Malalamiko kuhusu uongozi wa NSSF

Hivi vitu ni vya kawaida hasa miaka ya uchaguzi mkuu.

Pesa zinakusanywa ktumika kwenye uchaguzi mkuu, kumbuka donor waligoma kutoa pesa baadhi ya miradi, na sasa inagharimiwa na serikali ingawa kwa kusuasua, unadhani pesa inatoka wapi?!

Kila sehemu wanalia lakini tatizo ni uchaguzi wa mwisho wa mwaka.

Wanaopelekewa pesa ni kwa mkakati wa serikali tena nao hupata kidogo huku wakiangalia wapi pa kupata pesa.

Siasa ndizo zinaleta yote haya, usiumize kichwa saana.
 
Na waliandika sana humu jf sijui jamaa alihonga ilifutwa, wala hakuchuliwa hatua zozote leo kakabidhiwa dude mtashaa
Nakumbuka hata chief accountant wa ppf aliondolewa kimizengwe baada ya kutokukubaliana na ubadirifu uliokuwa unafanywa na Erio na wenzake hasa ktk kujilipa zaidi ya 200m kila baada ya miaka miwili.
Sasa nasikia amekuja na mbinu hyo kivingine, eti kujilipa 40% ya mshahara wa mwaka kila baada ya miaka mitatu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KOSA KUBWA MH MAGUFURI KAFANYA NIKURUDISHA WAKURUGEZNI WALIOFERI KUENDELEA KUENDESHA MASHIRIKA KAMA PSPSF NA NSSF. HUYU URIO SIJUI ANABEBWA KWA KUWA YAKUJUANA NA MKAPA LABDA LAKINI UKWELI NSSF NI TAASISI INATOA MATESO MAKUBWA SANA KWA WANACHAMA.MWANZO NILIDHANI NIKIBURI CHAO TU CHA WAFANYAKAZI WA CHINI LAKINI ANGALU MFANYAKAZI WA NDANI ANAONYESHA KUWA MAKAO MAKUU HAWAWASAPORT WATU WA CHINI NA MATOKEO YAKE HATA SISI WANACHAMA TULIFUNGUA MADAI YA KUKOSWA AJIRA KWA MJIBU WA SHERIA HATUJAPATA MAFAO YETU LICHA YA KUWA TUMEFUNGUA MIENZI MITANO ILIYOPITA NA HAKUNA MAJIBU.
mH MAGUFURI, NSSF KUNASHIDA KUBWA INABIDI IFANYIWE KAZI. NI AHERI HATA MCHECHU ALIKUWA ANADELIER INGAWA AWAMU HII ILIMUCHUKIA SANA
Ni Erio na siyo Urio
 
KOSA KUBWA MH MAGUFURI KAFANYA NIKURUDISHA WAKURUGEZNI WALIOFERI KUENDELEA KUENDESHA MASHIRIKA KAMA PSPSF NA NSSF. HUYU URIO SIJUI ANABEBWA KWA KUWA YAKUJUANA NA MKAPA LABDA LAKINI UKWELI NSSF NI TAASISI INATOA MATESO MAKUBWA SANA KWA WANACHAMA.MWANZO NILIDHANI NIKIBURI CHAO TU CHA WAFANYAKAZI WA CHINI LAKINI ANGALU MFANYAKAZI WA NDANI ANAONYESHA KUWA MAKAO MAKUU HAWAWASAPORT WATU WA CHINI NA MATOKEO YAKE HATA SISI WANACHAMA TULIFUNGUA MADAI YA KUKOSWA AJIRA KWA MJIBU WA SHERIA HATUJAPATA MAFAO YETU LICHA YA KUWA TUMEFUNGUA MIENZI MITANO ILIYOPITA NA HAKUNA MAJIBU.
mH MAGUFURI, NSSF KUNASHIDA KUBWA INABIDI IFANYIWE KAZI. NI AHERI HATA MCHECHU ALIKUWA ANADELIER INGAWA AWAMU HII ILIMUCHUKIA SANA

Erio ni mtoto wa dadake mkapa hagusiki, ana mainformer wa usalama hivyo hata mnaomsema humu hamko salama,
Ila kama ikimpendeza Rais basi asikilize maoni ya watu huenda kuna jambo kwa huyu bwana Erio
 
Tunaandika kwa masikitiko na malalamiko makubwa kuhusu hali ilivyodorora ndani ya shirika.

