Malezi/ Makuzi hujenga tabia ya mtu

complex31

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
379
1,208
Tabia ya mwanadamu yeyote toka anapokua na akili mpaka anakuwa mtu mzima asilimia kubwa hushabihiana na malezi aliyokua anayapata.

Kama ulipitia malezi kama kuanza kufanya kazi kama kupika, kufua, kwenda shule asubuhi mwenyewe, kujisimamia vitu vyako vingi kipindi cha shule ya msingi, mtu kama huyu akiwa mtu mzima mara nyingi hupenda kufanya vitu vingi peke yake na kutambua majukumu yake mapema kulinganisha na mtu aliekua anategema dada wa nyumbani.

Kwa wale waliokua na mlezi mkali sana mwenye kupiga na kupitia maisha yenye changamoto nyingi kama kuanza kufanya kibarua ili kupata ada ya kwenda shule hawa hata ukubwani hua ni watu wenye hasira sana, hupenda kufoka sana, kuogamba na watu kwa sababu zisizo na maana na hata akibahatika kupata kazi anakua hana mahusiano mazuri na wafanyakazi walio chini yake

Kwa wale waliokulia malezi ya kufuliwa, kupikiwa, kupelekwa shule na mara nyingi kuelekezwa vitu na wazazi wao hawa asilimia kubwa wanakua sio watu wa makuu sana, hupendelea kusikiliza mtu zaidi ya kuhukumu na wakibahatika kupata uongozi hua ni watu wakarimu wanaopenda kuelewa tatizo hasa nini badala ya kuhukumu

Kuna wale wengine malezi yao yanakua ni ya juu zaidi kiasi cha kwamba wanakua hawajui jamii hasa ikoje na walimwengu wakoje, hapa tunaongela wale ambao taa ya ndani ikiungua atasema ngoja nimpigie baba ataleta mtu wa kutengeneza.
Hawa hua hawajui thamani ya kitu na usishangae ukamuazima kitu chako cha thamani akipoteze na kuishia kukuambia hayo ni mambo ya kawaidia utapata lingine.
Malezi haya sana sana huwapata kwa wale wazazi wanaosema mtoto wangi sitaki atesske na kitu chochote kwani mimi nimeteseka sana

Aina nyingine ni wale waliokulia malezi ya kikatili mfano kuona mama yake mzazi akipigwa mbele yake, kuambulia kipigo kila anapofanya kosa, kuua wanyama/ wadudu kama mijusi, mbwa, paka kipindi cha utoto, hawa watu wa hivi hua ni watu wa visasi sana na ni wepesi kupiga/ kujeruhi kwani kwenye makuzi yake anakua amezoea kuona mambo kama hayo.


Ni vyema kujua malezi au tabia za mtu kabla hujaamua kumuoa au kufanya nae kazi kwa Karibu kuepuka msongo wa mawazo au ugomvi usiokua na chanzo.
 
Mungu huyu muache aitwa Mungu. Inaweza ikawa kweli unachowaza ila sasa wengine mbona wanajiuza na kwao matajiri? Nadhani kwa sie wenye watoto unaweza walea vizuri kabisa na bado wakawa na mambo ya ajabu. Mda mwingine mwachie Mungu tu awaongoze. .
 
Back
Top Bottom