GAGL
JF-Expert Member
- Aug 5, 2010
- 391
- 400
Gazeti la jana la Mwananchi la jana, liliripoti kuwa wiki ijayo kutakuwa na maandamano makubwa kukamilisha mpango wa kumuondoa Rais Mutharika madarakani kwa nguvu ya umma. Nafurahia hatua hii kwa kuwa naamini itatuambukiza na sisi pia kuchukua hatua kwa viongozi ambao kiukweli hakuna wanachofanya kutuondolea hali ngumu ya maisha. Hali ya serikali yetu na mwenendo wake, imetufanya wengine tuathirike kisaikolojia kwa kweli.