Tunaomba malalamiko haya yakufikie Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunasema hivyo baada ya hali kuonyesha wazi Waziri husika hana uwezo wa au amezembea kutatua matatizo ya sasa ya shirika

Ikumbukwe Mkurugenzi Mkuu ni kati ya wakurugenzi wazoefu waliokuwepo tangu awamu zilizopita. Na ni miongoni mwa Wakurugenzi wajanja sana ambao bila jicho pevu utashindwa kuelewa mapungufu au maovu yake.

Hivyo basi ni Mkurugenzi ambaye labda Mawaziri strong na wenye kufuatilia details kama Lukuvi ndiyo atamuweza.

HISTORIA YAKE

Alitokea PPF. Kwa wanaojua au Mh Rais ukitaka ukweli uliza ripoti za SSRA zilizoonyesha PPF ilikuwa ni miongoni mwa taasisi za hifadhi ya jamii ambazo zilikuwa chini kiufanisi, japo kiujanja ujanja na kutumia vyombo vya habari alionyesha picha tofauti na ukweli.

Ni mzoefu na mpika data kama aliweza kudanganya kuhusu idadi ya wanachama tu unategemea nini kwenye masuala nyeti zaidi kama ya fedha?

Kashfa ya ubadhirifu wa fedha akiwa PPF haikuwa siri. Mh Rais ukitaka kufukua haya ni kazi ndogo tu, naamini una watu wengi unaoweza kuwatuma wakathibitisha hili.

Sasa kama mtu alishindwa kusimamia kwa uhanisi taasisi ndogo kama PPF, ataweza vipi taasisi kubwa zaidi ya NSSF?

Kuutumia Usalama wa Taifa kwa maslahi binafsi. Mkurugenzi huyu ni miongoni mwa wakurugenzi wanaotumia baadhi ya staff wa usalama wataifa kwa maslahi yao binafsi.

Mtindo huu ulianza toka awamu zilizopita, lakini huyu anaendeleza mpaka sasa hivi.

Kwa wasioelewa baadhi ya staff wa UT wamekuwa wakilipwa kisiri (maarufu kama wako kwenye payroll ya Mkurugenzi) na wao kutumiwa na Mkurugenzi kwa maslahi binafsi kama kupewa taarifa za siri, kutengeneza zongwe kwa anaoamini ni wabaya wake, kutengeneza mazingira ya kuonyesha Mkurugenzi ni mchapakazi na muadilifu nk. Mh R naamini kwa kuwatumia baadhi ya staff wa UT waadilifu unaweza ukapata ukweli wa jambo hili

NDANI YA NSSF

Pamoja na kwamba NSSF ilikuwa inafanya vizuri ukilinganisha na PPF bado alipoingia hakutaka kujifunza mazuri na mapungufu ya shirika ili kuboresha vizuri, bado hakutaka kuendesha shirika kwa misingi ya uwazi na kuaminiana, bali kwa mbinu zilezile za PPF.

Na hapa kafanya mambo mengi ambayo ni kinyume na kanuni za utawala bora;

1. Kuengua viongozi wote wa NSSF na kusimika wanaomwabudu wengi toka PPF. Yaani mtu anatoka shirika dogo kioparesheni, kiufanisi, kifedha na kwa idadi ya wafanyakazi lakini viongozi wote wa juu anatoka nao huko!

Hili linashangaza na halina tafsiri nyingine zaidi ya kuwa na himaya ya siri ambayo imejengwa na ma royalists wake ili kuficha maovu yake.

TULISHANGAA ZAIDI Waziri kukaa kimya bila kukemea hili. Ili kutoa picha wakurugenzi WOTE wa makao makuu na mameneja karibu wote wa makao makuu amewaleta toka nje!

2. Mameneja wa Mikoa. Baada ya kuondoa uongozi wote makao makuu sasa amehamia mikoani, taratibu mameneja wote wanaostaafu anabadilisha mameneja wake toka nje!

Amefanya hivyo mkoa wa Songwe, Arusha na Mtwara, na bila shaka ataendelea pale ambapo kutakuwa na nafasi.

3. Kuunda makundi ya NSSF asili na team Elio. Hakuishia kubadilisha viongozi wetu tu bali ameleta hadi staff wa chini wengi toka PPF.

