Hili ziwa kwa Watanzania linajulikana kama ziwa NYASA wakati kwa Wamalawi linaitwa ziwa MALAWI. Kwa angalizo hili, tunaona kuwa, kinachopiganiwa ni maziwa mawili katika ziwa moja.
Kwa hiyo kwa Tanzania kununua chombo cha kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi wake haitakiwi kwa vile haijulikani hizi meli zitafanya safari katika ziwa lipi ndani ya ziwa moja.
Chanzo cha huu mgogoro siyo nchi ya Malawi bali ni hizi kampuni za Kiingereza hasa hii inayoitwa Surestream Petroleum.
Wamalawi wamekuwa ni REMOTE CONTROL kuhakikisha hii kampuni inapata kile inachokitaka kwa amani na shari.
Mambo kama haya ndiyo yalipelekea hawa Waingereza mwaka 2004 kukodisha mercenary wakiongozwa na former British Army Officer, Simon Mann ambaye alikuwa anapata pesa za mpango huo kutoka kwa mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Hilda Thatcher.
Rais Mugabe aliwabana Airport na deal lao likaishia hapo Airport pamoja na kwamba nia yao ilikuwa ni kufanya coup d'etat kwa kumteka au kumuua Rais Teodoro Obiong Mbasogo wa Equatorial Guinea.
Hawa jamaa wao vita zinawawezesha kwanza kuuza siraha ili muundelee kuuana wakati wao wakiendelea kuiba malighafi wakati nchi iko busy na vita.
Hili swala linahitaji zaidi ya uwezo wa kidiplomasia kulimaliza kwa amani pamoja na kwamba nasikia kuna kelele za watu hapa wanataka tuende vitani bila kujua kama hatutapigana na Malawi bali na wadau wa malighafi za Malawi.