Malawi yaituhumu Tanzania kuvunja makubaliano

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
SERIKALI ya Malawi imesema ina wasiwasi kuhusu hatma ya mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na kwamba hali hiyo inatokana na Tanzania kuvunja sehemu ya makubaliano ya usuluhishi.

Kauli hiyo inakuja wakati jopo lo viongozi wastaafu kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(Sadc), likijiandaa kuwasilisha ripoti yake baadaye mwezi huu.

Jopo hilo linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano, litakabidhi ripoti hiyo kwa viongozi wakuu wa nchi zote mbili.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Malawi, Ephraim Chiume, ameituhumu Tanzania kwamba imeanza kuzungumzia utatuzi wa mgogoro huo wakati ikijua kuwa mzozo huo uko katika hatua ya upatanishi maalumu.

Waziri Chiume aliikosoa kauli iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kuwa ufumbuzi wa mgogoro wa mpaka baina ya mataifa hayo mawili, unakaribia kupatikana.

Alisema kitendo cha Membe kuzungumzia maendeleo ya mgogoro huo kinapingana na makubaliano ya pamoja yaliyowasilishwa kwa Chissano na kwamba hatua hiyo inavunja moyo.

Waziri Chiume aliliambia gazeti la Nyasa Times kuwa pande zote mbili zilipokutana Nombemba 17 mwaka jana jijini Dar es Salaam, zilikubaliana kuzungumzia mgogoro huo ili kuepuka kuingilia juhudi za upatanishi.

Alisema hata hivyo, hivi karibuni ya Serikali ya Tanzania imekiuka sehemu ya makubaliano hayo.

"Tanzania wamevunja makubaliano, na sisi tunasisitiza kuwa Ziwa Nyasa ni la Malawi," alisema waziri.

Baadhi ya wachambuzi wa mambo, wamesema kauli huyo inaashiria kuwa huenda pande hizo mbili zikashindwa kukubaliana na mapandekezo yatakayowasilishwa na mpatanishi wa mzozo huo.

Mpatanishi huyo mwezi huu anatazamiwa kukutana na Rais Jakaya Kikwete na yule wa Malawi, Joyce Banda.

Hata hivyo, alivyotafutwa ili kuzungumzia malalamiko hayo, waziri Membe kupatikana, lakini Naibu wake Mahadhi Maalimu, alisema: "Ninachosema mimi kwanza hizo taarifa sijazipata na kama zipo basi Serikali itawasiliana kupitia mikondo sahihi. Serikali haiwezi kujibizana kupitia magazeti"

Hivi karibuni Serikali ya Tanzania na Malawi zilipeleka barua ya pamoja kwenye Jukwaa la Marais wa Wastaafu wa Nchi za Kusini mwa Afrika linaloongozwa Chissano, zikiomba zipatanishwe katika mzozo huo.

Hatua hiyo ilikuja baada ya majadiliano ya pande zote mbili kushindwa kuzaa matunda.

Kama sehemu ya kuepusha mgongano wa kimaslahi, jopo hilo la wasuluhishi halikuwahusisha viongozi wastaafu wa Tanzania Alhaji Ali Hassani Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Hali kadhalika Bakiri Muluzi wa Malawi.

Hata hivyo, duru za kidiplomasia mjini Lilongwe zinasema Serikali ya Malawi imejiandaa kwenda katika Mahakama ya Haki ya Kimataifa(ICJ) kama upatanishi huo utashindwa kuzaa matunda.

Gazeti la Daily Times limewanukuu maofisa wa Serikali wakisema kuwa karata ya mwisho kwa Malawi itakuwa ni kwenda katika mahakama hiyo.

Source: Mwananchi

Malawi wamekwisha chemka huko ndo mana wanajishtukia. Kuna kauli gani hapa ya kuingilia makubaliano wakati wao wameshaialika kampuni ya Africa kusini kuanza exploration na uchimbaji wa mafuta. Dawa yao ni kuwachapa tu mana wamekuwa watu wa kulalamika sana.
 
naona Malawi inaichezea shere TZ! binafsi sioni ubaya ktk kauli ya Mhe. Membe, At kusema 'ufumbuzi unakaribia kupatikana' ndo iwe nongwa!!!!
 
Sasa kama msuluhishi kashafikia hatua ya kutaka kuongea na wakuu wa nchi si ndio maana yake suluhu imekaribia kupatikana. Hawa wamalawi mbona wana matatizo hivi!!!
 
