Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Ni takribani siku nne, kumekuwa na mjadala mzito umeibuka baada ya taarifa kuwa vijana wawili wanaodai kuandika barua ya malalamiko kwa Balozi wa Vatican (Papal Nuncio), Archbishop Angelo Accatino wakimshtaki Padre Charles Kitima. Tukio hili limeibua maswali makubwa si tu juu ya madai yenyewe, bali zaidi juu ya uelewa mdogo wa taratibu na mchakato rasmi wa Kanisa Katoliki la Roma katika kushughulikia tuhuma za mwenendo mbaya wa makasisi na watumishi wake.
Kanisa Katoliki haswa la Roma, ni moja ya sehemu zenye utofauti mkubwa sana na taasisi za kisiasa au majukwaa ya kijamii, haliongozwi kwa makelele ya televisheni, Instagram, Facebook au TikTok, hotuba za kinafiki au malalamiko ya maneno ya kuongea vijiweni.
Vatican haisikilizi malalamiko ambayo ni “verbal”, wala haifanyi maamuzi kwa misingi ya presha ya vyombo vya habari, hata kituo kama EWTN ambacjo ndio chombo kinachorusha taarifa za kikatoliki bado huwa kinakula za kichwa wakienda vibaya. Kanisa Katoliki lina utaratibu wa kisheria (canon law) unaohitaji nidhamu, utambulisho, na ushahidi sio porojo.
Tatizo la msingi kwa vijana hawa wawili, Stanslaus Nyakunga pamoja na mwenzake Elia Phaustine linaonekana kuwa ni kutokuelewa kabisa nani anaandika, kwa nani, na kwa msingi upi.
Barua yoyote inayokwenda kwa Papal Nuncio lazima ianze kwa kujitambulisha kikamilifu: jina kamili, mawasiliano, jimbo (diocese) wanakotoka, na parokia (parish).
Lakini pia hata hali yao ya kikanisa—je, wamebatizwa? Je, ni Wakatoliki halali na hai? Kanisa Katoliki haliwezi kushughulikia kwa uzito malalamiko ya mtu ambaye hata hajathibitisha uhusiano wake wa kimsingi na Kanisa lenyewe au Makandokando?
Wakatoliki wanaelewa vyema, fuatilia maziko ya mkatoliki halisi na mtu ambaye sio mhuni utaelewa. Lakini pia je mmepata ushauri kutoka kwa Viongozi wa VIWAWA katika parokia zenu mkiwa kama vijana wa kanisa?
Ni muhimu kusisitiza jambo moja linalopuuzwa sana: kuvaa Rozari shingoni hakumfanyi mtu awe Mkatoliki. Ni wazi kuwa rozari takatifu ni chombo cha sala, ila si kitambulisho cha imani ya mtu.
Ukatoliki halisi unatambuliwa kwa sakramenti, hasa sakramenti ya ubatizo, pamoja na Ekaristi takatifu. Bila uthibitisho wa hilo, mlalamikaji anabaki kuwa ni makandokando tu, mtu mzushi anayetoa maoni kwa Mama Kanisa pasipo kuhusika moja kwa moja na Kanisa.
Ukiachana na Roman Catholic kuna wale wa wakatoliki wa Mashariki kama, Maronite , Melkite, Syro-Malabar, pamoja na Syro-Malankara ambao wote hawa wanatumia Rosari takatifu kwenye kusali. Hivyo suala la Stanslaus na mwenzake Elia kuvaa rozari sio kigezo kuwa ni wakatoliki.
Zaidi ya hapo, mchakato wa Kanisa ni wa ngazi. Malalamiko dhidi ya padre huanza kwa askofu wa jimbo husika. Mfano, kama wakatoliki wanaosali Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, wna wasiwasi na Padri Stephen Mvili, basi wanaanza kupeleka malalamiko yao kwa Askofu Mhashamu Romanus Mihali.
Kama askofu anahusika au ameshindwa kuchukua hatua, ndipo malalamiko yanaweza kupelekwa kwa ngazi ya juu zaidi—ikiwemo Papal Nuncio. Kuruka hatua hizi bila sababu nzito ni sawa na kujaribu kukata rufaa bila kesi ya awali.
Barua ya malalamiko pia haiandikwi kwa lugha ya jazba, kejeli au lawama za jumla. Vatican inahitaji taarifa za ukweli: tarehe, mahali, matukio mahsusi, mashahidi kama wapo, na ushahidi wowote unaoweza kuthibitishwa. Maneno ya “inasemekana”, “nilisikia fulani akisema” au “kijiwe fulani cha kahawa wanasema” hayana uzito wowote katika mfumo wa Kanisa Katoliki.
Kimsingi, kilichojitokeza hapa ni funzo pana kwa waumini na jamii kwa ujumla: Kanisa Katoliki ni taasisi ya karne nyingi yenye taratibu zake, si jukwaa la mitandao ya kijamii.
Haki ndani ya Kanisa haipatikani kwa makelele, bali kwa kufuata njia na utaratibu. Bila hivyo, hata malalamiko ya kweli yanaweza kupotea njiani—si kwa sababu hayana msingi, bali kwa sababu hayakuwasilishwa kwa namna iliyo rasmi.
Mwisho, sauti ya waumini ni muhimu, lakini sauti hiyo lazima iambatane na nidhamu, utambulisho na ukweli. Bila hivyo, barua yoyote, hata ikifika Vatican, inaweza kubaki kuwa karatasi tu isiyo na uzito wa kisheria wala wa kichungaji.
Ila nina imani kabsa kuwa Stanslaus na mwenzake Elia sio waumini wa Kanisa la Roman Catholic, nina uhakika wa 100%, wangekuwa wakatoliki wangefahamu namna ya kuwasilisha malalamiko yao bila kuita press za kipuuzi.
Kwa muktadha huu ilikuwa ni halali kabsa na busara kwa Archbishop Jude Thaddeus Rwai’chi OFMCap kusema kuwa hawa ni Malofa.