Makutano ya kiroho

Makutano ya kiroho

mkuu, tunasubiri hoja zako na wewe utuambie kuhusu hizi imani zilizozuka tz za kuegemea kwenye masula ya kiroho ili kutatua baadhi udhalili unaofanywa na wasiojulikana , je kwenye ndoto unawezaje kukutana nao.
Tungekuwa na watu makini na wasafi hawa wa kiroho wangeweza kutatua changamoto nyingi sana na kutengua vitendawili vigumu... Lakini bahati mbaya sana nao wamejawa na uchafu husuda na mambo mabaya
 
Si kwa muktadha wa kimapenzi ama hisia za kufikirika, zile tamanifu zenye kuleta mvuto wa hisia za mahusiano ya kingono... Zile za kusema you stole my heart - umeiba moyo wangu....!
Haya ni makutano ya kiroho uwapo nje ya ufahamu wako, uwapo usingizini
Kipindi hiki roho husafiri huko na kule na katika safari hizo, roho hukutana na roho nyingine nyingi tu.... Roho mbaya nzuri nknk, za majini za wachawi za watu wa kawaida nk nk
Unapokuwa na ndoto mbaya sana na za kutisha basi roho yako inakuwa imekutana na roho za kutisha ama roho mbaya
Unapokuwa na ndoto nzuri basi huko kwenye kuvinjari jua roho yako imekutana na roho nzuri....
Utambuzi na kumbukumbu ya makutano ya roho katika ufahamu hutegemea na asilimia mia ufahamu wako umeweza kukamata yani kuna kuanzia asilia 0 mpaka 100, kadiri asilimia zinavyopungua ndio kumbukumbu ya ndoto husika huwa finyu na kuwa kama vague memories na vile jinsi asilimia zinavyozidi basi ufahamu na kumbukumbu ya ndoto husika huwa dhahiri zaidi na kuleta uhalisia zaidi
Ndoto za namna hii, hizi zenye kuleta uhalisia zaidi huwa karibu sawa kabisa na ndoto maono, zile ambazo huweza kusimulia kwa usahihi kabisa mwanzo wake mpaka mwisho wake... Tofauti yake ni moja tu! Ndoto maono hizi huwa na tabia ya kujirudiarudia wakati hizo nyingine hazijirudiii japo huwa clear sana
Ulimwengu wa ndoto kwa asilimia kubwa sana huhusika na roho moja kwa moja, hivyo tunaposema kuna makutano ya kiroho jua kwamba si kingine bali ni kupitia ndotoni, japo kwa meditation pia inawezekana


Jr
Asanteeeee
 
Naona mada imekuwa ngumu kueleweka na wengi
 
Moderator, JamiiForums naomba msaada wa kuunganishwa hii mada imejirudia mara tatu
Screenshot_20180722-053536.jpg
 
Naomba tena kwa mara ya tatu hii mada imejirudia mara tatu tafadhali iunganisheni... Ningeweza mwenyewe nisingependa kuwasumbua
Screenshot_20180722-053536.jpg
 
Back
Top Bottom