Achman kilangi
New Member
- Aug 23, 2019
- 2
- 2
Serikali yoyote inayoheshimu utawala wa kidemokrasia huongoza Kwa kugawa mamlaka Katika ngazi tofautitofauti. Lengo likiwa ni kumrshishia kiongozi mkuu wa nchi na serikali ambaye ndiye Rais na kiongozi mkuu wa nchi na aliyebeba dhamana ya kufikia matarajio ya wananchi anaowaongoza Katika nyanja zote za maisha kama vile uchumi bora, siasa bora na mahusiano yenye tija na mataifa mengine.
Hivyo Katika kupewa mamlaka ya uongozi watumishi ikiwemo vijana Wenye Umri mdogo hukabidhiwa bendera ya utumikiaji wananchi Katika maeneo tofauti huku tukiamini Kwa Umri Wao wananchi watanufaika na mengi ikiwemo;
1) Utendaji wa kisasa zaidi unaojumuisha matumizi ya digitali Katika kuboresha majukumu Yao.
Viongozi vijana wameweza kuendana na maendeleo ya kidigitali Katika kutimiza majukumu waliyokabidhiwa mfano kutangaza malengo na ilani ya vyama vyao husika walivyotokea. Kwa kutumia mitandao yao ya kijamii wameweza kuufikia umma Kwa haraka na ukubwa Zaidi ikilinganishwa na namna ya uongozi wa viongozi wenye umri mkubwa ambao hawakukua Katika Ulimwengu wenye mabadiliko hayo.
2) Wepesi Wao Katika kuyafikia maeneo yenye changamoto.
Kutokana na Umri wao mdogo, kibaiolojia miili yao huwaruhusu Kwa wepesi zaidi kuzunguka Kwa muda mfupi zaidi kuweza kuyafikia maeneo yenye kuhitaji utatuzi Kwa kuyafikia ana Kwa ana na kuyachukulia hatua. Unataka wao wa mwili na akili huruhusu wafanikishe utumikiaji wao Kwa wepesi zaidi tofauti na viongozi ambao umri umesogea ambayo spidi yao kiuhalisia imepungua.
3) Kuwakilisha kundi kubwa la raia ambao ni vijana wenzao ambao ndio waliobeba asilimia kubwa ya wananchi. Viongozi vijana Kwa Kuwa wao huwakilisha kundi hili kubwa Zaidi na kiukweli wanafahamu kiuhalisia nahitaji ya kundi hili muhimu hivyo viongozi hawa Huwa kwenye nafasi Nzuri zaidi Katika kuleta mabadiliko Kwa wanaowatumikia kwani wanakuwa na uelewa wa nini hasa kinachohitajika kuweza kupiga hatua kama nchi.
4) Kuijenga AU kuibadilisha jamii kifikra na kimtazamo Kuwa hata vijana au watu wenye umri mdogo wanaweza kuaminiwa na kupewa mamlaka ya kuongoza Wengine na hata Kuwa sehemu ya maendeleo. Kwa kupewa dhamana hizo kubwa vijana huwafanya vijana wenzao hasa walio masomoni kutia nia na ari Katika Yale wanayoyasomea ili kujitengenezea nafasi nzuri zaidi kulitumikia taifa pale wanapohitimu kwani huwa hawavunjwi moyo na dhana ya kuwa nafasi za kiuongozi ni za watu wakubwa kiumri.
5) Viongozi wenye umri mdogo huongoza AU kutumikia watu wakiongozwa na elimu ya kisasa zaidi na iliyo sawa na mahitaji ya Ulimwengu wa sasa hasa nyanja za teknolojia, afya, na biashara tofauti na viongozi wenye umri mrefu ambao mifumo ya elimu zao Unaweza Kuwa ya kizamani kuendana na utatuzi wa changamoto za kisasa zaidi Katika maeneo husika wanayoyafanyia Kazi Ikilinganishwa na viongozi vijana ambao huweza kutatua changamoto hizo Kwa ustadi Zaidi kwa kushirikisha elimu waliyoipata hivi karibuni ambayo inashabihiana hasa na mazingira yaliyopo Kwa Wakati huo.
Lakini pamoja na manufaa yote Hayo na mengine mengi ambayo sikuyajumuisha hapa, bado kumeonekana kupungukiwa kwa Utendaji wao Kwa wananchi. Baadhi ya viongozi wenye umri mdogo pale wanapokabidhiwa mamlaka ya kiuongozi Katika maeneo mbalimbali ya kutumikia wananchi wameonesha mapungufu Katika Utendaji wao Ambayo ni muhimu kuyafanyia Kazi ili yasiharibu taswira ya kundi hili la vijana na Kuondoka maana na matarajio ya kiongozi husika anayewapa mamlaka hayo. Baadhi ya mapungufu Hayo ni kama;
1)Utendaji usiojumuisha busara na Hekima kama viongozi wa idea au taasisi wanazozitumikia.
Kama tunavyofahamu Umuhimu wa kutumia busara binafsi au Hekima hasa kutatua matatizo yanapotokea Kwa Kuwa hii huepusha hali au taswira mbaya Zaidi ambayo ingeweza kufikiwa iwapo busara au hekima isingetumika. Kwa viongozi hawa wa umri mdogo baadhi Yao wamejikuta wakitenda Kutokana na mihemko binafsi na maamuzi Yao binafsi hata pale inapohitajika busara Zaidi kutumika badala ya mamlaka waliyopewa.Tofauti na viongozi wenye umri mkubwa ambao wengi wao hukumbuka Umuhimu wa kutumia busara pale wanapokuwa kwenye nafasi na mazingira ya kutoa suluhu au utatuzi wa changamoto Fulani katika nafasi zao za uongozi Ndani ya jamii wanazotumikia.
