Makundi mbalimbali ya Watanzania wanaoichukia serikali ya Rais Magufuli na kwanini wanaichukia...

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,848
20,697
Tumeshudia Rais Magufuli akitukanwa kwa sababu zisizo za msingi kabisa,tena wakati mwingine kwa kufanya mambo ya msingi ambayo kama nchi tunayahitaji.Tumeshuaudia pia akibezwa na kudharauliwa.Lakini ni akina nani hasa wanahusika na vitendo hivi ambavyo si vya kiungwana kabisa, vyenye nia ovu ya kumkatisha Rais tamaa?Nimewagawanya watu hawa kwenye makundi makuu manne Makundi hayo na sababu ni kama ifuatavyo:-

1.Watu hao inawezekana kabisa kuwa ni vibaraka wa mabepari na nchi za magharibi,waliotumwa kukejeli na kujifanya wanadharau kila jambo jema,ili serikali ya awamu ya tano,ionekane si lolote si chochote,na hatimaye kudharaulika na wananchi.Watu wa aina hii serikali inapofanikiwa katika jambo lolote,wanaona kama hawajafanikiwa katika kazi waliyotumwa kuifanya.Lakini naomba tukumbuke kwamba mti kwenye matunda ndio unaopigwa mawe,kwa hiyo Magufuli ana matunda!

2.Lakini wapo pia watu wa vyama vya upinzani,hasa CHADEMA.Hawa kama vibaraka,nao wanatetea matumbo yao,so ni lazima wakosoe kila kitu,ili kuhalalisha uwepo wao.Wasipo onyesha kwamba serikali inakosea na haina inachofanya,kwa hiyo tunahitaji mabadiliko,uwepo wao utakuwa hauna maana.

3.Wengine ni watu ambao wameguswa moja kwa moja na utendaji wa Magufuli kwa njia moja au nyingine,ambayo imechangia maslahi yao ya kiuchumi kuathirika.Hapa yako makundi mengi,na si rahisi kuyataja yote.Hata hivyo naomba nitaje makundi machache tu.
i).Hawa wanaweza kuwa wana CCM ambao walikuwa wanafaidika na mihela ya mafisadi waliokuwa wanaifadhili CCM.

ii).Watu waliokuwa na vyeti feki ambao walienguliwa katika kazi zao.

iii).Wafanyibiashara ambao walikuwa hawalipi kodi inavyotakiwa,na hivyo kuiibia serikali.

iv).Wafanyabiashara waliokuwa wanafanya biashara zenye utata na zisizo halali kama Bureau de Change,na sasa biashara zao zimeathirika au kufutiliwa mbali.

v).Watumishi waliokuwa wanaiibia serikali kwa mbinu zozote zile,na mbinu hizo sasa hazipo tena.

vi).Wauza madawa ya kulevya kwa sababu zilizo wazi.

vii).Watumishi wazembe na wasio na weledi.Hawa wanaona maisha ya kazi katika zama za Magufuli ni taabu sana.No wonder watumishi wengi wanatamani muda wao wa kustaafu ufike haraka.

viii)Watumishi waliohamishiwa Dodoma na kuacha miradi na majumba yao Dar es Salaam.

ix)Wafanyabiashara wa malori makubwa na mabasi,hasa wa ukanda wa Dar-Kigoma,Dar-Mwanza,Dar-Arusha,Tanga-Arusha.Hawa wanahofia biashara zao kuathirika baada ya ujio wa SGR na kuboreshwa kwa reli ya Dar-Arusha na Tanga-Arusha.Nadhani mnakumbuka incidence ambayo mmiliki wa mabasi ya kampuni fulani alishiriki kung'oa mataruma ya reli ya Moshi-Arusha.Episode ile ina-prove kwamba point hii ni kweli.

x)Ndugu wa makundi hayo hapo juu.

4.Wafuata upepo wasiokuwa na mawazo yao original,kwa vile hawana ufahamu wa kutosha,kwa hiyo wanadakia kila wazo hata baya,na hivyo kupotosha umma.

Naomba nimalizie kwa kusema tena,kwamba si rahisi kutaja makundi yote,kwa hiyo naomba kwa leo niishie hapo.
 
