Malawi: Tunapinga Tanzania kupeleka Meli Ziwa Nyasa (Malawi).

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Nchi ya Malawi imepinga na kulalamika kuhusiana na kusudio la Tanzania kupeleka meli mbili za abiria katika ziwa Nyasa na kudai, kitendo cha kufanya hivyo kitaadhiri na kutishia mazungumuzo yanayotafuta suruhisho la muda mrefu ili kulimaliza mzozo wa ziwa Nyasa (malawi) uliodumu kwa muda mrefu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Efraimu Chiume alikaririwa jumamosi akisema, kwamba viongozi wa juu wa serikali ya Tanzania walisikika hadharani wakisema kwamba serikali ina mpango wa kununua meli sita na mbili zitapelekwa ziwa Malawi kusaidia kuondoa tatizo la usafiri.

Waziri Chiume alidai mpango wa kupeleka meli ziwa Nyasa (malawi) umekuja katika hali ambayo siyo mwafaka ikichukuliwa kuwa mazungumzo yalikuwa yanaendelea bila matatizo.

Maofisa wa serikali ya Tanzania hawakuweza kupatikana kuliongelea swala hili.

Malawi ambayo iko upande wa magharibi mwa ziwa inadai kumiliki nusu yote ya upande wa kasikazini mwa ziwa na huku Tanzania ambayo iko upande wa mashariki nayo ikidai kumiliki nusu ya upande wa kaskazini ya ziwa wakati nusu ya kusini mwa ziwa ikimilikiwa na Malawi na Msumbiji kwa pamoja.

Mwezi uliopita malawi ilirudi kwenye mazungumzo ambayo mwanzo ilijitoa baada ya kuilalamikia Tanzania kwa kuwatisha wavuvi wa Malawi, madai ambayo Tanzania iliyakanusha.

Mzozo kwa kiwango kikubwa umesababisha kukwama kwa utafutaji wa gesi asilia na mafuta katika ziwa Nyasa.

Mwaka jana serikali ya Malawi iliiruhusu kampuni ya Kiingereza inayoitwa Surestream Petroleum kuanza kutafuta mafuta.

Habari kwa hisani ya Reuters.
 
Hili ziwa kwa Watanzania linajulikana kama ziwa NYASA wakati kwa Wamalawi linaitwa ziwa MALAWI. Kwa angalizo hili, tunaona kuwa, kinachopiganiwa ni maziwa mawili katika ziwa moja.

Kwa hiyo kwa Tanzania kununua chombo cha kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi wake haitakiwi kwa vile haijulikani hizi meli zitafanya safari katika ziwa lipi ndani ya ziwa moja.

Chanzo cha huu mgogoro siyo nchi ya Malawi bali ni hizi kampuni za Kiingereza hasa hii inayoitwa Surestream Petroleum.

Wamalawi wamekuwa ni REMOTE CONTROL kuhakikisha hii kampuni inapata kile inachokitaka kwa amani na shari.

Mambo kama haya ndiyo yalipelekea hawa Waingereza mwaka 2004 kukodisha mercenary wakiongozwa na former British Army Officer, Simon Mann ambaye alikuwa anapata pesa za mpango huo kutoka kwa mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Hilda Thatcher.

Rais Mugabe aliwabana Airport na deal lao likaishia hapo Airport pamoja na kwamba nia yao ilikuwa ni kufanya coup d'etat kwa kumteka au kumuua Rais Teodoro Obiong Mbasogo wa Equatorial Guinea.

Hawa jamaa wao vita zinawawezesha kwanza kuuza siraha ili muundelee kuuana wakati wao wakiendelea kuiba malighafi wakati nchi iko busy na vita.

Hili swala linahitaji zaidi ya uwezo wa kidiplomasia kulimaliza kwa amani pamoja na kwamba nasikia kuna kelele za watu hapa wanataka tuende vitani bila kujua kama hatutapigana na Malawi bali na wadau wa malighafi za Malawi.
 
Tulikuwa na MV Ludewa ziwa Nyasa, tena enzi za Kamuzu .... Sidhani kama ni jambo la busara kuongea nao under the precedent kuwa ziwa ni lao mpaka sasa.

Tnafanya mazungumzo under the precedent kuwa tupo ziwani, wananchi wetu wanalitumia hilo ziwa, tuna Naval base Mbozi ziwani kabisa tangu enzi za Nyerere, kuna ptrol boats za jeshi ndani ya ziwa na tumekuwa na passenger boats za Tanzania under our maritime laws/jurisdiction.

Kwanini wanajifanya hawajui hayo???
 
Wanatumika...