Na baada ya kuleta staff hao kazi zina pangwa kwa mgawanyo wa makundi ya hao staff.

Yaani unaweza ukakuta mko ofisi moja lakini kazi inatoka kwa Mkurugenzi mgeni, inaenda kwa meneja mgeni, msimamizi mgeni kisha wanaitwa staff wageni pembeni na kupewa kazi.

Nyie wengine mnashangaa mbona jamaa wamejitenga na wanafanya kazi tusioijua na tuko ofisi moja? Na hata ukijaribu kuchangamana nao unaona kabisa hawako tayari. Ni jambo la kushangaza lakini ndivyo hali ilivyo!

4. Kutishia kuhamisha wafanyakazi kwenda halmashauri. Hili amekuwa akitamba waziwazi kwamba anaweza akahamisha staff yeyote kwenda halmashauri.

Bahati mbaya sana kwenye hili alimtumia hata Naibu Katibu Mkuu Utumishi alipokuja kwenye mkutano wa wafanyakazi Morogoro.

Kiongozi huyu alitamka “mimi nikiletewa jina la staff ili niwahamishe, siwapeleki kwenye mashirika bali nawapeleka halmashauri tena za ndani”.

Tunajua kiongozi huyu alipotoka kwa kutumiwa vibaya hasa kutokana na ugeni wake kwenye utumishi wa umma.

Ikumbukwe Mkurugenzi siku zake za mwanzo pale alipokuwa anatengeneza nafasi za watu wake alihakikisha anahamisha mameneja wengi wa makao makuu kwenda halmashauri, na wako waliokata rufaa kwa Waziri wa utawala bora wakahamishiwa sehemu nyingine tena ambako angalau wamepewa nafasi zinazoshabiana na walizokuwa nazo.

Hakuishia kwa mameneja tu amekuwa akihamisha hata watumishi wa chini kiasi cha watu kujiuliza kaiweka mfukoni utumishi?

5. Utamaduni mbovu. Hali ya hapo juu imepelekea wafanyakazi wengi kuvunjika moyo, kujenga nidhamu ya uoga na kupoteza morali ya kufanya kazi.

Nashangaa sana watu hawa wamekuja na slogan ya “Cultural change” eti wafanyakazi waliokuwepo wabadilike lakini wao wameshindwa kabisa kuona mapungufu yao!

MATOKEO

Kutokana na hiyo hali kumekuwa na matokeo mabaya kwenye utendaji kazi wa Shirika kama ifuatavyo;

Mawasiliano mabovu SANA kati ya mikoa na makao makuu, na hata wafanyakazi na maboss wao hasa wa makao makuu.

Maboss wa makao makuu ni wachache sana wanaopokea simu za kikazi toka mikoani, hata kama zinapigwa na mameneja wetu wa mikoani, kinyume na sera na nia ya shirika iliyowezeshwa kununuliwa simu na kulipiwa ‘airtime’.

Barua za kiofisi zimekuwa zikiandikwa hazijibiwi na hata ukiandika reminder ni kazi bure, na ukilazimika kupiga simu hazipokelewi kama nilivyoeleza hapo juu.

Siku za nyuma ilikuwa ni kawaida kuomba miongozo au ufafanuzi wa masuala mbalimbali toka kwa technical staff wa idara mbalimali za makao makuu, lakini sasa hivi hata wao hawapokei simu kabisa.

Ukibahatika kukutana naye anakwambia mpigie meneja(ambaye naye hapokei simu). Unajiuliza staff wa makao makuu wana umuhimu gani kama wanashindwa kussuport field offices kwa masuala ya kikazi na mengine ni urgent?

Huduma mbovu kwa wateja wa nje. Kutokana na makao makuu kushindwa kushughulikia masuala mbalimbali ikiwemo wateja kwa kujiweka mbali, mikoa inajikuta nayo inashindwa kuhudumia wateja kwa kusubiri majibu ya makao makuu.

Mikoa inalazimika kuwapa tarehe wateja huku ikiendelea kubembeleza kujibiwa na makao makuu. Hali imekuwa ni mbaya sana hasa idara ya mafao.