Malawi wamekwisha chemka huko ndo mana wanajishtukia. Kuna kauli gani hapa ya kuingilia makubaliano wakati wao wameshaialika kampuni ya Africa kusini kuanza exploration na uchimbaji wa mafuta. Dawa yao ni kuwachapa tu mana wamekuwa watu wa kulalamika sana.

Kufikiria kuwachapa ni hesabu za kujipotosha. "Mshindi wa ugomvi ni baada ya ugomvi"
 
naona Malawi inaichezea shere TZ! binafsi sioni ubaya ktk kauli ya Mhe. Membe, At kusema 'ufumbuzi unakaribia kupatikana' ndo iwe nongwa!!!!

This is information warfare. Kama mawaziri wetu wanakubaliana katika usuluhishi huu kwamba hawataongelea maendeleo ya usuluhishi, inabidi waheshimu makubaliano hayo, ama sivyo wanaweza kuwapa msemo Wamalawi ambao tunajua tangu mwanzo hawana nia ya suluhu katika suala hili.

Tatizo letu discipline ndogo. Waziri anaweza kusaini makubaliano kwamba hatazungumzia maendeleo ya usuluhishi, halafu kesho akaendeleza kidomodomo kwa kusema "usuluhishi unaendelea vizuri na suluhisho litapatikana karibuni".

Suala si kwamba kauli ni mbaya, suala ni kama umekubaliana kutoongelea maendeleo ya usuluhishi, ukiongelea maendeleo umevunja makubaliano na kumpa mpinzani wako msemo.

Je nini kilikubaliwa? Membe kasema nini? Membe kavuruga kilichokubaliwa?

Membe tangu aharibu issue ya Tanzania kuuzia silaha waasi wa Congo siwezi kumuamini katika mambo ya PR.
 
Watanzania tujitayarishe kwa vita vya kidiplomasia na kijeshi juu ya mpaka wetu na Malawi. Hawa jamaa hawaamini katika kuishi kwa pamoja (co-existence) na kuzingatia utawala wa sheria.
 
Malawi wamekwisha chemka huko ndo mana wanajishtukia. Kuna kauli gani hapa ya kuingilia makubaliano wakati wao wameshaialika kampuni ya Africa kusini kuanza exploration na uchimbaji wa mafuta. Dawa yao ni kuwachapa tu mana wamekuwa watu wa kulalamika sana.

raisi wenu si alisema tz haina uwezo wa kuichapa malawi? Sasa wataichapa je?
 
Kama vp waangalie nchi ambayo wananchi wake watanufaika na hiyo gas itakayopatikana huko ndo waipatie hilo ziwa na siyo kuwapatia wale watakaonufaishana wachache
 
This is information warfare. Kama mawaziri wetu wanakubaliana katika usuluhishi huu kwamba hawataongelea maendeleo ya usuluhishi, inabidi waheshimu makubaliano hayo, ama sivyo wanaweza kuwapa msemo Wamalawi ambao tunajua tangu mwanzo hawana nia ya suluhu katika suala hili.

Tatizo letu discipline ndogo. Waziri anaweza kusaini makubaliano kwamba hatazungumzia maendeleo ya usuluhishi, halafu kesho akaendeleza kidomodomo kwa kusema "usuluhishi unaendelea vizuri na suluhisho litapatikana karibuni".

Suala si kwamba kauli ni mbaya, suala ni kama umekubaliana kutoongelea maendeleo ya usuluhishi, ukiongelea maendeleo umevunja makubaliano na kumpa mpinzani wako msemo.

Je nini kilikubaliwa? Membe kasema nini? Membe kavuruga kilichokubaliwa?

Membe tangu aharibu issue ya Tanzania kuuzia silaha waasi wa Congo siwezi kumuamini katika mambo ya PR.

