Makundi ya vijana wa Kitanzania ambao hujihisi wameyapatia maisha

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
4,549
11,943
- Wanaojua kuzungumza Kiingereza hata kama wanazungumza Kiingereza "broken". Wote ni mashahidi, hawa hata hapa JF wapo. Siku zote hujihisi wao ni bora na maisha wameyapatia.

- Wanaomiliki matoleo mbalimbali ya simu za iPhone. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Waliochukua mkondo wa masomo ya sayansi walipokuwa sekondari na baadaye wakaenda vyuo vikuu kusomea kozi mbalimbali za uhandisi. Hawa hata ukiwakuta mtaani bila ajira, by default wanajihisi tayari wameyapatia maisha.

- Wenye followers kuanzia 20K, 30K, 40K au zaidi kwenye mtandao ya kijamii. Hili ni kundi ambalo linajihisi limeyapatia sana maisha kwa kuwa na followers wengi. Wanafollow mastaa tu. kama wewe sio star usitegemee ukurasa wako kupata followback au like kutoka kwenye kundi hili.

- Wahitimu vijana wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Siongezi neno kuhusu kundi hili.

- Vijana wa Kitanzania ambao kwa wakati fulani waliwahi kuishi Marekani au Uingereza halafu kwa sasa wamerudi Bongo kupambana na msoto wa maisha.

- Wanaomiliki gari jamii ya Vitz, IST na Altezza. Jeuri na mikwara yao barabarani inatupa picha halisi.

- Wanajeshi vijana miezi yao kwanza kwenye ajira Jeshini halafu uwakute Uraiani wamevaa zile sare zao zenye mabaka mabaka.

Ongezea wengine unaowajua.

Karibuni.
 
Tunakwama wapi kama taifa? Niliamini tukiwa na watu wanaofanya tafiti itasaidia sana watoa maamuzi kupanga na kutekeleza mipango sahihi yenye tija. Mbona tuna watu wanavipaji na uwezo mkubwa tu kwenye tafiti na intelijensia?

Hii kazi yote iliyofanyika hapa sio ndogo!!!


Ila sipo kwenye kundi hata moja hapo juu, kwa mbaaali nilisoma mchepuo wa sayansi ila ndio ikawa elimu yangu ya juu kabisa sekondari.
 
Jana nilikua na-argue na malaya mmoja twitter, kisa ana followers elfu 25 anajiita motivational speaker, basi mimi nina followers chini ya 100 pamoja na a/c kua ina miaka zaidi ya 9 twitter, basi anajiona mkuuuubwa na mjaaanja kisa ana followers 25k na anatweet kwa iphone basi anajiona mjaaanja,unawaangalia unawaonea huruma.

Watu wa hivyo wanajiona wameyapatia sana maisha huku sisi tusio na followers wengi tukionekana hatuna kitu.

Watu wengine hovyo sana.
 
Back
Top Bottom