Nitatoa mfano. Kwa miaka ya nyuma kati ya huduma ambazo Shirika limekuwa likitoa kwa ufanisi na wakati ni malipo ya pensheni ya uzee ambayo yalikuwa yakilipwa bila kukosa tarehe 24 ya kila mwezi.

Baada ya uongozi mpya kuja ukaja na zoezi la uhakiki walipwa pensheni na kulipa kupita benki. Zoezi ambalo kimantiki ni zuri lakini wameonyesha MAPUNGUFU MAKUBWA SANA ya kiutendaji katika zoezi hili.

Makao makuu wameshindwa kukamilisha zoezi pamoja na kutumiwa nyaraka husika kikamilifu tena zaidi ya mara moja.

Inasikitisha kuna wazee sana na wengine wagonjwa ambao sasa ni mwaka au zaidi ya mwaka hawajapata pensheni sababu tu ya uzembe wa kitengo cha mafao makao makuu.

Mfano ni mikoa ya kanda ya ziwa. Ambao tuko kwenye shirika kwa muda mrefu tunajua isingewezekana hata chembe mzee wa pensheni kusimamishiwa pensheni kwa hata miezi 2 kwa uzembe wa staff, moto ungewaka kwa aina ya viongozi tuliokuwa nao na mitazamo yao juu ya ulipwaji wa pensheni ya kila mwezi.

Kukosekana kwa weledi kwa viongozi wa makao makuu(Incompetence). Mikoa imekuwa ikilazimika kuandika barua za kuomba miongozo juu ya masuala mbalimbali ambayo yanaonekana kushindwa kutatuliwa/kushughulikiwa vizuri na sheria, miongozo na taratibu zilizopo.

Hili ni jambo la kawaida kwa shirika kubwa na lenye aina ya shughuli(operations) kama zinazofanywa na NSSF.

Aidha kutofautina sana kwa mazingira toka sehemu moja kwenda nyingine, utamaduni na msimamo na msukumo wa jamii ya sehemu moja kwenda nyingine, barua zimekuwa zikiandikwa makao makuu kuomba miongozo au kibali cha kushughulikia jambo mahsusi.

Lakini viongozi wa makao makuu wameonyesha; aidha, kukwepa kwa makusudi kubeba responsibilities ya kutoa maamuzi, au kushindwa kuelewa uhitaji wa jambo husika na hivyo wanatoa majibu yenye tofauti au kukwepa maudhui ya walichoandikiwa.

Huduma mbovu si kwa wateja wa nje tu bali hata kwa wafanyakazi. Imekuwa ni jambo la kawaida mfanyakazi kusafiri kikazi bila kulipwa masurufu ya safari kwa wakati, mfanyakazi anaweza akalipwa hata baada ya siku kumi au zaidi toka kumaliza safari ya kikazi.

Fikiria mwajiri anakutaka usafiri hajakulipa, unalazimika kuhangaika kukopa ili utimize matakwa ya mwajiri.

Idara za makao makuu kushindwa kuhudumia field offices. Hili ni tatizo kubwa kwa idara nyingi.

Tumeshindwa kuelewa, je ni makusudi ili field offices zikwame kufanya kazi au mkurugenzi mkuu hajui? Nitatoa mifano kuna ofisi moja ya Dar es salaam iliishiwa majalada ya kufungulia madai.

Kwa zaidi ya mwezi moja makao makuu walishindwa kuwezeshaa kupatikana kwa majalada husika! Ukizingatia ukubwa wa ofisi hiyo na uwingi wa wanachama wanaofungua madai, maana yake zilikuwa zinapokelewa nyaraka halafu hamna namna ya kuzihifadhi!

Sasa kitu kidogo kama hiki lakini chenye unyeti wa hali ya juu makao makuu wanashindwa kuhudumia, wapo kwa ajili ya nini? Idara ya utawala na utumishi nayo imeshindwa kabisa kuwajibika.

Eti mkurugenzi anatoa waraka mikoani barua zote zielekezwe kwa mameneja wa kurugenzi yake, nao wanatoa waraka barua zote za mikoani zielekezwe kwa staff Fulani Fulani wa makao makuu.

Hizo barua(kumbuka ni nyeti na za shirika zima) zikitumwa kwa hao staff hupati mrejesho. Hapa hali ni mbaya saana. Unaweza ukaandika barua hata mara tatu, baadaye ukiwasiliana na meneja naye anakujibu ni staff Fulani ndiyo anahusika, mnabaki mnaangaika na simu hazipokelewi.

