Malaysian Prime Minister: Flight M 370 Malaysia Plane Crashed Into Indian Ocean

Malaysian Prime Minister: Flight M 370 Malaysia Plane Crashed Into Indian Ocean

[h=1]Malaysia:Ndege ilianguka baharini[/h]
140324141155_najib_malaysia_presser_304x171_afp_nocredit.jpg
Waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak


Shirika la ndege la Malaysia limewaambia jamaa na familia za abiria waliokuwa wanasafiri kwa ndege iliyotoweka MH370 kwamba ndege hiyo imepotea na kwamba hakuna manusura.
Tangazo hilo limetolewa kwa familia hizo kwa njia ya ujumbe wa simu ya mkononi , ambao BBC iliweza kuuona.

[h=2]Taarifa zinazohusiana[/h]



Ndege ya Malaysia MH320 ilitoweka ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur tarehe 8 mwezi huu.
Aidha tangazo hilo limekuja huku juhudi za kutafuta mabaki ya ndege hiyo Kusini mwa Bara Hindi zikimalizika kwa siku ya tano bila mafaniko.
Waziri mkuu wa Malaysia amesema kuwa ndege hiyo ilianguka Kusini mwa Bahari Hindi, bila ya manusura wowote.
Aliambia waandishi wa bahari kuwa udadisi uliofanyiwa data ya Satelite kutoka Uingereza ndio umewathibitishia kwamba ndege hiyo ilimalizia safari yake Magharibi mwa mji wa Perth mbali na eneo lolote la kutua.
Ameomba vyombo vya habari kuheshimu familia za watu waliokuwa ndani ya ndenge hiyo, akisema kuwa anasikitishwa sana kwani kipindi chote walichosubiri taarifa njema , mwishowe imekuja kuwa taarifa mbaya hata zaidi.
Ndege ya Malaysia MH-370, ilipoteza mawasiliano wiki mbili zilizopita na meli za nchi mbali mbali pamoja na ndege zimekuwa zikitafuta angalau mabaki ya ndege hiyo bila ya kupata chochote.

aiseee!!!kwahyo zoezi la utafutaji ndio limefungwa,au sio?R.I.P Kama ni kweli hawapo hai tena!POLE SANA KWA WAFIWA.it really pains to my deepest of my heart.
 
Pole sana kwa ndugu,jamaa na marafiki kwa kuwapoteza wapendwa wao!Mungu aziweke mahali pema roho za marehemu wote!
 
Sasa hiyo conclusion wameipata wapi ikiwa hata mabaki ya ndege yenyewe hayajaonekana? Magharibi mwa Perth ndiyo wapi? Nchi gani? Na je nchi hiyo haikuwa na taarifa zozote kuhusu kupotea kwa ndege? Yaani nao hawakuiona ikianguka? Au hawana air security? Hii habari ina baraka kutoka mamlaka husika? Au ni speculations tu kama zingine?
 
sasa ule moshi mweupe unaotembea baharini ni nini?mbona maswali ni mengi mno?mimi nazidi kuchanganyikiwa.
 
Samahani mimi nikombali na tv, je wameonyesha ushahidi wowote wakubeba hiyo taarifa yao? Au ni makisio tu baada ya kuchoka kutafuta?
Ni kwa mujibu wa inmarsat.kampuni iliyoko London kwa kutumia technolojia ya kisasa ambayo haijawahi kutumiwa.satellite zao zina monitor position,speed,altitude na direction za ndege.data zao zimegota ktkt ya indian ocean

Australia,China aircrafts na France satellite wameona debris kusini mwa indian ocean
 
Sio siri mi naandika coment hii huku nalia.mie siamini km kweli hii ndege imeanguka baharini.ninachoamini mpk kesho ndege imetekwa.ee mungu uliyeko mbinguni wanusuru waja wako katika hili.
 
Kwa hili swala Serikali ya Malaysia nimeivulia kofia kwa blunders na usanii wa hali ya juu walioufanya kwenye sakata hili,kuanzia kuita Waganga wa Jadi mpaka kutoa wrong informations kila mara. Huku ndipo tulipoenda kujifunza na kuchukua mfumo wa Big Result Now na ndio maana umekuwa ni usanii mtupu. Na pia Malaysia wanasahau kuwa wanaraibi reputation nzuri ya Malaysia Airways walioijenga kwa muda mrefu na kwa gharama kubwa. Shame on them Malaysia!
 
Unajua hizi serikali zetu bwana huwa zinabeba siri nzito sana zaidi ya uelewa wetu aisee. Inawezekana serikali ya Malaysia inajua nje ndani ya hili suala...sasa wameahidiwa na hao wahusika (possibly one of the world power) kupewa fedha za kufidia ndugu wa hao wahanga pamoja na mikataba mizito mizito ya biashara, misaada na ushirikiano wa kimataifa sababu kulikuwa na watu ambao lazima walikuwa wapotezwe mule (michezo ya wakubwa hiyo)
NOTE: Angalia bendera ya malaysia utajua ninaongelea nini! Huu Ni Mtazamo Wango Tu...!
 
Unajua hizi serikali zetu bwana huwa zinabeba siri nzito sana zaidi ya uelewa wetu aisee. Inawezekana serikali ya Malaysia inajua nje ndani ya hili suala...sasa wameahidiwa na hao wahusika (possibly one of the world power) kupewa fedha za kufidia ndugu wa hao wahanga pamoja na mikataba mizito mizito ya biashara, misaada na ushirikiano wa kimataifa sababu kulikuwa na watu ambao lazima walikuwa wapotezwe mule (michezo ya wakubwa hiyo)
NOTE: Angalia bendera ya malaysia utajua ninaongelea nini! Huu Ni Mtazamo Wango Tu...!

Insurance ina cover.kimataifa hapo kila binadam aliyefariki mrithi wake minimum analamba $ 120,000

Serikali itaishia kuhongwa zana chakavu za kivita tu
 
Insurance ina cover.kimataifa hapo kila binadam aliyefariki mrithi wake minimum analamba $ 120,000

Serikali itaishia kuhongwa zana chakavu za kivita tu

Pia wanaweza pewa pamoja na vitisho juu ya kwanba if they won't comply na matakwa ya hao wababe wa dunia wanaweza undiwa propaganda then wakawa designated as a rogue state harbouring terrorist..kumbuka malaysia ni taifa la kiislam so they might be framed with any terrosist-harbouring scandals! Hii dunia ina wenyewe bwana!
 
najiuza swali moja tu na wadau mnaojua hili mnijuze je ndege hiyo ilikuwa na mafuta ya kutosha kuifikisha ilipoangukia?
 
Mungu ndiye anaejua yote,kama kweli Mungu awalaze pema pepon abiria waliokatizwa maisha yao,inauma sana
 
Back
Top Bottom