Kifo cha Makweta,kimenifikirisha na hakika nimekumbuka kuwa yeye ndiye mtu maarufu kuliko wanasiasa wengi waliopata kutawala katika mkoa wa Iringa na Njombe ikiwamo.Ni huyu Makweta ambaye aliwahi kuwa mbunge wa wilaya zote za mkoa wa Njombe wa sasa pia ni mtu wa pekee toka maeneo yetu aliyeshika uwaziri katika wizara nyingi.Kwa muda mrefu alikuwa mbunge wa eneo lote la Ludewa,Makete,Wanging'ombe na Njombe yote ambayo sasa imezalisha majimbo ya uchaguzi matatu.
Katika historia ya mkoa wa Iringa na Njombe Makweta atabaki kuwa mtu maarufu namba mbili baada ya Chifu Mkwawa aliyekuwa chifu wa wahehe miaka ya 1880s.
Makweta lazima aheshimiwe kwa jitihada zake za kuendeleza maeneo yote ya ukanda wa kusini kwa kuhamasisha upandaji wa miti ya mbao na kuni,ujenzi wa sekondari na mapambano makubwa aliyoongoza dhidi ya ugonjwa wa funza uliowatesa sana watoto wa Njombe hasa maeneo ya Lupembe na Mkambako.
Kwa wale wote wanaozaliwa au kuishi katika maeneo tajwa hapo juu yafaa tushiriki kwa ukaribu katika shughuli za kumsindikiza katika maisha ya amani ya milele.Makweta amekufa mwili lakini mawazo na falsafa zake zitaishi milele.Makweta ulitutoa porini ukatuleta barabarani.We shall always remember you and love you forever.R.I.P JACKY.