Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,279
- 33,880
MAKTABA YAPOKEA KITABU CHA VASSANJI KUTOKA MAREKANI
Kwa wale waliokulia Kariakoo ya miaka ile akisoma kitabu chochote cha Vassanji ataiona ile Kariakoo ya enzi zetu na yote yaliyokuwapo miaka ile.
Niliijua kalamu ya Vassanji kwa mara ya kwanza Amsterdam nyumbani kwa dada yangu marehemu Haki Kilomoni.
Kwa kujua mapenzi yangu ya vitabu gumzo letu lilikuwa vitabu na yeye akaniambia kuwa akiwa na hamu ya kuikumbuka Kariakoo tuliyokulia husoma kitabu cha Vassanji: "And Home was Kariakoo."
Ndugu yangu huyu aliyenipa hidaya hii aliyeko mbali naamini kabisa na yeye akitaka kuikumbuka nyumbani anamsoma Vassanji.
Vassanji kaandika vitabu vingi na kingine kinachogusa Dar es Salaam kakipa jina, "Uhuru Street."
Vassanji kaondoka Tanzania miaka mingi iliyopita lakini moyoni haijamtoka.
Sishangai kuwa kila aliyekuwa ughaibuni dawa ya kupoza ukiwa wake wa kuwa mbali na nyumbani ni kurasa za Vassanji.