Malawi kupiga marufuku 'kupumua'?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,864
30,322
Malawi kupiga marufuku 'kupumua'?


110204064606_sp_fart_226i.jpg
Malawi kukataza watu kujamba?


Mzozo umezuka nchini Malawi kufuatia mapendekezo kutaka kufikishwa bungeni kuhusu kujamba, kuwa ni kosa.
Waziri wa sheria wa Malawi, George Chaponda amesema muswada huo utakaojadiliwa kuwa sheria ndani ya bunge wiki ijayo, utapiga marufuku kabisa kwa mtu kufanya haja hiyo hadharani. Waziri huyo amekiambia kituo kimoja cha radio nchini humo- kwa maneno yake - "nenda chooni kama unajisikia kujamba".
Hata hivyo mkuu wa wanasheria nchini Malawi Anthony Karanga amesema kufanya haja hiyo hakufikii kuharibu hali ya hewa kiasi cha kuwa kosa la jinai.
Mwandishi wa BBC nchini humo anasema wananchi wa Malawi wanajiuliza mapendekeo ya sheria hiyo, iwapo itapitishwa, itatekelezwaje.

Chanzo:BBC Swahili - Habari - Malawi kupiga marufuku 'kupumua'?

Je Wa Tanzania Mtaweka sheria za Kupumua Hadharani? :ban::yield::love::love:
 

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,358
Bongo kuweka sheria ni rahisi sana ila utekelezaji wake ni ndoto
 

Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,592
5,337
mbona sheria hii ilisha pitishwa bngeni kule malawi? sema ni vigumu kukata sentensi sababu ushahidi unapotea haraka. na pia sanction inafwata watu uliowaudhi na sio rahisi watu kujitokeza kumshtaki convict...
Vitu vingine vinavyo shindw kueleweka ni swala la wagonjwa, na recidivisim (kurudia kosa).
Kazi ipo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom