Bukyanagandi
JF-Expert Member
- Jun 24, 2009
- 11,061
- 16,743
Heshima yako mkuu, sina shaka unajua makao makuu ya REUTERS yako wapi na ni Kampuni ya akina nani; hilo tu ndilo litakupa picha kamili ni kitu gani kinaendelea behind the SCENE. Hivi hii kampuni ya Kiingereza (Surestream Petroleum) bado inaendelea na utafiti wake wa mafuta katika Ziwa Nyasa au walitii AMRI ya Serikali ya TANZANIA?Nchi ya Malawi imepinga na kulalamika kuhusiana na kusudio la Tanzania kupeleka meli mbili za abiria katika ziwa Nyasa na kudai, kitendo cha kufanya hivyo kitaadhiri na kutishia mazungumuzo yanayotafuta suruhisho la muda mrefu ili kulimaliza mzozo wa ziwa Nyasa (malawi) uliodumu kwa muda mrefu. Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Efraimu Chiume alikaririwa jumamosi akisema, kwamba viongozi wa juu wa serikali ya Tanzania walisikika hadharani wakisema kwamba serikali ina mpango wa kununua meli sita na mbili zitapelekwa ziwa Malawi kusaidia kuondoa tatizo la usafiri. Waziri Chiume alidai mpango wa kupeleka meli ziwa Nyasa (malawi) umekuja katika hali ambayo siyo mwafaka ikichukuliwa kuwa mazungumzo yalikuwa yanaendelea bila matatizo. . . . . Mwaka jana serikali ya Malawi iliiruhusu kampuni ya Kiingereza inayoitwa Surestream Petroleum kuanza kutafuta mafuta. Habari kwa hisani ya Reuters.