Makutano Show: Exclusive Interview na Prof Ibrahim Lipumba

Makutano Show: Exclusive Interview na Prof Ibrahim Lipumba

Makutano Show

Member
Joined
Aug 3, 2012
Posts
21
Reaction score
65
Wana-JF

Jumamosi hii katika kipindi cha Makutano kuanzia saa tisa mchana nitakuwa na Profesa Ibrahim Lipumba. Nitazungumza nae kuhusu mambo yanayogusa medani ya kisiasa, na pia mtazamo wake kuhusu hali ya nchi kwa sasa. Kama ilivyokuwa kwa vipindi vingine napenda kupata maswali toka hapa jamvini ambayo atayajibu moja kwa moja. Kipindi kinakuwa hewani kupitia Magic FM, 92.9 Dar, 93.3FM Dodoma, 98.6FM Arusha/Moshi, 101.7FM na pia online: MakutanoShow on USTREAM: Makutano na Fina Mango. Radio

Karibu.
 
Muulize masuali yafuatayo:

1. Je bado ana nia ya kugombea urais 2015? kama jibu ni ndiyo, haoni kuwa ni muhimu sasa akmuachia mwana CUF mwingine akasimama?

2. Muulize kuhusu ndoa waliyoifunga na CCM huko Zenji

3. Muulize kwa nini wasiungane na CDM kuleta upinzani wa maana utakao iondoa CCM madarakani?

4. Nini maoni yake kuhusu chama kipya cha ADC.
 
1. Kwa nini yeye na chama chake wanatumia nguvu nyingi sana kuisema vibaya chadema na kupambana nayo badala ya kupambana na ccm kwani chadema si chama tawala. Hata kwenye chaguzi hasa za madiwani (mfano kule mwanza) cuf iliiunga mkono ccm na kuipinga chadema.

2. Je kweli cuf ni chama cha upinzani? majibu kuhusu ndoa yao na ccm bado hatujaridhika nayo.

3. Vipi kuhusu yeye lipumba pampja na chama chake kuonesha waziwazi kuegemea upande wa waislamu na hivyo kuleta hisia kuwa ni chama cha waislamu?

4. Kwa kuwa cuf sasa imepoteza mvuto, kwa nini wasiwaambie wananchi kura za cuf ziende chadema kama ambavyo dovutwa alivyosema kura zake apewe kikwete 2010?
 
Muulize nini mikakati ya cuf kujijenga na kujiimarisha hasa bara ili kuchukua dola mwaka 2015?.
 
Lengo lake ni nini kumwekea dhamana Shekhe Ponda?
 
Muulize chama chao hakina watu wengine competent wa kugombea Urais? Mbona kila siku ni wale wale tu? Hawaoni kwamba wao hawakubaliki ndo maana hawashindi. Wajaribu kuwasimamisha watu wengine waone.
 
1. Kwa nini yeye na chama chake wanatumia nguvu nyingi sana kuisema vibaya chadema na kupambana nayo badala ya kupambana na ccm kwani chadema si chama tawala. Hata kwenye chaguzi hasa za madiwani (mfano kule mwanza) cuf iliiunga mkono ccm na kuipinga chadema.

2. Je kweli cuf ni chama cha upinzani? majibu kuhusu ndoa yao na ccm bado hatujaridhika nayo.

3. Vipi kuhusu yeye lipumba pampja na chama chake kuonesha waziwazi kuegemea upande wa waislamu na hivyo kuleta hisia kuwa ni chama cha waislamu?

4. Kwa kuwa cuf sasa imepoteza mvuto, kwa nini wasiwaambie wananchi kura za cuf ziende chadema kama ambavyo dovutwa alivyosema kura zake apewe kikwete 2010?

Nafikiri swali la kwanza unalo jibu wewe mwenyewe iwapo utajibu ni kwanini wewe kama mvaa magwanda unatumia nguvu nyingi kuisema CUF?