Hamna makubaliano yaliyo vunjwa hapo....... kusema tu muafaka karibu utapatikana ndiyo iwe kukiuka makubaliano...... au ndiyo kuelezea maendeleo ya usuluhishi...... Nilicho na uhakika ni kwamba Membe aliongelea kuwa karibu tutapata suluhu kwa kuangalia ratiba ya hiyo kazi ya usuluhishi.... maana hiyo haikuwa siri...... ilikuwa ikieleweka wazi kuwa Chisano ataanza kazi lini na kumaliza lini..... hivyo kusema muafaka u karibu..... na kweli uko karibu maana baadaye mwezi huu taarifa itawasilishwa kwa wakuu wa nchi husika....sasa hilo la kuvunja makubaliano linatokea wapi

wenyewe ndiyo wamekiuka kwa kiwango kisicho mithirika..... maana wameipa kampuni ya Afrika ya Kusini kufanya utafiti wa gesi na mafuta kwenye eneo la mgogoro.....
 
hapa inabidi umakini ingawa kuwachapa iwe suluhisho la mwisho
 
Makubaliano yapi?

Unayajua?

Membe anayeyajua kwa mujibu, kashindwa kuyakanusha. Wewe ulikuwepo kwenye mikutano yao?

You are not even privy to what you are refuting, how can I take you seriously?

Wahabeshi wawili wamedhulumiana Baghdad, mmoja anasema "huyu wa pili kanidhulumu kwa sababu kachukua ujira mara mbili, na makubaliano yalikuwa ujira ni mara moja"

Aliyetuhumiwa katafutwa kujieleza hapatikani.

Sie Waswahili Baghdad hatukuwepo na wala hatujui kilichoendelea, badala ya kuuliza Baghdad kiliendelea nini, makubaliano yalikuwaje, kwa nini mtuhumiwa hajajibu na kadhalika.

Tunakuja resi eti kumaka "hakuna makubaliano yaliyovunjwa hapo".

Kama vile tulikuwepo Baghdad.

Kama huyu Waziri wa Malawi anachosema ni kweli. Tatizo lako wewe na la Membe ni moja.

Nyote ni Watanzania mnaoishi katika nyakati ngumu kwa Mtanzania kuwa mwerevu.

We are mostly plagued by a low degree of attention to detail coupled with a highly misplaced and disproportionately trusting optimism.

If not unhealthy idiocracy altogether.
 
Makubaliano yapi? Unayajua? Membe anayeyajua kwa mujibu, kashindwa kuyakanusha. Wewe ulikuwepo kwenye mikutano yao? You are not even privy to what you are refuting, how can I take you seriously? Wahabeshi wawili wamedhulumiana Baghdad, mmoja anasema "huyu wa pili kanidhulumu kwa sababu kachukua ujira mara mbili, na makubaliano yalikuwa ujira ni mara moja" Aliyetuhumiwa katafutwa kujieleza hapatikani. Sie Waswahili Baghdad hatukuwepo na wala hatujui kilichoendelea, badala ya kuuliza Baghdad kiliendelea nini, makubaliano yalikuwaje, kwa nini mtuhumiwa hajajibu na kadhalika. Tunakuja resi eti kumaka "hakuna makubaliano yaliyovunjwa hapo". Kama vile tulikuwepo Baghdad. Kama huyu Waziri wa Malawi anachosema ni kweli. Tatizo lako wewe na la Membe ni moja. Nyote ni Watanzania mnaoishi katika nyakati ngumu kwa Mtanzania kuwa mwerevu. We are mostly plagued by a low degree of attention to detail coupled with a highly misplaced and disproportionately trusting optimism. If not unhealthy idiocracy altogether.
Tulia mkulu..... Ni tamko tu halijatolewa..... (Tangazo kwa Umma) Makubaliano yoote nayaelewa na hakuna sehemu iliyoelezea kuwa usitaje mwisho wa kazi aliyopewa Mzee Chisano.... (maafisa habari wataelezea hilo)...... Huyu Ephraim anajaribu kujihami......maana tayari wamempa mtu kazi ya kutafuta mafuta...... sasa kwa uelewa wako yupi ambaye amevunja makubaliano????
 
Chiume asiwe muoga kiasi hicho, uzuri mh Membe amezungumza kwa mtazamo wa heri si shari.
 
Tulia mkulu..... Ni tamko tu halijatolewa..... (Tangazo kwa Umma) Makubaliano yoote nayaelewa na hakuna sehemu iliyoelezea kuwa usitaje mwisho wa kazi aliyopewa Mzee Chisano.... (maafisa habari wataelezea hilo)...... Huyu Ephraim anajaribu kujihami......maana tayari wamempa mtu kazi ya kutafuta mafuta...... sasa kwa uelewa wako yupi ambaye amevunja makubaliano????

Makubaliano unayaelewa kuliko Membe ambaye kashindwa kujitetea?
 
Back
Top Bottom