Tatizo hili limekuwa sugu sana, Karibu kila chuo kuna wahadhiri hunyanyasa mabinti kwa kutumia kisingizio "Mwalimu na mwanafunzi wa chuo wote ni watu wazima"
wengine wamewahi kufumaniwa baada ya wanafunzi kupeleka ushahidi wa kunyanyaswa lakini wanaishia kuhamishwa vituo vya kazi, kuonywa au kufukuzwa kazi, HAKUNA KWENDA JELA !!
Huyu aliefungwa itakuwa katembea na binti wa mtu mzito, akaapa kula nae sahani moja
SUMBAWANGA: Aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo cha Paradise Business, Godfrey Mwakitalima ahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela
Mhadhiri huyo alikamatwa ndani ya chumba cha nyumba ya kulala wageni ya llembula iliyopo eneo la Chanji Wilaya ya Sumbawanga, alipokwenda kufanya mapenzi na mwanafunzi wake.
Hakufahamu kama mwanafunzi huyo ametoa malalamiko yake Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),iliyoandaa mtego na kumnasa mhadhiri huyo akiwa kitandani.
Takukuru ikampeleka mahakamani, mhadhiri huyo kwa kosa la kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake kama sharti la kumpa alama za juu katika somo la ujasiriamali.
Baada ya kusikiliza ushahidi wa jamhuri na Mhadhiri huyo wa Paradise Business College alijitetea kuwa mwanafunzi huyo alikuwa mpenzi wake wa muda mrefu,ila Mahakama ilimhukumu kifungo cha miaka 20 jela.