Swali la pili jibu lake ni rahisi sana. Kama kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ndiyo unaita ndoa ya vyama, vipi pale magwanda walipokuwa wanaunda upinzani rasmi bungeni pamoja na CUF mlikuwa mmeolewa? Na huu upuuzi ulipata kuletwa mara ya kwanza kwenye mdahalo wa Hamad Rashid na Mbowe. Kilichotokea kwenye mdahalo nafikiri magwanda mnafahamu sana kwani mliishia kuchakachua video ya mdahalo mpaka Hamad Rashid akasema ile nukuu maarufu "wanaolia kuchakachuliwa ndiyo waalimu wa kuchakachua"

Swali la tatu kama ukiweza kuelewa vipi Chadema inaonyesha waziwazi kugemea upande wa Wakristo na kuleta hisia ni chama cha Wakristo, basi utakuwa umejijibu.

Swali la nne ni swali la kimtazamo. Sawa na mtu akuambie wewe kuwa kwa sababu ushaanza kupoteza mvuto kwanini usimuambie mkeo asianze mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.
 
Fina naomba umuulize maswali yafuatayo!

1.Anazungumziaje uchumi wa nchi na matatizo yaliyopo hasa mfumuko wa bei?

2.Anazungumziaje elimu aliyo nayo kama mchumi ,je serikali ina mtumia kutatua matatizo yaliyopo hasa ya kiuchumi? Na nini mchango wake kwa taifa?

3. Kama angekuwa yeye Lipumba ame vaa viatu vya jk ange fanya nini kuhusu hizi safari za kila leo?

4.Nini mchango wa chama cha wananchi cuf katika kuleta na kushawishi maendeleo kwa taifa letu?

5.je kipindi gani alishawai kujuta kuwa mwana siasa? Na nini kilitokea?

6. Matatizo yanayo tokea hapa nchini hasa ya chuki za kidini, yeye lipumba ana shauri nini, na angekuwa ame vaa viatu vya jk ange fanya nini kumaliza tatizo?
 
Muulize Prof kwa nini wafuasi wa chama chake akina Sheikh Ponda na Sheikh Faridi wanaendekeza fujo na imani kali za kidini halafu chama hakiwakemei?

Kwa nini alimua kubakia CUF wakati ADC inameguka wakati yeye hana sauti ndani ya CUF mbele ya Maalim Seif?
 
Muulize very very solid, kuna agenda gani kati ya Cuf na uislam? mtaani leo wanasema kauli ya Lipumba ya jana kusitisha maandamano wameitii, na ukiangalia mikutano yake pale jangwani utafikiri kuna mawaidha ni balaghashia na baibui.

CUF si chama cha kidini kwa mujibu wa katiba yake na sheria za usajili wa vyama bila ya kusahau katiba mama inayopiga marufuku vyama vya kisiasa vyenye katiba ya dini!
Lakini hoja ya kudai CUF inauhusiano gani na Waislamu? Katiba yetu TZ haikatazi chama cha kisiasa kuwa na mahusiano mazuri na Waislamu, wakristo au wapagani ila ikiwa chama cha kisiasa kitakuwa na mahusiano mabaya na dini hizo kama kilivyo CHADEMA na Waislamu basi hapo ni dosari kubwa kwa amani ya nchi yetu!

Marekani ambae ni Mwalimu wetu wa Demokrasia kuna mahusiano makubwa kati ya vyama vya Republican na Demokrat na Mayahudi! Mayahudi huingia hata na mkataba na chama cha kisiasa ili kukidhi mahitaji yao! sasas kwanini TZ iwe haramu?

Waislamu wanamahusiano mema na CUF kwa sababu angalau ni chama pekee cha kisiasa kinachokubali kutetea madai ya Waislamu ambao ni sehemu kubwa ya jamii ya wa tz! CUF kikotayari kupokea madai ya Waislamu kuhusu ubaguzi wa Elimu, Umaskini, Ukosefu wa ajira, mahakama ya kadhi, OIC nk!

Jee, Chadema wako tayari kupokea malalamiko ya WAISLAMU NA KUYAFANYIA KAZI? KAMA jibu ni ndio basi bila shaka uhusiano wao na Waislamu utakuwa mzuri! kinyume chake usitegemee Waislamu kuipa kura Chadema ambao wanatuhuma za kuibeba Dini ya Kikristo pekee!

HAKI SAWA KWA WOTE ndio sera za CUF!!! tunataka kujua sera za CHADEMA ni zipi?
 
