Nashangaa sana kwamba Watanzania wengi, hasa watu wa bara, hawajagundua kwamba awamu ya sita imevunja muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar bila maandishi au matangazo. Hadi sasa kuna makubaliano kwamba Zanzibar watajifanyia kila kitu ambacho nchi rasmi inafanya isipokuwa hawatakuwa na jeshi la ulinzi.
Na kuna makubaliano kwamba serikali ya muungano haitaingilia jambo lolote au kutoa maelekezo yeyote upande wa Zanzibar kwa sababu sasa wamekuwa kama serikali kamili. Hata ziara za viongozi wa serikali ya muungano kule Zanzibar zimedhibitiwa. Na pia mabalozi wa nje wanapewa nafasi zao, na nadhani raisi wa Zanzibar ndie anateua watu wake na raisi wa Tanzania kutangaza rasmi.
Haya yote yamefanyika kimya kimya, na naweza kudiriki kusema yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika mazingira ya kuwa na raisi wa Tanzania kutoka Zanzibar. Hiyo imeonekana ni zile nafasi zinaitwa "it is now or never".
Ila jambo la kusikitisha ni kwamba katika hali hii Zanzibar ni kama imepewa fursa kubwa ya kujiendeleza haraka hasa katika miundo mbinu kwa sababu yajayo hayajulikani. Kama umeangalia vizuri, kuna miradi mikubwa ya miundo mbinu inayoendelea huko visiwani, pamoja na kubadilisha majengo ya shule karibu yote. Umewahi kujiuliza Zanzibar wanapata wapi fedha za kufanya haya mambo makubwa?
Ni kwamba, mbinu iliyotumika ni Tanzania kuchukua mikopo ya nje, ambapo sehemu kubwa sana ilienda Zanzibar kama gawio lao. Ile mikopo haikuwa kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania bara, mlengwa alikuwa Zanzibar. Ndio maana baadhi ya wanasiasa wa bara, walipogundua hilo walikasirika sana. Na tukumbuke kuwa daraka kubwa la kulipa hii mikopo liko Tanzania bara.
Ni kweli kwamba kuna fedha zinabaki Tanzania bara lakini faida kubwa ya ile mikopo ilikuwa ni kwa ajili ya Zanzibar. Tukichukua mkopo wa tuseme Trilioni 10, ukawapa Zanzibar gawio lao la trilioni mbili, zile trilioni mbili zinazoenda Zanzibar ni fedha nyingi sana kufanyia mambo mengi sana, wakati trilioni nane zinazobaki bara impact yake kuona zimefanya nini ni kidogo sana kwa sababu ya ukubwa wa nchi. Na ukweli ni kwamba mfumo wa gawio ulitengenezwa kwa kupendelea upande wa Zanzibar.
Sasa jambo ambalo limeanza kuwaamsha watu wa bara ni hili la meli za nje kusajiliwa Zanzibar. Kwa kiburi kabisa, pamoja na skendo zilizolikumba jina la Tanzania, Zanzibar wanadai tulishakubaliana tunajiendesha kama nchi kamili, na tuna haki ya kusajili meli. Wanadai kama hatutaki watumie jina la Tanzania basi mabadiliko yafanywe wazisajiri kwa jina la Zanzibar.
Na pia kuna baadhi ya wanasiasa wanahoji, kama Zanzibar wanaruhusiwa kujifanyia kila kitu kama nchi na kutoingiliwa, kwa nini bado wanateuliwa kwenye nafasi zinazohusu muungano au hata mambo ya bara peke yake? Baadhi ya majibu wanayopewa ni kwamba raisi ana uhuru wa kuteua timu yake ambayo itaona itamsaidia, na anaweza kuchukua watu bara au visiwani katika nafasi yeyote.
Kwa hiyo kila mtu akae akijua muungano haupo tena, makubaliano yamefanywa Zanzibar wajifanyie kila kitu isipokwa kuwaja jeshi, lakini makubaliano haya hayatatangazwa rasmi.