Makubwa ; Ney wa mitego kujenga kanisa

Jimmy George

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,733
1,648
Nay wa Mitego anasema anafungua kanisa lake la kumuabudu Mungu.

Amedai kuwa kanisa lake litakuwa si la biashara, bali la kumuadu mwenyezi Mungu aliye hai.

“Acha kanisa likamilike, mwenye Mungu asimamie tutajua nini kinaenda kutokea lakini sio kanisa kwaajili ya kupiga hela,” Nay aliiambia E-News.

Nay amedai kuwa mchungaji wa kanisa lake atakuwa tofauti na hatotegemea sadaka za waumini ili kuendesha maisha yake, bali kazi yake nyingine itakayoweza kumuingizia kipato.

Rapper huyo amejinadi kuwa anatarajia kupata waumini wengi kupitia kanisa lake na kwamba litakuwa chanzo cha mafanikio katika mambo yao.

Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam.

Source: Bongo5
 
Huyu ni mnafiki kuna siku alikuwa anahojiwa na kituo cha matangazo cha RFA William Bundala alimuuliza Nay vipi unaamini uwepo wa Mungu? Nay
siyo kivile na mara ya mwisho sikumbuki nilienda lini kanisani labda nilipokuwa kuwa mdogo sijajitambua lakini mpaka leo hii sijawahi
 
Source; bongo5
Watu wengi siku hizi wanaelewa kanisa kumaanisha jengo. Huku si kuelewa kibibilia maan ya kanisa. Neno “kanisa” maana ya asili yatoka kwa neno la Kiyunani ekklesia lili lo na maana ya “kusanyiko” au “walioitwa.” Maana ya asili ya “kanisa” sio ile ya jengo, bali ni watu. Ni kinaya kwamba unapowauliza watu ni kanisa gani wanashiriki, mara nyingi huwa wanajihushisha na jengo. Warumi 6:5, yasema, “…salimia kanisa linalokutana kwa nyumba.” Paulo anaashiria kanisa lilo katika nyumba yao- si jengo la kanisa bali mwili wa washiriki.

Kanisa ni mwili wa Kristo, ambapo ye ndie kichwa. Waefeso 1:22-23 yasema, “Akivitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.” Mwili wa Kristo umejengwa na wanaoamini katika Yesu Kristo toka siku ya Pentekosti (Matendo Ya Mitume 2) hadi Kristo arudi. Mwili wa Kristo uko na sehemu mbili:

1) Kanisa lote kwa ujumula ambalo ni wale wote wako na uhusiano na Kristo. “Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni Upendo” (1 Wakorintho 12:13). Aya hii inasema yeyote atakaye amini in sehemu ya mwili wa Kristo na ameupokea Roho wa Kristo ni ushaidi. Kanisa la jumla la Mungu ni wale wote ambao wamepokea wokovu kwa imani katika Yesu

2) Lile Kanisa ya nyumbani vile emeelezwa katia Wagalatia 1:1-2: “Paulo, mtume, (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu), na ndugu wote walio pamoja name, kwa makanisa ya Galatia.” Hapa tunaona kwamba katika mkoa (mji) wa Galatia kulikuwa na makanisa mengi chenye tunaita makanisa ya nyumbani. Kanisa la Kibaptisiti, Kilutheri, Katholiki na mengine, si kanisa, vile iilvyo katika kanisa la ujumla, bali haya ni makanisa ya nyumbani (Mshambani/Mjini), ule mwili wa nyumbania wa waumini. Kanisa la jumla linajumlisha wale wote ni wa Kristo na wamemwamini kwa wokovu. Washirika wa kanisa la jumla lazima watafute kuwa na ushirika na kujengana wakiwa katika lile kanisa la nyumbani.

Kwa ufupi, kanisa si jengo ama dini. Kulingana na Bibilia, kanisa ni mwili wa Krsito-wale wote wameweka imani yao kwa Yesu Kristo kwa wokovu (Youhana 3:16; 1 Wakorintho 12:13). Kanisa la nyumbani ni kusanyiko la Wakristo wa kanisa la jumla. Kanisa la nyumbani ni mahali ambapo washirika wa kanisa la jumla wanaweza kutumia nguz0 ya “mwili” ya 1 Wakorintho 12: himizana, funzaneni, na kujengana ninyi kwa ninyi katika hekima na neema ya Bwana Yesu Kristo.
 
Huyu ni mnafiki kuna siku alikuwa anahojiwa na kituo cha matangazo cha RFA William Bundala alimuuliza Nay vipi unaamini uwepo wa Mungu? Nay
siyo kivile na mara ya mwisho sikumbuki nilienda lini kanisani labda nilipokuwa kuwa mdogo sijajitambua lakini mpaka leo hii sijawahi
Ndio ivo... Tumemuhubiria mpaka amebadilika na kuamua kuwa balozi mzuri wa Yesu Kristo...
 
Jinsi anavyotukana kwenye nyimbo zake na sasa hili
Apelekwe kwa mkemia mkuu akapimwe anatumia nini
 
Huyu ni mnafiki kuna siku alikuwa anahojiwa na kituo cha matangazo cha RFA William Bundala alimuuliza Nay vipi unaamini uwepo wa Mungu? Nay
siyo kivile na mara ya mwisho sikumbuki nilienda lini kanisani labda nilipokuwa kuwa mdogo sijajitambua lakini mpaka leo hii sijawahi
Kwani anafungua kwa ajili ya kusali yeye?

Anafungua kwa ajili ya biashara.
 
Huyu ni mnafiki kuna siku alikuwa anahojiwa na kituo cha matangazo cha RFA William Bundala alimuuliza Nay vipi unaamini uwepo wa Mungu? Nay
siyo kivile na mara ya mwisho sikumbuki nilienda lini kanisani labda nilipokuwa kuwa mdogo sijajitambua lakini mpaka leo hii sijawahi
Binadam tunabadilika mkuu
 
Jamaa anajifanya kanye west eti au akina madona.
Eti na yeye anataka waru wamjengee conspiracy theories eti haeleweki.
 
Back
Top Bottom