Naitaja ufafanuzi kati ya shekhe Ponda,uislam,Pr.Lipumbu na cuf uhusiano wao ukoje.?
 
Muulize chanzo cha kuporomoka umaarufu wa CUF. Kwa nini viongozi walioiweka chama juu waliondolewa na yeye mwenyewe au kujiondoa wenxewe
 
Dada Fina;

Maswali;

1. Kwa nini chama cha CUF hakijawahi kubadili mwenyekiti wake. Hakuna kikomo cha kukaa kiti hicho? Na je , yeye haoni kama chama chake kimekosa demokrasia.

2. Ni wazi kumetokea utofauti mkubwa katika kuendesha serikali ya umoja wa kitaifa; haoni kwamba muungano wao na ccm ni kitu ambacho kimeshindikana?

3. Anasemaje kuhusu muungano na chama kikuu cha upinzani CDM. Je yupo tayari?
 
Makutano Show,

..muulize kuhusu suala la MUUNGANO wa Tanganyika na ZNZ.

..je, bado CUF inasimama ktk hoja yake ya serikali 3, au inaunga mkono hoja ya Maalim Seif kuwa na muungano wa mkataba?

..kama anaunga mkono serikali 3 unatakiwa umuulize kwanini? kwanini anaona serikali 3 ni bora kuliko serikali 2, au "muungano wa mkataba"??

..kama anaunga mkono muungano wa mkataba, unapaswa kumuuliza faida za muungano huo, haswa kwa wa-Tanganyika. pia umuulize kwanini mahusiano yetu yasiwe kupitia EAC, au SADC, au kuna ulazima gani wa kuwa na mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar??

..kuhusu muungano pia, unaweza kumuuliza kuhusu faida zake kwa WATANGANYIKA. kuna baadhi yetu ambao tunaamini muungano huu UNATUNYONYA wananchi wa-Tanganyika. Ushahidi wa madai hayo upo ktk tafiti mbalimbali kama ule uliofanywa na PROF.TEDDY MALYAMKONO. sasa tunaomba kujua ni nini mtizamo wa Prof na chama cha CUF kuhusu madai ya wa-Tanganyika kwamba muungano umekuwa-burden kwao??

..kuna suala la madai ya Radio Imaan kwamba hapa Tanzania kuna MFUMO KRISTO. Je, msimamo wa CUF na Prof kuhusu madai ya kuwepo MFUMO KRISTO.

..kuna suala la Shekhe Ponda. Huyu bwana alishatokea kule ZNZ ktk mikutano ya Uamsho. Pamoja na mambo mengine, mikutano hiyo inasifika kwa kutoa matamshi ya kashfa dhidi ya wa-Tanganyika, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, na muungano kwa ujumla. Sasa nini msimamo wa CUF na Prof kuhusu kashfa hizo??

..mwisho, maadamu Prof ametoa offer ya kumdhamini Shekhe Ponda, je yuko tayari kutoa mkono wa pole kwa kukarabati walau kanisa moja liliotiwa kiberiti, au kufidia mali zilizoibiwa??

NB:

..waandishi wengi wa habari huwa mnashindwa kuuliza maswali magumu, and follow up questions.

..pia ktk kila interview uhakikishe kwamba wananchi wanapata kitu kipya kutokana na interview hiyo?
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri swali la kwanza unalo jibu wewe mwenyewe iwapo utajibu ni kwanini wewe kama mvaa magwanda unatumia nguvu nyingi kuisema CUF?

Swali la pili jibu lake ni rahisi sana. Kama kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ndiyo unaita ndoa ya vyama, vipi pale magwanda walipokuwa wanaunda upinzani rasmi bungeni pamoja na CUF mlikuwa mmeolewa? Na huu upuuzi ulipata kuletwa mara ya kwanza kwenye mdahalo wa Hamad Rashid na Mbowe. Kilichotokea kwenye mdahalo nafikiri magwanda mnafahamu sana kwani mliishia kuchakachua video ya mdahalo mpaka Hamad Rashid akasema ile nukuu maarufu "wanaolia kuchakachuliwa ndiyo waalimu wa kuchakachua"

Swali la tatu kama ukiweza kuelewa vipi Chadema inaonyesha waziwazi kugemea upande wa Wakristo na kuleta hisia ni chama cha Wakristo, basi utakuwa umejijibu.

