Malawi wameiva kidiplomasia kuliko Tanzania?

Mkuu,

Wajua Vita ni aina mojawapo ya Diplomasia inayofuata baada ya kushindwa kwa majadiliano. Hata mafunzo/ mazoezi ya Kijeshi yanayoendelea pamoja na kusogeza majeshi mpakani?
 
Malawi imesitisha shughuli za kutafuta mafuta na gas kwenye eneo la ziwa Nyasa lenye utata. Tanzania ilionekana kuchachamaa na kutaka kupigana vita. Je, aliyetaka kupigana na ambaye ameamua kufuata njia zinazofaa kimataifa ni yupi amekomaa kisiasa na kidiplomasia? Malawi haikuwa na option ya vita on the table lakini Tanzania ilionesha kuwa na option hiyo on the table, je haikuwa tayari deals za kununua silaha na matumizi mabovu katika vita zimechongwa? Thanks Malawi for the wisest decision!!

Source: Mwananchi 10/08/2012
Gazeti la Malawi linasema Tanzania is war-mongering,wakati mgogoro umeanzishwa na Foreign Minister wao kusema Lake Malawi yote ni yao,sasa who is war mongering? Hii labda inaonyesha udhaifu wa Jk,kwa sababu muda mrefu Malawi imekaa kimya kuhusu huo mpaka;au inaonyesha ujeuri Wa Joyce Banda,ambaye alomost she did not become President,sasa anataka kuanzisha vita kuwaunganisha watu wake.
This is bad,wewe una hofu kwamba Tanzania is immature,mimi nina hofu hiyo hiyo,this problem is not over until it is over.
 
premitive negro...dont be brainwashed by arabs who own all tanzania. They r just using u black man.
 
Nadhani unazungumzia miaka ya sabini!

Sikuwepo huko nazungumzia juzi tu wakati waTZ wameenda kwenye mkutanio wa umoja wamataifa, Nchi za kiafrika wanaulizwa nini sera yenu ya mambo ya nje?
Wote wanawageukia waTZ nakuuliza eti sera yenu nyinyi ni ipi?
Haya wakawambia ni diplomasia ya kiuchumi wote wakaanza kuimba jamanani it is economic diplomacy.lol!
We still at the top binam!
 
Suali lako nadhani umejijibu tayari.vita ikitokea kuna watu wataneemeka sana ingawa nadhani tukutane nao mahakamani tu tujue pumba na mchele ni zipi.Kingine nawaza kuna haja gani ya kugombania hayo mafuta wakati rasilimali nyingine tumeshindwa kuzitumia vizuri ili zitusaidie kujiendeleza.si tuwaachie tu hao Wamalawi ????
 
HILO ZIWA MALI YA MALAWI .PIA BURUNDI NA RWANDA NI MALI YA TANGANYIKA KWA MUJIBU WA HELIGOLAND TREATY.
mm yt macho!
 
Sijui kama kweli Malawi wameiva kidiplomasia kwani matamshi ya waziri wa mambo ya nje ya awali yalikuwa ya kibabe. Nadhani kuwa huyu mama rais wa malawi ndiye ana busara zaidi kuliko hata Lowasa na Sitta. Viongozi hawa wa Tanzania walifanya makosa makubwa ya kidiplomasia kuanza kutangaza uwezekano wa kupeleka majeshi mpakani na hivyo kusababisha mtafaruku wa kidplomasia ambao haukuwa wa lazima. Ingawa sheria za kihistoria zinayumba sana kuhusu mpaka huo (nina collection ya documents nyingi sana za kiingereza, kijerumani na za kireno zilizoandikwa kati ya mwaka 1883 na mwaka 1910 ambazo zinacomplicate madai ya nchi zote mbili), Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuliko Malawi inatakiwa ndiyo iwe na busara zaidi katika kutatua mgogoro wa mpaka huo. Mimi ningekuwa nina madaraka kwenye serikali ya Tanzania huenda ningekubali kuwapa wamalawi kitu fulani nchini Tanzania (ambacho hawana huko Malawi) kusudi tumalize kwa amani bila hata kuingiliwa na mataifa ya nje mgogoro huu wa mpaka ambao umedumu tangu tupate uhuru. Kwa mfano nigewapa gati maalumu bandarini Dar na kuwapa eneo maalumu kwa ajili yao tu kwa miaka hamsini au zaidi ili wawezekutumia eno hilo na gati hilo kusafirishia na kupokea mizigo yao nje ya nchi bila kuingiliwa na mamlaka ya Tanzania, yaani iwe kama vile wako Malawi tu. Chini ya mkubaliano hayo nigewakubalia pia kuwaruhusu watu wao idadi kadhaa waje kufanya kazi kwenye gati hilo kwa masharti rahisi sana. Iwapo wakoloni walikuwa wanaweza kuandikiana Treaties ambazo leo ndiyo eti zinatuongoza zaidi ya karne moja, ni aibu kwetu kushindwa kumaliza mgogoro huu mdogo kwa kuweka treaties zetu tunazokubalina nazo bila kupigana.
Mkuu sio kutishia kupeleka majeshi mpakani majeshi yetu tayari yapo mpakani na vifaa vya kutosha wanasikilizia outcome ya hayo mazungumzo
 
Back
Top Bottom