Malezi waliyotupa wazee wetu wa miaka ile.

Bismack

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2018
Messages
392
Points
500

Bismack

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2018
392 500
Kuna wakati nilikua naona kabisa baba yangu ni katili aliyepindukia mana kichapo kilichokua kinatembezwa nyumbani hakikua cha mchezo kwa sisi vijana tuliokua bado wadogo, ilifika hatua mpaka mama mmoja jilani ndo alikua anakuja kumuomba baba atusamehe mana hata kwa huyo mama hali ilikua hivohivo mmewe akianza kupiga utasema anataka kuua.

Basi bwana siku moja nimetoka shule nikala msosi nikashiba, bahati mbaya siku hiyo mzee alikua kaacha redio yake ya panasonic mezani nilivoiona nikaifakamia nikaiwasha nikaanza kupata mziki, sasa nikaona hii sauti mbona ndogo nikasema acha niongeze sauti nikaanza kuzungusha kile kidude cha volume mpka nikakihalibu yani ukikizungusha kinazunguka hakifiki mwisho.

Hakika siku hiyo ndo niliuona umhimu wa yule mama aliyekua anakuja kutuombea msamaha mana kipigo cha siku hiyo sitokuja kukisahau na kuanzia hapo niliheshim kitu chochote cha baba yangu, bila yule mama kufika nyumbani nadhani sahivi nisingeandika huu uzi mama yule Mungu amubariki kwakweli sababu hata mama yangu ile kesi alishindwa kuiamua aliishia kulia tu.

Baba yangu alikua mkali sana enzi hizo yaani hata akute hujavaa shati ujue hapo patachimbika au unyoe nywele kihunihuni labda uwe na pakwenda ila siyo nyumbani, na ikitokea jilani akaja kusema kosa ulilolifanya huko mtaani au shule hachelewi kukutandika mbele ya mleta tarifa. Mambo kama haya ambayo mzee alikua ikifanya kiukweli yaliniweka katika wakati mgumu sana kwa kipindi kile mpka nikawa najiuliza lini nitakua na kuepuka hivi vboko vya hapa nyumbani mana mzee akisafiri ndo ilikua full shangwe sababu mama yangu hajui mambo ya kupiga yeye anaongea tu.

Nimekua sasa najitambua na nimeelewa umhimu wa kile alichokua akikifanya baba japo kwa kipindi kile nilikua namuona ni katili aliyepitiliza, mana ninaona madhala vijana wengi waliolelewa kimayaimayai, wengine ndo hawa ambao hawawezi kufanya kazi ngumu, kupika hawezi, jembe hawezi kushika , hata shoka hajui inafanya kazi gani.

Namshukulu sana baba yangu kwa kunichapa pengine nisingekua nabehave hivi.
 

Forum statistics

Threads 1,391,835
Members 528,475
Posts 34,090,917
Top