Malecela akoleza moto sakata la gesi

Malecela akoleza moto sakata la gesi

The Khoisan

Platinum Member
Joined
Jun 5, 2007
Posts
18,742
Reaction score
18,483
[h=1]Malecela akoleza moto sakata la gesi[/h]WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwanasiasa Mkongwe nchini, John Malecela, ametoa wosia kuhusu mgogoro wa gesi akiiomba Serikali kufanya kila iwezalo ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mtwara wananufaika kwanza na rasilimali hiyo.

Malecela alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa na gazeti hili kutoa maoni yake kuhusu mgogoro wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam unaoendelea kushika kasi katika siku za hivi karibuni.
“Ukiwa karibu na waridi unatakiwa kunukia waridi. Wakazi wa Mtwara nao wanatakiwa wanukie waridi,” alisema.

Malecela alisema, pamoja na ukweli kwamba rasilimali inayopatikana nchini ni kwa ajili ya watanzania wote, ukweli kwamba wakazi wa eneo inakopatikana rasiliamali hiyo wanapaswa kunufaika nayo, haukwepeki.

“Hatutakiwi kuwaacha hivi hivi wana-Mtwara eti kwa sababu hii ni rasilimali ya Watanzania wote. Ni lazima wanufaike zaidi, wao kuliko wengine kwa kuwa wako karibu na waridi,” alisema Malecela.
Alisema licha ya gesi hiyo kuwa ya watanzania wote, Serikali inatakiwa kuandaa utaratibu ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Mtwara wananufaika zaidi na rasilimali hiyo.

Malecela alieleza kuwa umaskini uliokithiri katika baadhi ya mikoa nchini ukiwamo mkoa wa Mtwara, ndio unaosababisha watu waanze kudai rasilimali zinazotoka katika maeneo yao wakiamini kuwa ndio mwanzo wa ukombozi wao.
“Serikali iyaangalie kwa umakini maeneo yanayotoa utajiri na rasilimali, ni lazima wapewe upendeleo ili wafurahie matunda mali asili yao,” alisema Malecela.

Kuhusu gesi kutoka Mtwara
Malecela alisema anaunga mkono gesi kusafirishwa mahali popote palipo na soko kubwa ili iweze kuwanufaisha Watanzania lakini, lazima kuwe na mkakati wa kuwanufaisha pia wakazi wa eneo husika.

“Mnaweza kuisafirisha gesi kwenda mahali popote palipo na soko kubwa, lakini mkaangalia namna mnavyoweza kuwanufaisha wakazi wa Mtwara,” alisema na kuendelea;
“Rasilimali inayogundulika popote ndani ya Tanzania ni mali ya watanzania wote, hivyo hata gesi ya Mtwara si ya wakazi wa Mtwara peke yao.”

“Kama ilivyo kwa bwawa lililopo katika Jimbo la Mtera linalozalisha umeme na kuingizwa katika gridi ya taifa kwa ajili ya watanzania wote, gesi nayo inatakiwa kuwanufaisha watanzania wote,”

Mkazi Mtwara atishia gesi kutoonekana
Katika hatua nyingine Kikongwe Somoe Issa (90) ambaye ni mkuu wa kaya ya Msimbati, kijiji ambacho gesi asilia inavunwa ameionya Serikali kutoendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi.

Kikongwe huyo ambaye haoni wala kusikia alisema hayupo tayari kuona gesi hiyo ambayo imepatikana katika kijiji hicho ikiondoka mkoani Mtwara.

“Atakayejaribu kuondoa gesi hii kitakachomkuta atakijua yeye mweyewe…ninasema gesi isiende kokote…iwapo atabisha inawezekana akasafirisha maji tu na isiwe gesi yenyewe” alisema bibi huyo kupitia kwa mkalimani wake Asha Hamis. Aliongeza kuwa,“mwaka walioanza kuchimba (2005) walifika hapa bila kubisha hodi, wanajua kilichowakuta…bomba lilikuwa haliendi chini wala kurudi juu…walinifuata hapa nikaenda kufanya tambiko

”
 
Hawa waandishi wa habari kweli ni viboko!

Mimi sioni moto wowote katika kusema waridi latakiwa kunukia, ni ukweli mtupu!
 
Na MTERA DAM iko jimbo la MTERA.........NGOJEJI MSIKIE MAMBO MUDA SIO MREFU.......Megawati zote zile!
 
Ngoja Le mutuz aje ampinge kwa vijembe hapa. Maana mtoto yule siku hizi! Kapinda kwelikweli.
 
Ngoja Le mutuz aje ampinge kwa vijembe hapa. Maana mtoto yule siku hizi! Kapinda kwelikweli.

Le mutuz amejipambanua kuwa yeye ni mchumia tumbo. Kwa sasa yuko bize na kusaka vyeo vya upendeleo. Baba yake sijui huwa anajisikiaje akimuona mwanae anashabikia ujinga. Nadhani huwa anamkumbuka sana Ipy mwanae aliyetangulia mbele ya haki mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi amen.
 
mzee wetu ana akili - anamzidi mbali sana mwanae!! sijajua genetic ilikuwaje!
 