Si haba...
Huwezi kuwaambia wananchi wa Kasulo, Mbamba Bay wasitumie ziwa eti kwa kuwa mazungumzo yanaendelea...
Kila nchi iendelee kutumia upande wake kama ilivyokuwa awali...
 
Wanatumika...

wacha watumike. kwanin nyinyi mlivokuamnatumika na mataifa ya nje dhidi ya mataifa dhaifu na majiran zenu.mliona mmefika. sasa waacheni na wao. ndo mchezo wa kichawi wakiisha mnageukiwa na nyinyi
endeleeni malaw na moto wenu. hawa jamaa kelele nyngi hawana kitu labda ulevi
 
Hili ziwa kwa Watanzania linajulikana kama ziwa NYASA wakati kwa Wamalawi linaitwa ziwa MALAWI. Kwa angalizo hili, tunaona kuwa, kinachopiganiwa ni maziwa mawili katika ziwa moja.

Kwa hiyo kwa Tanzania kununua chombo cha kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi wake haitakiwi kwa vile haijulikani hizi meli zitafanya safari katika ziwa lipi ndani ya ziwa moja.

Chanzo cha huu mgogoro siyo nchi ya Malawi bali ni hizi kampuni za Kiingereza hasa hii inayoitwa Surestream Petroleum.

Wamalawi wamekuwa ni REMOTE CONTROL kuhakikisha hii kampuni inapata kile inachokitaka kwa amani na shari.

Mambo kama haya ndiyo yalipelekea hawa Waingereza mwaka 2004 kukodisha mercenary wakiongozwa na former British Army Officer, Simon Mann ambaye alikuwa anapata pesa za mpango huo kutoka kwa mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Margaret Hilda Thatcher.

Rais Mugabe aliwabana Airport na deal lao likaishia hapo Airport pamoja na kwamba nia yao ilikuwa ni kufanya coup d'etat kwa kumteka au kumuua Rais Teodoro Obiong Mbasogo wa Equatorial Guinea.

Hawa jamaa wao vita zinawawezesha kwanza kuuza siraha ili muundelee kuuana wakati wao wakiendelea kuiba malighafi wakati nchi iko busy na vita.

Hili swala linahitaji zaidi ya uwezo wa kidiplomasia kulimaliza kwa amani pamoja na kwamba nasikia kuna kelele za watu hapa wanataka tuende vitani bila kujua kama hatutapigana na Malawi bali na wadau wa malighafi za Malawi.

Kweli kwani nchi za magharibi zimekuwa na zoezi endelevu la kuanzisha chokochoko za kivita Africa na kufahidi kwa kuiba rasilimali zetu pamoja na kutuuzia silaha
 
Hawa malawi kunakitu kimejificha nyuma siku moja watakisema tu tunawasubili kwanza walishaunga mkono ushoga kwa hiyo siyo ndugu zetu.
 
Haya sasa tuangalie kati ya president mwanamke na president mwanaume nani zaidi?
 
Kwa hiyo wanataka kutuambia kuwa wananchi wetu wanaovua katika Ziwa Nyasa wanafanya hivyo kwa hisani ya watu wa Malawi? Au na wao waache kuvua kwanza kwa vile tuko kwenye mazungumzo?
 
Hii kitu inasikitisha sana ila bado mapema ukweli kuifikia jamii...

Naamini mda utafika siri zitavuja tu.
 
wacha watumike. kwanin nyinyi mlivokuamnatumika na mataifa ya nje dhidi ya mataifa dhaifu na majiran zenu.mliona mmefika. sasa waacheni na wao. ndo mchezo wa kichawi wakiisha mnageukiwa na nyinyi
endeleeni malaw na moto wenu. hawa jamaa kelele nyngi hawana kitu labda ulevi

Wewe sio mtanzania, afu nahisi utakuwa Mliberali tu.. huwezi ongea pumba hivi... nimekutukana
 
chadema umeungana na rwanda,m23 na sasa malawi et mnatafuta umaarufu kimataifa.hatuwezi acha kutekeleza irani ya uchaguzi kwa maneno ya chiume
 
kikwete shusha batalion moja hapo kwa huyo maza tumalize mazungumzo
 
Serikali ya Malawi wana lao jambo...

Hapana shaka katika hili........hawa watakuwa wamekubaliana na serikali yetu kuwa kwa vile ahadi ya kununua meli haitekelezeki basi Wamalawi "waibebe" serikali yetu ili ionekane kuwa kununua meli kwa sasa haiwezekani kutokana na mgogoro wa mpaka wakati ukweli ni kuwa serikali haina uwezo wa kununua meli hiyo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom