Makumbusho ya Taifa na bidhaa za kukumbuka

maramojatu

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
1,175
1,542
Za jumapili wanaJF,
Leo naomba nitumie jukwaa hili adhimu kuelezea niliyokuwa nimeyaona kwenye makunbusho yetu ya Taifa nilipotembelea hapi wiki mbili zilizopita. Nimewahi kutembelea pia miaka ya nyuma.

Nakiri makumbusho ni sehemu muhimu ya kujifunza Kwa hiyo inabidi kuwepo na vitu vya kutosha vya kihistoria kwa wananchi kukumbuka.
Kwenye makumbusho yetu nimeona vitu vichache sana vinavyohusu historia ya mtanzania. Kwenye siasa emphasize imekuwa kwa Nyerere na machifu wachache. Sikuona contribution ya wananchi kwenye hata hiyo siasa.

Pia historia ya ukoloni imepewa kipaumbele sana, siasa ya Tanzania kabla ya ukoloni sikuona imepewa kipaumbele kihivyo.
Pia vitu vya maonyesho vimebaki ni vile vile miaka nenda miaka rudi, havibadiliki. Nashauri wanahistoria wetu waendelee kutafiti vitu vilivyotumika miaka mingi ilopita kwa kuwatumia wananchi.

Cha kushangaza tena nimekutana na kona ya Wamarekani... Jamani tuwe makini hivi tukienda Washington DC makumbusho yao itakuwa na kona ya kuelezea historia na matukio ya Tanzania?
Ushauri wangu tuwatumie wananchi kuendeleza vitu vya kuonyesha kwenye makumbusho ya Taifa na tuonyeshe historia halisi ya utamaduni wa mtanzania kwenye nyanja zote na sio tu siasa za Nyerere na ukoloni.

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom