Malema awashukia Viongozi wa Afrika Kusini kwa kuuza bandari ya Durban. Tanzania tujiangalie

Mlaleo

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
13,395
9,764
Kijana Machachari wa South Africa ameichana chana nchi yake kwa kuwaita watawala wajinga baada ya kuuza Bandari ya Durban kwa tamaa ya Pesa tu na haukuna kingine ikipita miaka kadhaa tunasema tumetawaliwa..

Viongozi wabovu wanashindwa kuongoza nchi wanaharibu mali za nchi kwa kulindwa kisha wanasingizia hatuwezi kujiongoza wanawapa wageni kila kitu ili wapate pesa na waendelee kuenjoy matunda ya nchi.. Wanauza nchi kwa highest bidder.

Amesema ule wimbo wa ua makaburu ua Wakulima wazungu sio kosa bali ni jumbe wa wanyonyaji wa wananchi... sasa CCM jiangalieni ondosheni majizi yote chamani majizi yasiyo na faida kazi yao chamani ni kuleta mawazo ya kuumiza wananchi tu kama kuongeza kodi kuweka matozo kila nyanja za fedha wanawaletea adhaa raia wapole... Kama utawala huu una akili waende China na waombe kuendesha Airport ya Shanghai na waambie Wachina kuwa Uongozi wa Tz utawaongezea mapato mengi yanayopotea pale airport China..

Tunauza Utu wetu kwa pesa.. Walaaniwe.

Tanzania tunahitaji tufufue Mashirika yetu kisha kuweka sheria kali kwa atakayeleta upuuzi ikiwezekana adhabu ya kunyonga kama China tuone kama kuna kitu kitakufa au mjinga atakaye hubiri uwekezaji
 
IMG_20230323_192240.jpg
 
Nchi ni dubwana kubwa sana,unaweza kuharibu muda wako bure, ukatumia muda mwingi kukosoa kwa hasira za kipuuzi,ukapoteza muda badala ya kuutumia muda huo hata kujilimia mbogamboga kwa ustawi wa familia yako.
TAKE A NOTE!
 
Siku moja,omba maiki kwenye mkutano wa CHADEMA,uwaambie hivyo,watakushukuru sana.Tena sisitiza kabisa kua achaneni na kukosoa,limeni mbogamboga,mpate vijihela huku bandari akipewa mwarabu kwa mkataba wenye walakini.
Nadhani ungekuwepo hata kipindi cha Nyerere,kipindi kile yeye na wenzake wanapigania uhuru,usingesita kumshauri aachane na hizo habari,aendelee kufundisha tu pale St.Mary's secondary.
Safi sana mkuu,una akili nyingi sana.
Nchi ni dubwana kubwa sana,unaweza kuharibu muda wako bure, ukatumia muda mwingi kukosoa kwa hasira za kipuuzi,ukapoteza muda badala ya kuutumia muda huo hata kujilimia mbogamboga kwa ustawi wa familia yako.
TAKE A NOTE!
 
Amesema ule wimbo wa ua makaburu ua Wakulima wazungu sio kosa bali ni jumbe wa wanyonyaji wa wananchi... sasa CCM jiangalieni ondosheni majizi yote chamani majizi yasiyo na faida kazi yao chamani ni kuleta mawazo ya kuumiza wananchi
Sasa hapo unawaambia ccm wajiondoshe wenyewe au? 🤣
Elewa kuwa majizi ndio hao hao!
 
Back
Top Bottom