Wee kweli ni mr zero moto alioukoleza mzee malecela ni upi huo? Acha umbeya mtoto wa kiume, mzee malecela kaongea kwa hekima na tahadhali kubwa sana akiweka mbele maslahi mapana ya taifa. sasa unaposema kakoleza moto katika suala la gesi, ni moto gani aliokoleza hapo? acha hizo mr zero!
 
we kweli ni kisima jongoo,,
ukitaka moto wa mlipuko kama bomu ili uweze kurealize??
 
Story kama hizi zinajaza kurasa kwenye magazeti tu. Hakuna tija yoyote ndani yake.
 
Wee kweli ni mr zero moto alioukoleza mzee malecela ni upi huo? Acha umbeya mtoto wa kiume, mzee malecela kaongea kwa hekima na tahadhali kubwa sana akiweka mbele maslahi mapana ya taifa. sasa unaposema kakoleza moto katika suala la gesi, ni moto gani aliokoleza hapo? acha hizo mr zero!

Wewe ndiyo ule utajiri wa Mazuzu tulionao TZ!! Kwa akili yako tu ya kawaida unaona kuwa ni mimi ndiyo nimeandika hiyo story?? Ungeuliza walau source ningekuelewa kidogo au na wewe ndiyo ileile familia...............!! Kabadilishe kitwa cha habari mwananchi: Malecela akoleza moto sakata la gesi - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
KITAIFA

Na Raymond Kaminyoge Dar na Abdallah Bakari, Mtwara

Posted Jumatatu,Januari7 2013 saa 8:43 AM

KWA UFUPI

ASEMA LICHA YA KUSTAHILI KUWANUFAISHA WATANZANIA WOTE,UKIWA KARIBU NA WARIDI UNATAKIWA KUNUKIA

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwanasiasa Mkongwe nchini, John Malecela, ametoa wosia kuhusu mgogoro wa gesi akiiomba Serikali kufanya kila iwezalo ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mtwara wananufaika kwanza na rasilimali hiyo.

Malecela alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa na gazeti hili kutoa maoni yake kuhusu mgogoro wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam unaoendelea kushika kasi katika siku za hivi karibuni.

"Ukiwa karibu na waridi unatakiwa kunukia waridi. Wakazi wa Mtwara nao wanatakiwa wanukie waridi," alisema.

Malecela alisema, pamoja na ukweli kwamba rasilimali inayopatikana nchini ni kwa ajili ya watanzania wote, ukweli kwamba wakazi wa eneo inakopatikana rasiliamali hiyo wanapaswa kunufaika nayo, haukwepeki.

"Hatutakiwi kuwaacha hivi hivi wana-Mtwara eti kwa sababu hii ni rasilimali ya Watanzania wote. Ni lazima wanufaike zaidi, wao kuliko wengine kwa kuwa wako karibu na waridi," alisema Malecela.

Alisema licha ya gesi hiyo kuwa ya watanzania wote, Serikali inatakiwa kuandaa utaratibu ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Mtwara wananufaika zaidi na rasilimali hiyo.

Malecela alieleza kuwa umaskini uliokithiri katika baadhi ya mikoa nchini ukiwamo mkoa wa Mtwara, ndio unaosababisha watu waanze kudai rasilimali zinazotoka katika maeneo yao wakiamini kuwa ndio mwanzo wa ukombozi wao.

"Serikali iyaangalie kwa umakini maeneo yanayotoa utajiri na rasilimali, ni lazima wapewe upendeleo ili wafurahie matunda mali asili yao," alisema Malecela.

Kuhusu gesi kutoka Mtwara
Malecela alisema anaunga mkono gesi kusafirishwa mahali popote palipo na soko kubwa ili iweze kuwanufaisha Watanzania lakini, lazima kuwe na mkakati wa kuwanufaisha pia wakazi wa eneo husika.

"Mnaweza kuisafirisha gesi kwenda mahali popote palipo na soko kubwa, lakini mkaangalia namna mnavyoweza kuwanufaisha wakazi wa Mtwara," alisema na kuendelea;

"Rasilimali inayogundulika popote ndani ya Tanzania ni mali ya watanzania wote, hivyo hata gesi ya Mtwara si ya wakazi wa Mtwara peke yao."

"Kama ilivyo kwa bwawa lililopo katika Jimbo la Mtera linalozalisha umeme na kuingizwa katika gridi ya taifa kwa ajili ya watanzania wote, gesi nayo inatakiwa kuwanufaisha watanzania wote,"

Mkazi Mtwara atishia gesi kutoonekana
Katika hatua nyingine Kikongwe Somoe Issa (90) ambaye ni mkuu wa kaya ya Msimbati, kijiji ambacho gesi asilia inavunwa ameionya Serikali kutoendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi.

Kikongwe huyo ambaye haoni wala kusikia alisema hayupo tayari kuona gesi hiyo ambayo imepatikana katika kijiji hicho ikiondoka mkoani Mtwara.