Swali la nne ni swali la kimtazamo. Sawa na mtu akuambie wewe kuwa kwa sababu ushaanza kupoteza mvuto kwanini usimuambie mkeo asianze mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.

Umesahau moja: Ndoa iliyofungwa kati ya CHADEMA na Christian Democratic party (CDU) cha Ujerumani kinachoongozwa na Bi Angela Markel. aKIWEZA KUJIBU HILO atapata majibu yote ya maswali yake.
 
Muulize kwanini yeye hana mke lakini Chama chake cha CUF kina mume?
 
Sina la kuuliza ila nitasikiliza Makutano Show

ohhhh! nimekumbuka
Muulize prof hivi:

Kwanini kule Arusha walivyo kwenda kuzindua movement yao Walisomba watu ns mabasi kutoka Dar es Salaam?...Jee cuf haina wafuasi Arusha?
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri swali la kwanza unalo jibu wewe mwenyewe iwapo utajibu ni kwanini wewe kama mvaa magwanda unatumia nguvu nyingi kuisema CUF?

Swali la pili jibu lake ni rahisi sana. Kama kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ndiyo unaita ndoa ya vyama, vipi pale magwanda walipokuwa wanaunda upinzani rasmi bungeni pamoja na CUF mlikuwa mmeolewa? Na huu upuuzi ulipata kuletwa mara ya kwanza kwenye mdahalo wa Hamad Rashid na Mbowe. Kilichotokea kwenye mdahalo nafikiri magwanda mnafahamu sana kwani mliishia kuchakachua video ya mdahalo mpaka Hamad Rashid akasema ile nukuu maarufu "wanaolia kuchakachuliwa ndiyo waalimu wa kuchakachua"

Swali la tatu kama ukiweza kuelewa vipi Chadema inaonyesha waziwazi kugemea upande wa Wakristo na kuleta hisia ni chama cha Wakristo, basi utakuwa umejijibu.

Swali la nne ni swali la kimtazamo. Sawa na mtu akuambie wewe kuwa kwa sababu ushaanza kupoteza mvuto kwanini usimuambie mkeo asianze mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.

KUDADEKI@

Ebwana unatisha kwa kujibu hoja, yule jamaa umemjibu kwa asilimia mia moja. hapa hahitajiki tena prof lipumba kujibu. waambie hao jamaa naona wameshaanza kuogopa lipumba kumwekea dhamana sheikh ponda, waambie uchaguzi ujao upinzani mkali utakuwepo kati ya CUF NA CDM. Watu wengi hawajui kuwa CUF uchaguzi ujao utakuwa na sapoti kubwa. ni suala la muda tu kuthibitisha maneno yangu.
 
Sawli,
1. Je ngome kuu za CUF inazo weza jivunia zipo sehemu gani ya Tanzania bara na visiwai?( mikoa au Kanda)
2. Je kwa nini CUF wasichague maeneo ambayo wananguvu wakatumia resources zao katika kanda hizo na kupata viti vya uwakilishi na kura za kutosha kuliko kutaka kusambaa nchi nzima ingali hawana resources za kutosha?
3. Kwanini Vyama vya Upinzani ikiwemo CUF hawaongelei tatizo sugu, la Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama, na hata Muundo wa Bunge la katiba?
4. Kwanini Vyama vya Upinzani havijakutana/kutoa tamko juu ya Vipaumbele vya kitaifa? hii ni tofauti na malengo ya chama, hapa nina maana National ethics, codes, strategies and resource management of a country.
4. Edapo katiba mpya haitakuwa tayari 2014, CUF ipo tayari kwenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kwa katiba ya zamani?, je kama katiba haitakuwa tayari 2015 CUF itashiriki uchaguzi mkuu 2015?
5. Endapo katiba mpya itaamua vinginevyo juu ya muungano, ila siyo serikali tatu, je CUF watabadili katiba yao, au wataendelea na lengo lao la serikali tatu?

Wakatabahu!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom