Makusanyo Januari kufikia Sh tril 1.5

Makusanyo Januari kufikia Sh tril 1.5

To serikali:
Acheni misifa isiyo na tija.. Kama makusanyo yamekuwa makubwa tayari mnangoja nini kulipa madeni ya wazabuni!? Miradi na shughuli zetu zinakwama nyie mmeweka hela tu hamtulipi.
Tulipeni basi chap chap maisha yalegee kidogo.
 
Daily news and habari Leo wamekosea sijui in Bahati mbaya au laaa ila kamishna wa Tra kasema wanatarajia 1.050 trillion
 
waniongezee mshahara sasa!mi ni wa kima cha chini but makato ya kodi mpaka nadata!
 
Hizi sindimba mbona zinakua kila kukicha..???

Hayo makusanyo SISI wananchii yanatuhusu nini??..
Wanatakiwa watupatie mipango ya maendeleo ya miaka mi5 kwakutegemea hizi pesa hewa wanazo turingishia kila mwisho wa mwezi.
Acheni maigizo sababu hayatusaidii chochote hasa hizo hotuba zenu za makusanyo ya kila mwezi
Ukiishi kiushabiki utaona si muhimu kwako
 
Sio ku panic, bali huyo jamaa eti kwa akili yake anaona makusanyo kuwa makubwa ni kama kuwakomoa wapinzani. Utadhani hao wapinzani wanachangia kodi zao kwa serikali ya Msumbiji.
Hospitali zikipata pesa na kuboreshwa wanakwenda wote, mapato yakiwa mazuri na barabara zikitengemaa wanapita wote, sasa utaonaje kuwa hilo jambo mwingine kakomolewa?
Hizo ni akili zake matope tuu, maana mie naweza kuwa mfuasi wa Chadema na mama yangu akawa mfuasi wa CCM na mjomba ni ACT lakini wote tunafarijika na kazi ikifanyika ya kukusanya na wote tukapata huduma nzuri za kijamii.
Siku mojamoja ukichaa ulee wa CDM unakutoka
Hahaha
 
Much as tungependa makusanyo yaongezeke hata kufikia trilioni mbili, lakini napenda kuwapa angalizo wana JF. Taarifa hizi, kama zilivyoripotiwa na gazeti la habari leo, sio sahihi. Mwandishi, pamoja na mwariri wake, wamechanganya mambo. Lengo la makusanyo lilikuwa trilioni 1 na bilioni 45, na mpaka taarifa inatoka zolishakusanywa trilioni 1 na bilioni 31. Wanatarajia kufikia Jumatatu wafunge mahesabu ya Januari wakiwa na zaidi ya trilioni 1 na bilioni 50.

Tatizo ni mwandishi kushindwa kutofautisha trilioni 1.045 likiwa lengo la Januari, na trilioni 1.4 (trilioni 1 na bilioni 400) zilizokusanywa December 2015.

Huu ndo ule ukanjanja unaozungumziwa kuhusu waandishi wetu walio wengi
Basi vizuri mkuu
 
kuna huyu jamaa anajiita MOTOCHINI
huyun jamaa yeye anarukiarukia points za wenzie utamsikia
"ndio"
"tupe point hahaaa"
"hihihi nyumbu wa CDM"
ndugu bdlika na zama toa hoja jadili kwa hoja usidandie points alaf huna maelzo ya udadavuzi wa kina
ushauri2
epuka povuuuu
 
Pesa zilizopelekwa January mashuleni ns February wqmapeleka kiasi hicho hicho!
January pesa zilitosha kwa kuwa SHULE zilifunguliwa katikati ya january. Lakini kwa mwezi wa February haziwezi kutosha. Labda wapeleke Mara mbili ya kiwango kilichopelekwa january!
 
UKAWA watasema hizo ni kodi za makontena yaliyoshikwa bandarini!
 
Wewe ndio mgese wa akili kutokana na kuchezewa kikubwa utotoni
Tunafanya comparison na mataifa mengine ili tujue tuko umbali gani kufikia maendeleo na ustawi WA kweli. Tunajifunza kutoka kwa waliotutangulia tujue njia ya kupita
Next time uwe na manners to your betters when addressing them
Imbecilic buffon


Hauwezi kulingansha nchi kama Uingereza yenye uchumi wa dola US trilion 2 na nchi yetu ya TanZania yenye uchumi wa dola bilion 60 tu, ni mjinga tu na ndiyo anaweza kufanya ulinganisho wa namna hiyo, kwa maaana hata unaanzia wapi kulinganisha na TanZania ambayo ni nchi inayoondelea yenye umri wa miaka 51 tu ulinganishe na Uingereza yenye umri wa Miaka zaidi ya 700 kama nchi na nchi ambao ilitawala 1/4 ya Dunia nzima?


Hili tunajifunza tangu shule ya msingi jinsi ya kulinganisha vitu vinavyolingana na siyo visivyolingana!
 
Nadhani kuna tatizo kubwa sana when it comes to usahihi wa taarifa. Mimi nilisikiliza taarifa ya habari na kuwasikia hao mabwana wa TRA wakidai kuwa lengo la makusanyo ya January 2016 ilikuwa ni shilingi trilioni moja na bilioni 45. Mpaka jana walikuwa wamekusanya trilioni moja na bilioni 31, na kwamba kufikia Jumatatu wanategemea kuvuka hilo lengo walilojiwekea.
Sasa naliona tatizo hapa kwa mwandishi wa habari hii: trilioni 1 na bilioni 45 sio sawa na trilioni 1 na bilioni 450...(1.045 trilion sio sawa na 1.450 trilioni).

Mods, rekebisheni hii taarifa, wengi watapotoshwa hapa
Tatitzo la weledi katika nchi yetu ndipo hapa linapoanzia kwa maana kupata kazi kwenye gazeti tajwa kigezo kikubwa ni vyeti vyako na mara nyingine hata kama umevipata kariakoo mradi uwe na wa kukushika mkono.
Mwandishi kama huyu hata ukimkuta anajaza slips za kuweka pesa benki inakuwa shida, ukimwmbia andika kwa maneno 257,652.42 hawezi! Na ndio hawa hawa wanaosisitiza bunge lisionyweshwe live.
Sote tunapenda na tunamuombea JPM akusanye kodi zaidi lakini tuwe makini tusiwazidishie mzigo huo walipaji pia tukishakusanya basi zitumike kwa adabu halisi ya matumizi na sio ufujaji!
 
Wewe Ni buffon hujui hata cardinal principle moja ya development economics sasa kumfundisha punguani Ni mission impossible


Hata kama sijui yote hayo lkn nina akili za kutosha kujua kwamba hauwezi na haupaswi kulinganisha vitu visivyolingana na hii kanuni tunafundishwa tangu watoto shuleni tuliambiwa kulinganisha ndizi na ndizi, machungwa na machungwa na siyo kulinganisha ndizi na machungwa kuna hata sababu kwa nini kwenye michezo kuna makundi ya vijana, wazee, jinsia hizi zote hupangwa tofauti hivyo hii ni kanuni ya kwanza kabisa ambayo binadamu hujifunza sasa nakushangaa wewe unayejiita mchumi kama unashindwa kuelewa jambo rahisi kama hili unaweza hata kuchukuwa samples za utafititi wako na baadaye kufanya data analysis? Kwa maana hapa unahitaji hii kanuni ya kuangalia vitu vinavyolingana kwanza na kuviweka pamoja!
 
Back
Top Bottom