Naomba nitafakari kwanza then nitarudi kuchangia. Ila sometimes ni ngumu sana kwa watoto na inawaathiri sana na mara nyingine huwa wale wazazi wanakuwa na malezi mazuri sana bila kujali kuwa sio mtoto wao. Na huwezi kuona tofauti yoyote kati ya watoto wa ile familia.
Mbu nimependa sana topic yako,imenigusa directly. I wil say ni muhimu sana kuwa na visitation rights no matter how costly it wil be. Hata kama mtoto atapata malezi mazuri vipi kutoka kwa step parent bado yuko attached na real parent wake in a way,at least biologically na huwezi kuibadilisha iyo but u can only strenthen it.
...Maisha yanapelekea wengi wetu kujikuta tunaingia mahusiano mapya tayari tuna mtoto/watoto. Ili kuondoa ile hofu ya baba/mama wa kambo si sawa na 'mzazi'...Je? wazazi wapya (Step parent) tuna nafasi gani katika malezi na makuzi ya mtoto au watoto wa mume/mke?...
Utamlea na kumkuza unavyotaka wewe ukimhusisha mume/mkeo, au utamhusisha (biological) pia na mzazi wake?
Fikiria kwenye dhana ya mzazi wa kambo unavyoweza laumika/sifika kwa malezi ya mtoto/watoto hao.
Tafakari umuhimu wa visitation rights, baba/mama kumtembelea mtoto, au kumshinikiza mtoto aende likizo kwa baba/mamake.
Je, kipato, Imani ya dini, mila na desturi zina athari gani kwenye malezi ya mtoto/watoto hawa iwapo wazazi wanatofautiana dini, mila na desturi...?
Mkuu unajua kuna kitu kimoja. Kukubalika kwa yule mtoto katika familia hii mpya. Yaani mama mpya au baba mpya amkubali yule mtoto kama wake na ampe malezi kama mtoto wake.
Na je imani nayo ina nafasi gani kwa yule mtoto kama mzazi mmojawapo au wazazi wakabadilisha dhehebu je yule mtoto anaathirika vipi na je atafuata imani ya upande gani
Na je yule mtoto anamuonaje mzazi mpya. Anaikubali familia mpya au anachukua muda kuikubali
Vile vile je kama ni mpya hafungamani na mzazi yeyote kati ya wale je yule mzazi wake ana haki ya kumtembelea mwanae na je huku anakokuja kutembelea mtoto wake anapewa makaribisho yanayostahili kama mzazi wa yule mtoto.
Na je mtoto anaona mabadiliko hayo kwa wazazi wake wapya kwa yule mzazi wake.
Je kuna kificho cha mawasiliano kati ya mzazi yoyote
Mkuu unajua kuna kitu kimoja. Kukubalika kwa yule mtoto katika familia hii mpya. Yaani mama mpya au baba mpya amkubali yule mtoto kama wake na ampe malezi kama mtoto wake. Na je imani nayo ina nafasi gani kwa yule mtoto kama mzazi mmojawapo au wazazi wakabadilisha dhehebu je yule mtoto anaathirika vipi na je atafuata imani ya upande gani. Na je yule mtoto anamuonaje mzazi mpya. Anaikubali familia mpya au anachukua muda kuikubali Vile vile je kama ni mpya hafungamani na mzazi yeyote kati ya wale je yule mzazi wake ana haki ya kumtembelea mwanae na je huku anakokuja kutembelea mtoto wake anapewa makaribisho yanayostahili kama mzazi wa yule mtoto.
Na je mtoto anaona mabadiliko hayo kwa wazazi wake wapya kwa yule mzazi wake. Je kuna kificho cha mawasiliano kati ya mzazi yoyote
Mbu hapo ni kukosea unapomlazimisha jambo lolote mtoto kama huyo. Mwache with time atajua kuwa huyu ni mzazi wangu na napaswa nimuheshimu na kumwita baba au mama
Na worries kubwa ni hiyo. Hata ile kuja kumtembelea mtoto inaraise ile doubt kuwa kumuintertain mtu kama yule ni kutaka kurudisha uhusiano upya wakati ni just for mtoto tuu
Hii imenigusa moja kwa moja mbu… yaani ile directly… Nashukuru for the post for naamini kua michango ya wengi katika this thread itanisaidia mimi na wengine moja kwa moja… Thank you… Kwa maoni yangu…
Imani ya dini
Imani ya dini hua tatizo saana pale inapokua wale wenye dini zao wameshikilia dini zao to the extent anataka kila alomzunguka awe dini yake, na kama vile za wenzie sio dini… Inapokua hivi huwa kwanza ni vigumu hata kuoana dini tofauti maana kila mmoja hujiona wa maana…
However kwa wale ambao wanaoana dini tofauti athari ya malezi kwa mtoto naona sio mbaya saana but sometimes yaweza kua hata for the better… Yule mtoto anakua exposed to two sides of the religion i.e. Islam vs Christianity.. IMO naona kama mtoto anakua na exposure nzuri, na pia humuwekea busara Fulani ambayo imetokana na ile tolerance ya wazazi ya dini ya mtu mwingine na the like….
Athari saana ni pale inapokua watoto weshakua brainwashed na their religion or the new mzazi – hapo naona amani inakua finyu, maana lazima kutakua na migongano ya mara kwa mara na dharau juu… from one or both sides…
Narudi na upande wa kipato....
Mkuu Mbu hapo ndo unapaswa uhandle the situation kibusara zaidi kumfanya yule mtoto akue akijua kuwa hakuna tatizo. Hutakiwi kumuonyesha kuwa uliachana na mama yake kwa ugomvi au misukosuko maana wako wengine wanahamishia hasira kwa mtoto. Mtoto hatakiwi kuonyeshwa hayo wala hasira za wazazi zisihamishiwe kwa mtoto.
Kama ni kumtembelea mtoto au mzazi ondoa kile kinyongo (japo najua ni ngumu) kwa muda wakati wa kumtembelea mtoto asije akahisi kuwa baba au mama ana kinyongo na mama au baba