Tunatamani mkurugenzi huyu angejifunza kwa wakurugenzi waliopita kama Mniwako ambaye lolote lililokuwa linaendelea ndani ya shirika alikuwa analijua na mbinu mojawapo ni kutozikimbia barua za kikazi.

Sasa hivi ni kitu cha kawaida kwa gari la shirika kupaki kwa mwezi mzima eti matairi yameisha, fedha zipo ila ‘wafalme” wa makao makuu wako busy na mambo mengine. Ni aibu na kurudisha nyuma taifa.

Sasa hivi ni jambo la kawaida japo ni aibu ofisi za NSSF, kukatiwa maji, kukosa/kukatiwa umeme.

Tembelea ofisi za NSSF hali ni mbaya wanashindwa hata kufanya matengenezo ya vitu vidogo kama vitasa, fedha zipo ila “wafalme” wamejifungia makao makuu na kutengeneza gap kwa kutotoa, miongozo inayoeleweka(mara nyingi wanatoa miongozo inayokinzana) au kutofikika na kutojibu maombi mbalimbali kupitia barua.

MAPENDEKEZO

- Tunapendekeza Mh Rais au hata Waziri akiamua kwa dhati kushughulikia hili kuunda timu ya watu wa nje kuja kuchunguza hili kuthibitisha tuhuma hizi.

- Pamoja na mbinu watakazotumia wanaweza pia;

1) Kupita mikoani kuthibitisha kama kuna utitiri wa barua zilizoandikwa makao makuu na hazijibiwi. Mtashangaa ushahidi mtakao pata.

2) Kucheki kama kweli kuna ofisi zilizokosa/kukatiwa umeme, maji, magari kupaki sababu eti ya matatizo madogo yanayo hitaji attendance ya makao makuu

3) Angalia hali ya ofisi za NSSF (physical appearance) na kujiridhisha zinatunzwa ipasavyo?

4) Angalia muundo wa uongozi na wafanyakazi kwa ujumla na kina nani wanaopewa vyeo au majukumu ya kikazi na wametokea wapi?


Ni mzoefu na mpika data kama aliweza kudanganya kuhusu idadi ya wanachama tu unategemea nini kwenye masuala nyeti zaidi kama ya fedha?

Sasa baba lao ni alipoingia na kukuta lengo ni kukusanya 1tr akashusha hadi 760m ili likifikiwa asifiwe kua ameweza kukusanya kuliko watangulizi wake.
Mtakoma wenyewe.
 
Wawatume kukagua nini wkt pesa wameichukua wao wenyewe?
Kwa sasa huduma za NSSF ni za hovyo na lawama wanatupiwa serikali kuwa wamechukua fedha za NSSF.

Kwahiyo hapo serikali itume kikosi kazi kufanya uchunguzi na ikibainika kuna uzembe wahusika wachukuliwe hatu.

Sio sawa mtu kukosa huduma eti kwa hoja za kukosa majalada.

Wapo watumishi kwa sasa wanateseka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si mstaafu mmojawapo ni ndg yake,acha ajilipe tu.
Nakumbuka hata chief accountant wa ppf aliondolewa kimizengwe baada ya kutokukubaliana na ubadirifu uliokuwa unafanywa na Erio na wenzake hasa ktk kujilipa zaidi ya 200m kila baada ya miaka miwili.
Sasa nasikia amekuja na mbinu hyo kivingine, eti kujilipa 40% ya mshahara wa mwaka kila baada ya miaka mitatu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwandishi umeeleza vyema. Kusema kweli kumekuwa kukipita nyuzi nyingi sana za malalamiko hasa ya wanachama juu ya malipo ya Pension zao. Wameeleza mara nyingi hapa kuwa wanazungushwa sana na kutopewa mirejesho na wamekuwa wakitaja baadhi ya staff kuwajibu nyodo sana na kutaja baaadhi ya ofisi.
Nadhani wahuhusika wameona na naamini watafuatilia kwa kina. Hata hivyo umeeleza kwa kina na kutoa data muhimu.
Lakini waTZ pia ni vichwa ngumu sana kwa kasi ya Mh.raisi anavyokemea mambo haya kila siku lakini watu wameota mapembe yaliyokomaa na hawaogopi wala kuwa na hofu.
Mtu unalipwa mshahara mzuri na beneficiaries kibao kwa kodi za wananchi unashindwaje kufanya kazi na kusaidia WaTZ wanyonge?.
Inasikitisha sn. Kushindwa kulipa wanachama wenu ni wizi na utapeli.
 