2) Baadhi ya viongozi hawa vijana hutaka kutumia nafasi walizopewa kuhakikisha wanaishi maisha ya kisasa wanayoyaona Kwa watu wengine wakubwa hata inapokuwa nafasi hizo hazimudu aina hiyo ya maisha.
Kutokana na ujana wao kuhitaji mambo mengi hasa ya kisasa na wao Kwakuwa umri unawaruhusu husahau dhamana walizopewa na mipaka Yao kama viongozi na kujikuta wakitamani aina Fulani ya maisha kama vijana na hivyo kujikuta wakitumia nafasi walizokabidhiwa kutumikia wananchi kujinufaisha au kuyafikia aina ya maisha hayo wanayoyatamani. Hivyo Vijana hawa hutumia vyeo vyao kama daraja la kufanikisha au kuyafikia maisha yasiyo ndani ya Uwezo wao hivyo kuweka pembeni kusudi la kwanza la kuwaletea maendeleo wananchi.
3) Viongozi hawa vijana baadhi Yao huamua kutumia elimu zao na maarifa ya kisasa wanayoyaona vyuoni na mashuleni kufanya uhujumu na udanganyifu kwa serikali yao na kurudisha nyuma mipango na dhamira ya kiongozi aliyewapa mamlaka hayo na hata kuwaangusha wananchi ambao walikuwa na matarajio mengi kwao. Tofauti na viongozi wenye umri mrefu ambao elimu Yao pengine haiwaruhusu kufahamu mambo mengi ya mkato au yasiyo Wazi kuyahusisha Kwa lengo la kufanya udanganyifu Katika maeneo yao ya Kazi.
Sasa ili kuweka Imani na kufikia malengo ya kuwapa nafasi vijana Katika utendaji inatupasa kufanya maboresho Katika baadhi ya maeneo ili kurudisha Imani Kwa wananchi na mamlaka zao za uteuzi;
1) Viongozi vijana wasiteuliwe Kwa kuzingatia vyama vyao vya siasa walivyotokea. Hii huwapelekea viongozi hawa kufanya Kazi Kwa kuweka mbele matakwa ya vyama vyao na Sio matarajio ya mamlaka walizopewa kuzifanyia Kazi. Badala Yake ufanisi unapaswa kuwa sehemu ya vipaumbele vya kuwapa nafasi vijana hawa kuwaingiza Katika mifumo ya Utendaji kuwatumikia wananchi.
2) Kabla ya uteuzi wa viongozi kufanyika haswa viongozi hawa vijana kunapaswa kuwe na ufuatiliaji wa maadili yao tangu wakiwa masomoni na kuweza Kupata mrejesho wa watu walioishi nao Katika mazingira tofauti tofauti ili kuyazuia matatizo wanayoweza kuyasababisha Katika Utendaji wao. Ni muhimu kuwafahamu vyema vijana hawa Kwa kufuatilia Historia zao walikotokea na tabia zao na sio kuzingatia ubora wa vyeti vyao vya taaluma Pekee kwani taaluma na maadili huwa Vitu viwili tofauti.
3) Tume ya maadili inapaswa kupewa meno Zaidi ya kuwawajibisha viongozi hawa wanaokiuka maadili ya uongozi Katika nafasi zao za utumishi na isiwe kiongozi aliyewateua Pekee Kuwa na mamlaka ya kuwawajibisha kwani pengine huchelewa kuyaona au kuyafikia mapungufu hayo Kutokana na wingi wa majukumu Yake.
4) Viongozi vijana waanze kupewa madaraka ya ngazi za chini kabla ya kuwapa mamlaka makubwa ili kuweza kuwafahamu vizuri tabia zao Kwa kufuatilia Utendaji wao.
Hii itatoa taswira ya kiasi cha mamlaka wanayopaswa kupatiwa bila kuathiri matarajio ya watumikiwaji na mamlaka zinazowateua.
5) Viongozi vijana wanapaswa kuwajibishwa hata wanapokuwa nje ya Viti vyao walivyovitumikia ikiwa wakitenda kinyume na maelekezo na matakwa ya nafasi zao. Hii itawajenga vijana wenzao ambao Wana ndoto za kuutumikia umma hapo baadae kwani huona madhara ya uongozi mbaya na athari Zake kwao binafsi na jamii waliyoitendea Isivyo.
Kiujumla viongozi vijana ni chachu ya maendeleo Katika taifa lolote linalohitaji kupiga hatua kimaendeleo Lakini pia ni kundi linalopaswa kutazamwa ziadi kimaadili ili kutoruhusu taswira mbovu na matokeo hasi ya uongozi kwa jamii wanazozitumikia na Zaidi kwa kiongozi au mamlaka zilizowateua zikiamini wao Kuwa Msaada mkubwa Katika kufikia matakwa ya wananchi.
Nawasilisha andiko hili na shukrani za dhati Kwa Jamii forums ikimpendeza Mungu likawe mwanzo wa mabadiliko Katika jamii yetu ya kitanzania.
Wenu Katika ujenzi wa taifa,
Achman Charles Mashiku.
0682103680.