"Atakayejaribu kuondoa gesi hii kitakachomkuta atakijua yeye mweyewe…ninasema gesi isiende kokote…iwapo atabisha inawezekana akasafirisha maji tu na isiwe gesi yenyewe" alisema bibi huyo kupitia kwa mkalimani wake Asha Hamis

Aliongeza kuwa,"mwaka walioanza kuchimba (2005) walifika hapa bila kubisha hodi, wanajua kilichowakuta…bomba lilikuwa haliendi chini wala kurudi juu…walinifuata hapa nikaenda kufanya tambiko"

Bibi huyo alilazimika kutumia lugha ya kimakonde kwa maelezo ndiyo anayoifahamu vizuri, alisema wakati wa tambiko hilo wazungu waliokuwa katika mradi huo walilazimika kunywa maji kwa kutumia kifuu cha nazi ambapo mmoja wao alikataa.

"Yule aliyekataa niliwaambia aondoke, wale wenzake walimsafirisha na baada ya hapo waliaza kuchimba na gesi ikapatika…leo wanasema gesi inaondoka, hilo sikubali…mimi ndiye mwenye eneo hili, nilifanya tambiko gesi ipatikane na sasa nitafanya tambiko isiondoke" alisisitiza kikongwe huyo ambaye hajui mwaka aliozaliwa.

Kauli ya Kikongwe huyo kupinga gesi kwenda Dar es Salaam na kutishia kusafirishwa kwa maji badala ya gesi iwapo serikali itapuuza madai ya wananchi inarejesha historia ya vita ya Majimaji iliyoasisiwa wilayani Kilwa, mkoani Lindi mwaka 1905-7.

Katika vita hiyo viongozi wa kimila walisema kuwa bunduki za wazungu zitatoa maji badala ya risasi, jambo ambalo lilihamsisha wananchi wengi kupigana vita hivyo.

Kwa kauli hiyo ya mkuu huyo wa kaya anaungana na wakazi wengi wa Mkoa wa Mtwara wanaopinga mradi huo, wakiwemo wanasiasa, viongozi wa dini, mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji na CCM wilaya ya Mtwara mjini.

Katika salamu zake za mwaka mpya, Rais Kikwete, alisema gesi ni mali ya Watanzania lakini akasema Serikali itahakikisha inaandaa utaratibu kwa wananchi wa Mtwara kunufaika zaidi na gesi hiyo.

Hivi karibuni wananchi wa Mtwara waliandaa maandamano kupinga usafirishaji wa gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

Sakata hilo lilizikidi kuchukua sura mpya baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Mikindani, Mtwara, Ali Chinkawene na Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM) Hasnain Murji kumpinga Rais Kikwete wakitaka gesi isisafirishwe kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.

AH... MALECELA... Anagombea nini tena??

Uh... Sasa HUYU KIKONGWE wa MIAKA 90; Haoni Wala Kusikia anajuaje kuna GAS MTWARA?
Uh... Na LUGHA ni KIMAKONDE... Inabidi wamnunulie NYUMBA na pia KIMAWASILIANO waulize pia kama kuna OIL...

LOL... INDIGINEOUS LOCAL SCIENCE is BETTER the WESTERN TECH SCIENCE... Wazungu UUUH
 
kati ya big thinkers wachache ambao CCM imebakiwa ni huyu mzee MALECELA! mzee keshaona mbali up to 2015 kwamba kama CCM inataka ipate kura nyingi za watu wa kusini isikilize kilio chao otherwise they're lossers! sasa mtihani utakuja kwamba wananchi wa mikoa mingine yenye raslimali nao wataiga ya wana-kusini endapo wana-kusini watatekelezewa matakwa yao! let's wait & c!!!
 
kati ya big thinkers
wachache ambao CCM imebakiwa ni huyu mzee MALECELA! mzee
keshaona mbali up to 2015 kwamba kama CCM inataka ipate kura
nyingi za watu wa kusini isikilize kilio chao otherwise they're lossers!
sasa mtihani utakuja kwamba wananchi wa mikoa mingine yenye raslimali
nao wataiga ya wana-kusini endapo wana-kusini watatekelezewa matakwa
yao! let's wait & c!!!

Le Mutuz angekuwa na hata robo ya akili za mzee wake, asingekuwa anafanya u-PIMP hapa mjini...
 
Yule Mtoto wake yuko hai au alishakufa??manake haonekani tena humu
 
Kutoa usia (wosia) ndo kukoleza moto??????
 
wATU WA mTWARA MKIZUBAA MNALIWA.... wENZENU WA MARA NA SHINYANGA WALIZUBAA KWENYE DHAHABU SASA HIVI WANAAMBULIA KUNYWA MAJI YENYE SUMU NA MAHANDAKI WATAKAYOACHA.
MPAKA KIELEWEKE TU. KAMA BIBI AMBAE HAONI AMEWEZA KUBAINI HIZI MBINU CHAFU JE, MNAONA, KUSIKIA, KUTEMBEA, KUSOMA NA KUANDIKA TENA WASOMI PHD NA PROF TUCHUKUE HATUA KUKOMBOA NCHI YETU.
HUU NI WIZI MTUPU.
 
Back
Top Bottom