Malalamiko ya waendesha Bodaboda wa Mkuranga,Kibiti kupitia 93.7 Fm Efm Redio leo asubuhi

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,358
Kupitia kipindi cha redio ya Efm Leo asubuhi waendesha Bodaboda wanalalamika kunyanyaswa na Polisi na kuharibiwa pikipiki zao wanazotumia kwa muda wa jioni au usiku.

Polisi ilishatoa tangazo na ilani yao kuwa Mwisho wa Bodaboda ni saa 12 jioni sasa wewe saa 3 usiku Unapenda wapi kama mmoja wa niliyemsikia alikamatwa saa 3 usiku.

Niwasihi tu waendesha bodoboda kuwa huitaji kulazishishwa kutii amri ya Polisi ni uamuzi wako kutii au kutotii lakini ujue tu madhara ya kutotii amri ya Polisi ni yapi.

Hii operation haijulikani itaisha lini ushirikiano wako ni muhimu tu.

Na usiku hujazuiwa kutoka mfano kuna wagonjwa, wajawazito ambao wanahitaji Huduma muda wowote Polisi haiwezi kuzuia watu kama hawa kupata Huduma.
 
Hawa wananchi wasipolindwa wanalalama na wakilindwa wanalalama...saa 3 unatafuta nini barabarani ukiwa na boda boda?

Nakumbuka loliondo wasomali wengi sana walifichwa kwenye maboma ya wamasai.
 
wagonjwa wakizidiwa hawapelekwi hospitalini kuanzia saa 12 jioni??
Mgonjwa anapelekwa hospitali muda wowote ili mradi ni mgonjwa.

Mjamzito akipatwa na uchungu muda wowote anapelekwa kujifungua haijulishi ni usiku wa saa ngapi na haijazuiliwa.
 
Kuna mashamba yangu huko mkuu, vipi nikija kukagua kazi niliyo iacha usalama upo?
Hakuna shughuli zilizositishwa kufanywa nje ya muda Polisi waliosema kila mmoja awe kwake na Bodaboda zisitembee
 
Sawa, ntakuja mapema mkuu, ila itabidi nitembee na bastola yangu kwa ajili ya kujihami..
 
Hakuna shughuli zilizositishwa kufanywa nje ya muda Polisi waliosema kila mmoja awe kwake na Bodaboda zisitembee
Jibu la kijinga, kwahiyo kila mwenye duka liko nybani kwake, kila mwenye shamba shamba liko nyumbani kwake?
 
Kupitia kipindi cha redio ya Efm Leo asubuhi waendesha Bodaboda wanalalamika kunyanyaswa na Polisi na kuharibiwa pikipiki zao wanazotumia kwa muda wa jioni au usiku.

Polisi ilishatoa tangazo na ilani yao kuwa Mwisho wa Bodaboda ni saa 12 jioni sasa wewe saa 3 usiku Unapenda wapi kama mmoja wa niliyemsikia alikamatwa saa 3 usiku.

Niwasihi tu waendesha bodoboda kuwa huitaji kulazishishwa kutii amri ya Polisi ni uamuzi wako kutii au kutotii lakini ujue tu madhara ya kutotii amri ya Polisi ni yapi.

Hii operation haijulikani itaisha lini ushirikiano wako ni muhimu tu.

Na usiku hujazuiwa kutoka mfano kuna wagonjwa, wajawazito ambao wanahitaji Huduma muda wowote Polisi haiwezi kuzuia watu kama hawa kupata Huduma.
Mipasho kazini
 
Jibu la kijinga, kwahiyo kila mwenye duka liko nybani kwake, kila mwenye shamba shamba liko nyumbani kwake?
Hata kama ni jibu ni la kijinga lakini haibadili amri ya Polisi kuhusu muda wa raia kuwa ktk makazi yao na vyombo vya usafiri hususani Bodaboda kutotembea kuanzia saa 12 jioni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom