hamuogopi/hamuoni aibu?? hamthamini mwili wa binadam mwenzenu??

ujinga tu
 
Hizi mambo za kuzika watu na suti ya 2M na cheni za gold. hakiyanani ata mi nikikuona unazika marehem na izo mambo navunja kaburi. wenzenu tunatoa dhahabu ardhini ninyi mnairudisha ardhini, ujinga huu
 
Nothing is the number when you die...! Kitendo cha kuweka mlinzi kiliatract wezi

mshana jr...comment yako imering a certain bell in my brain..I believe long, long time ago nimewahi kusoma kitabu chenye title ya "Nothing is the Number When You Die" am I right?
 
mshana jr...comment yako imering a certain bell in my brain..I believe long, long time ago nimewahi kusoma kitabu chenye title ya "Nothing is the Number When You Die" am I right?

Yeah miaka ile ya tisini mwanzoni una kumbukumbu nzuri Inkhubu
 
Last edited by a moderator:
Watu hawaogopi jamani, mie nikipita makaburini mwili unanisisimka nasoma dua zote nnazo zijuaa seuze kuuvunja kaburi Duu 🙆, mara linatoka Joka ...
 
Hizi mambo za kuzika watu na suti ya 2M na cheni za gold. hakiyanani ata mi nikikuona unazika marehem na izo mambo navunja kaburi. wenzenu tunatoa dhahabu ardhini ninyi mnairudisha ardhini, ujinga huu

Kabisa unaweza bilautani!!
 
Haya bwana unamzika mtu na cm ili aingie jf? au ampigie nan! Wawe wanazika na nyumbayake simali yake
 
dunia inaelekea ukingoni, niliona documentary ya Kibera hapa naiona bongo
 
Haya bwana unamzika mtu na cm ili aingie jf? au ampigie nan! Wawe wanazika na nyumbayake simali yake
tena simu yenye vocha za maana, huenda wako ambao wangeendelea kumtumia vocha
 
Watu hawaogopi jamani, mie nikipita makaburini mwili unanisisimka nasoma dua zote nnazo zijuaa seuze kuuvunja kaburi Duu , mara linatoka Joka ...
heri umchokonoe pweza, binadamu kashindikana
 
Back
Top Bottom