alieharibu nssf ni yule aliekuwa anajenga misikiti kila palipo na jengo la shirika. nssf siyo nyumba ya ibada, ni shirika la umma. vijana wa kiislamu mlioajiriwa ndani ya shirika fanyeni kazi acheni hizi risala ndefu mnazoandikiwa na maimamu.

Naona Watu wameanza kujificha kwenye Kichaka cha Udini kujinusuru

Mtoa Mada kashauri Rais atume timu ya watu waadilifu wachunguze then wampe taarifa

Kama kuna hiyo Misikiti pemben ya Majengo ya Nssf pia utasaidia kuiambia hiyo Task force
 
Tunavyomfahamu utendaji wa Mhe.Rais anahitaji kuunda tume? kwani mnadhani hajui kilichokuwa kinaendelea ndani ya NSSF na nini kimefanyika? Acheni majungu . Wacheni watu wapige kazi.

Naona Watu wameanza kujificha kwenye Kichaka cha Udini kujinusuru

Mtoa Mada kashauri Rais atume timu ya watu waadilifu wachunguze then wampe taarifa

Kama kuna hiyo Misikiti pemben ya Majengo ya Nssf pia utasaidia kuiambia hiyo Task force

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunavyomfahamu utendaji wa Mhe.Rais anahitaji kuunda tume? kwani mnadhani hajui kilichokuwa kinaendelea ndani ya NSSF na nini kimefanyika? Acheni majungu . Wacheni watu wapige kazi.



Sent using Jamii Forums mobile app

Mleta uzi kashauri NSSF ichunguzwewna wewe umeshauri isichunguzwe, yote hayo ni maoni na ndio msingi wa Jf kila mmoja kuwa huru kuwaza apendavyo
 
Sasa amekuja anaejenga kanisa mbona ndio kafeli kabisa bora aliyekuwa anajenga msikiti kuliko mjenga kanisa
alieharibu nssf ni yule aliekuwa anajenga misikiti kila palipo na jengo la shirika. nssf siyo nyumba ya ibada, ni shirika la umma. vijana wa kiislamu mlioajiriwa ndani ya shirika fanyeni kazi acheni hizi risala ndefu mnazoandikiwa na maimamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eee bana see hili Taifa letu si la udini wala ukabila nyie ndio mnaokosa uzalendo na Taifa lenu yaaani badala ya kujadili mada zenye kuleta tija wewe unabwabwaja tuuu...eti kanisa ...eti misikiti kweli nimeamini tuna vilaza weeeengi sana

Tusipotezeane muda aisee
Wakristo. Mmmmmmmmmmmhh hata ndalichako kavuruga wazara ya elimu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati kuna Kiongozi mmoja wa nchi alishauri Watanzania tupende kusoma ili tuwe na uwezo wa kupambanua issues mbalimbali ninachoona hapa watu mna chuki zenu binafsi na kusahau NSSF ni Taasisi na ofisi ya mtu kapuni hebu basi tujifunze kidogo Taasisi inaendeshwaje halafu tuje kuleta Uzi wenye mashiko dah yaaani mnaboa saaana@Big youu,

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mi nauliza hivi katika uelewa wangu kama mshikaji hapo juu alivyosema nani asiyejua umahiri wa Erio Katika Hifadhi ya Jamii mwenyewe huyu jamaa Nina mind kwa kuwa Kabana njia zote za kupata pesa kwa njia za chini ya kapeti kama tulivyokuwa tunaenda pale NSSF zamani lakini ndio katunyooosha wooote tuliokuwa tunapenda maisha ya Mafanikio ya fasta fasta yasiyo halali oooh ngoja niiishie zangu maana naona ishakuwa ndivyo sivyo.. kuchele kuchele
Mleta uzi kashauri NSSF ichunguzwewna wewe umeshauri isichunguzwe, yote hayo ni maoni na ndio msingi wa Jf kila mmoja kuwa huru kuwaza apendavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom