Makusanyo Januari kufikia Sh tril 1.5

Makusanyo Januari kufikia Sh tril 1.5

mbona sioni mkizungumzia reli ambayo ndo nyenzo mhimu ya usafirishaji....hizo bidhaa zitawafikiaje wananchi kutoka viwandani bila kutumia reli
Tulia hilo litatekelezwa
Nivizuri kuonesha Upo kizalendo zaidi
 
Go go Magufuli!
Negativists hawatakosekana, lakini hawawezi kuturudisha nyuma! HAPA KAZI TU!!
 
  • Thanks
Reactions: nao
Kwenye makaratasi ni kweli ila kwenye uhalisia si kweli.....
Maana hatuoni la muhimu lolote bado wanafunzi wanakaa chini
Mnapo kosoa muwe MNA sababu
Sio kila jambo ni sababu katika muda Fulani
Raise ndio kwanza ana miezi 3
Pesa ndizo hizo zinapelekwa kwenye maendeleo
Sasa unaanza kuunda unda chuki
 
Huyu Ndulu naye ni jipu tu, anatuzingua.. Miaka kibao yupo BOT ila serikali kiuchumi ilikuwa chalia,
Kiuchumi kama nchi tunajitahidi, tatizo kubwa ni wanufaika wa ukuaji wa kiuchumi.
Kama wataendelea hivi kutenga hela ya kutosha kwa miradi ya maendeleo miaka 3 mingi wananchi watanufaika moja kwa moja.

Tukitoa ushabiki nchi nyingi zinayumba kiuchumi kwa sasa, suala la Zanzibar likimalizwa vizuri itatusaidia sana.
 
Kwenye sekta ya elimu serikali iangalie kwa jicho la tatu, pesa inayopelekwa ni kidogo ukilinganisha na mahitaji ya shule husika, mfano shule inapelekewa sh 140,000 kama admistation cost maanake hapo wanunue vifaa vya kufundishia, walipe walinzi nk Ambapo pes hiyo haitoshi kabisa. Je hapo unategemea elimu kuwa bora au bora elimu?
Kingine mpango huu wa elimu bure haukuwa umeandaliwa mapema kutoka kwenye bunge la bajeti 2015/2016 hivyo shule zilikuwa na wazabuni wa huduma mbali mbali waliotoa huduma kwa shule hizo, mfano shule nyingi zina madeni kwa wazabuni mfano madeni ya kudurufu mitiani nk ambapo shule husika ilitegemea january makusanyo yakishakuwa mazuri kutoka kwa wanafunzi ilipe madeni, lakini sasa zinashindwa fanya hivyo kutokana na pesa inayopelekwa kuwa kidogo sana na vile vile kutokuwa na kifungu hicho. Hvyo serikali iangalie kwa jicho la pili juu ya madeni hayo make vinginevyo itasababisha mgogoro mkubwa baina ya shule na wazabuni
Umeongea vyema mkuu
Lakini hebu tujiulize
Pesa hizo za serikali zitapelekwa kila mwezi
Tukiacha ule wizi wa wakuu wa shule naamini zitatimia
 
Hiyo ndo serikali sasa. Haya mambo ni kama mageni machon petu. Watu hawaamini kinachoendelea. Hii serikali ipe miaka miwili tu kama hakutatokea dhoruba yoyote uone nchi itakavyopiga hatua. Tutakuwa mbali sana. Uchumi wetu utakuwa mkubwa sana. Tutapaa kama airforce one. Tutakuwa hatuna haja ya misaada yao. Wakae nayo tu. Hatumpigii mtu magoti tena. Hata hao milenium challenge funds wabaki tu na hizo hela zao. Nchi hii ni tajiri sana
Kabisa mkuu
Nchi hii ina neema tele
Nikuamua tu
 
Hiyo ndo serikali sasa. Haya mambo ni kama mageni machon petu. Watu hawaamini kinachoendelea. Hii serikali ipe miaka miwili tu kama hakutatokea dhoruba yoyote uone nchi itakavyopiga hatua. Tutakuwa mbali sana. Uchumi wetu utakuwa mkubwa sana. Tutapaa kama airforce one. Tutakuwa hatuna haja ya misaada yao. Wakae nayo tu. Hatumpigii mtu magoti tena. Hata hao milenium challenge funds wabaki tu na hizo hela zao. Nchi hii ni tajiri sana
Balozi wa Uingereza allwahi kunukuliwa akisema bajeti ya Tanzania ni sawa na kiasi wenyeji wa London wanachotumia kununulia CD za muziki.
Hâta tukikusanya tr2 kwa mwezi hazitoshi kuwaendeleza wananchi wote,na kuwafanya waache kula viwavi na kulala kwenye tembe kama mifugo.
NB:Kenya wako wachache kuliko sisi,makusanyo yao ni zaidi ya mara mbili kuliko sisi lakini bado wanapokea misaada kiasi fulani
Mwisho jiulize déni la taifa trillioni 40 kwa mwendo huu litalipwa lini
 
Kila kizuri kinachofanyika na serikali watu mnalaumu kikifanyika kibaya ndio kabisaaaa lawama juu ya lawama sasa nyinyi kwa maoni yenu mnataka serikali ifanye nini ndio mfurahi?
 
Balozi wa Uingereza allwahi kunukuliwa akisema bajeti ya Tanzania ni sawa na kiasi wenyeji wa London wanachotumia kununulia CD za muziki.
Hâta tukikusanya tr2 kwa mwezi hazitoshi kuwaendeleza wananchi wote,na kuwafanya waache kula viwavi na kulala kwenye tembe kama mifugo.
NB:Kenya wako wachache kuliko sisi,makusanyo yao ni zaidi ya mara mbili kuliko sisi lakini bado wanapokea misaada kiasi fulani
Mwisho jiulize déni la taifa trillioni 40 kwa mwendo huu litalipwa lini
kama mtaendelea kuwa na fikra za kusaidiwa kamwe hautaendelea na maendeleo hayaji kama chafya.kumbuka mtegemea cha nduguye hufa maskini
 
Umeongea vyema mkuu
Lakini hebu tujiulize
Pesa hizo za serikali zitapelekwa kila mwezi
Tukiacha ule wizi wa wakuu wa shule naamini zitatimia

Mkuu hapa naomba ufafanuzi zaidi. Hizo pesa Tshs. 140,000/= ni matumizi ya mwezi na ni lazima zitumike, hivi Mkuu wa shule ataiba Shs. ngapi katika hizo? Umesema hizo pesa zitatimia kwa vipi na mahitaji ni ya kila mwezi?.
 
Hivi ile gesi ya kinyelezi tuliyoambiwa uchaguzi wa mwaka jana ukiisha mgao wa umeme utakuwa histolia vipi Haujaanza kazi?
 
Jakaya wakati anaingia Madarakani Serikali ilikuwa inakusana 170Bilioni.... Akaongeza hadi kufikia 900Bilioni.
Halafu kila akisikia makusanyo ni mabilioni basi anawashwa safari ili akazitumbue ulaya na usa yeye na maswahiba wake. Chezea mkwere wewe.
 
Ni kweli TZ ni tajiri sana.Kwa jinsi tunavyokwenda kwenye makusanyo nadhani ingekuwa busara tukajiwekea lengo la Trill.2.5 ili jamaa wasilale.Na lengo hili naamini linawezekana.Uvujaji wa mapato ulikuwa mkubwa mno.

Back
Top Bottom