Sio kwl mtoa mada...yote uliyoyazungmza ama kuyandika..nikulize wewe. Je idadi ya wanaokosa ajira inakurdhisha?je mwenendo wa kuporomoka kwa sekta binafsi unakufurahisha? Je mwenendo wa democrasia kwenye taifa letu unakufurahisha? Je Sera ya kilimo kuhusu uzalishaji na masoko unakufurahisha? Je mfumo wa kuadhibu watu ama kwa kupoteza au kufungulia kesi za uhujumu uchumi watu paspokufuata sheria kunakufurahisha? Semeni ukweli ili system ijifunze inapokosea nchi hii ni yetu sote hakuna atakayeondoka nayo akifa!!
Kumbukeni tunahtaji kutenda mema ili vzazi vyetu vije vijifunze ustaarabu wetu!!! areafiftyone,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkulima gwakikolo,
Hakuna nchi ambayo viongozi wake wako perfect.Si Marekani,Uingereza,Ufaransa au popote pale.Ujue haaa niliyo andika ni sahihi,Donald Trump amekuwa impeached kwa kuwa Wamarekani hawaridhiki naye, David Cameron na Theresa May waliondoka madarakani kwa kuwa Waingereza hawakuridhika nao, Ufaransa kila kukicha leo ni maandano kwa kuwa Wafaransa sera za Macron hawazitaki.Jamani hakuna mahali ambapo things are perfect, ila Magufuli anajitahidi under the circumstances.

Jambo la kushangaza ni kwamba sikuona Kikwete au Mkapa wakitupiwa madongo kama Magufuli,ingawa serikali zao zilikuwa za hovyo sana.Why?Kwa sababu makundi yote niliyo yaorodhesha yalifanya mambo kama yalivyotaka.Leo Magufuli akiridhia uovu wao,kelele zote zitakwisha.Hata wewe naamini unayoyasema ni scapegoat,sababu za kuichukia serikali za awamu ya tano unazijua mwenyewe,ila naamini upo kwenye kundi au makundi niliyo yaorodhesha.
 
Awamu hii sioni kundi wala mtu alienusurika kuumizwa au kuathiriwa na maamuzi ya serikali hata wewe muandishi unajua yote so stay cool wote tunachukia serikali sema hatuna uhuru wa kueleza yaliyo moyoni kwa sababu mbali mbali ikiwemo kulinda ugali,kifungo na kupewa ma kesi ya uhujumu uchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeye ni mzalendo aliyekosa kazi baada ya mgodi wa bulyanhulu kufungwa. Haya majina ya areafiftyone zone zero, zone two etc yapo ndani ya mgodi wa bulyanhulu. Obviously this was a miner. Hata uandishi wake ni wa kiwango cha chini sana, kawaida ya maminer.
Areafiftyone(Area 51) iko Marekani mkuu, haipo Bulyankulu.Hii peke yake ni proof tosha kwamba ufahamu wako ni mdogo.Kuhusu uandishi,naamini you can only dream of my capacity.
 
Jibu hoja mkuu mwenzako ameleta hoja hapa JF! Au uko kwenye group la kufuata upepo!
Mkuu mimi sijaona hoja zaidi ya pumba tuliyozoea kutoka kwa watu wa aina yake humu. Kinachotrend kwenye nchi hii kwa sasa ni US wamefikiaje kudeal na mtu mmoja ambaye wala hayupo katika list ya viongozi wa kitaifa nchini halafu kuna mtu anakuja na blah blah za vyeti feki sijui kuhamishwa Dodoma. Kweli?
 
Areafiftyone(Area 51) iko Marekani mkuu, haipo Bulyankulu.Hii peke yake ni proof tosha kwamba ufahamu wako ni mdogo.Kuhusu uandishi,naamini you can only dream of my capacity.
Mkubwa sitokaa nidream for sort of this write up. Kabisa.
 
Awamu hii sioni kundi wala mtu alienusurika kuumizwa au kuathiriwa na maamuzi ya serikali hata wewe muandishi unajua yote so stay cool wote tunachukia serikali sema hatuna uhuru wa kueleza yaliyo moyoni kwa sababu mbali mbali ikiwemo kulinda ugali,kifungo na kupewa ma kesi ya uhujumu uchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi siichukii.Ni kweli yapo mambo machache ambayo si ridhiki nayo,but overall,serikali ya awamu ya tano inafanya vizuri.Kama ni marks naipa 80%.
 
Rais tuliyenaye sasa ana maono,anauthubutu na ni mkali.Kwa Watanzania tulipokuwa tumefika,huyu ndiye Rais tunayehitaji.Infact mimi ningetamani awe mkali na awe na uthubutu zaidi.

Maono angefanya yafuatayo

1. Kukuza Ajira

2. Kuhakikisha tunapata katiba bora sio bora katiba

3. Wasiojulikana wote angewashughulikia

4. Angehakikisha demokrasia ya kweli sio democcm

5. Angebiresha Elimu yenye tija sio GPA za Vilaza wasiweza chochote

Nk

Nk
 
Back
Top Bottom