Makosa ya Tanzania yameinufaisha Msumbiji

Makosa ya Tanzania yameinufaisha Msumbiji

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,768
Reaction score
49,949
Wakati wa Awamu ya Nne, ugunduzi mkubwa wa gas ulifanyika Tanzania. Ni ugunduzi huu ndio uliomfanya Rais Kikwete kutamka kuwa yeye angekuwa Rais wa Mwisho kuongoza Tanzania maskini.

Prof. Muhongo naye kila mara alinena kuwa sasa uchumi wa Tanzania utakuwa ni uchumi wa gas.

Ilipoingia awamu ya tano, kila kitu kikavurugika. Tafiti zikasimama, mradi mkubwa kuliko yote tangu Tanzania iumbwe, mradi wa ujenzi wa kiwanda cha LNG, wenye thamani ya dola bilioni 30, wenye pesa wakaamua kusimamisha.

Wawekezaji wakaelekeza nguvu zao za utafiti Msumbiji. Leo Msumbiji inafahamika kuwa na gas nyingi kuliko ya kwetu. Sasa kiwanda kikubwa kabisa cha LNG kitajengwa Msumbiji. Nasi tutafaidika kwa kuagiza gas toka Msumbiji!! Ndiyo utajua ule msemo, 'kosa mali upate akili'.

Bonde la Ruvuma lipo Tanzania na Msumbiji. Aquifer ni ile ile. Na kwa sababu aquifer ni moja, visima vya gas vikiwekwa karibu na mpakani upande wa Msumbiji, basi kuna uwezekano wa gas ya Tanzania kujiendea yenyewe upande wa pili, na Msumbiji kujichukulia kilichokataliwa na mwenyewe, bila ya kukiuka sheria yoyote. Kwanza kwa upande wa Tanzania, bonde la Ruvuma, wala hatutaweza kujua kama tuna gas na mafuta au hapana.

Kwa sera zetu za sasa, hata gas tuliyo nayo, tusingejua kama tunayo.

Ukitaka kuona wenzetu walivyojizatiti kutumia mali zao za asili kujenga uchumi wao, soma zaidi:

Mozambique shows off Rovuma’s £42bn investment in bid to attract North Sea suppliers

7:27 CAT | 13 Feb 2020

0 Comments Print Share

[https://clubofmozambique]

Drillship Deepwater Millennium flaring offshore Mozambique, East Africa

Officials from Mozambique have showcased the level of investment in the prolific Rovuma basin in a bid to attract the expertise of North Sea companies to its supply chain.

Natalia Camba, local content manager from the country’s National Petroleum Institute, was speaking at the opening of Subsea Expo about a trio of projects off the country’s coast which have attracted a combined $54bn of investment (£42bn).

Mozambique’s oil and gas sector remains in its “infancy”, with hopes to attract UK expertise to further develop the industry.

Ms Camba said there are “opportunities everywhere” for suppliers, with the Rovuma Basin so far being assessed to have 165 trillion cubic feet of gas in place.

The region has two projects already in development: the $8bn Coral field which is due to begin production in 2022 and the $23bn Golfinho/ Atum field.

Meanwhile the third, the $23.6bn Rovuma LNG project, is due for final approval in the first quarter of this year and will produce 15 million tonnes of liquefied natural gas per year.

[https://clubofmozambique]Natalia Camba of Mozambique’s National Petroleum Institute
Ms Camba said the country offers “countless opportunities for investment” throughout the value chain, with the approval of projects “contributing to the building of infrastructure, hence boosting exploration interest”.

She pointed to a host of areas that UK firms could get involved in, from industrial services to supply vessels and lab analysis services, with the government’s local content regulations benefiting those who are in some way partnered with companies based in Mozambique.

The country expects further exploration drilling as a result of its upcoming sixth licensing round later this year.

Ms Camba was speaking at the Global Opportunities Business Breakfast hosted by Scottish Development International and the UK’s Department for International Trade.

Also speaking was Ketan Pednekar, SDI’s senior oil and gas trade specialist based in Mumbai.

He told the conference there was “a big opportunity for all of you to be suppliers for these subsea projects” upcoming in India, particularly major developments in the Bay of Bengal.

Mr Pednekar highlighted the third “cluster” of the 98/2 oil and gas project off the country’s east coast, which will see State-controlled operator ONGC invest $3.2bn.

[https://clubofmozambique]Ketan Pednekar of Scottish Development International
The award of works is expected next year ahead of production in 2023-24.

He also referenced work at the 2004/1 asset, also in the Krishna Godavari basin, which will cost $560m, with work expected to be awarded later this year.

By Allister Thomas
 
Sisi gesi sio kipaumbele chetu!, gesi ilikuwa kipaumbele ili tuitumie kuzalishia umeme, lakini sasa kwa vile tumegundua umeme wa hydro power ndio the cheapest, tumeamua kujenga Stigler na tutaingia mkataba na Mungu mwenyewe maji yasipungue!, zile kelele za mambo ya tabia nchi, joto dunia, etc, ni kelele za mabeberu tuu.

Angalia kwenye gesi yetu, akina sisi tulisema nini na lini




P
 
Wawekezaji wakaelekeza nguvu zao za utafiti Msumbiji. Leo Msumbiji inafahamika kuwa na gas nyingi kuliko ya kwetu. Sasa kiwanda kikubwa kabisa cha LNG kitajengwa Msumbiji. Nasi tutafaidika kwa kuagiza gas toka Msumbiji!! Ndiyo utajua ule msemo, 'kosa mali upate akili'.
'In fact' mkakati ulikuwa ni kuwawahi Msumbiji, ndio maana mambo yalifanywa yaende haraka haraka.

Sasa sijui kama ile Haraka yetu ilikuwa haina Baraka, ama ndio hivyo tena msemo huo wa 'kosa mali..."

Hivi ile mikataba ilikuwa mibaya kiasi cha kuiweka pembeni kabisa na kuanza kusuka upya?
Tulipiga mahesabu ya hasara za uchelewaji huo na kiasi ambacho tulikuwa tunapigwa, tukaona ni bora kusubiri..., hadi lini na Msumbiji kishashika soko? Msumbiji anayo nyingi zaidi, mara mbili ya yetu, hapo kweli tutafurukuta, au itabidi tusubiri hadi hiyo ya Msumbiji ianze kuisha...lini, miaka hamsini ijayo?

Hapa tulijifunga goli. Lakini akina Zitto na wenzake CHADEMA bado hawawezi wakalieleza hili mbele za wananchi nao wakapata ufahamu mzuri wa mambo ya ajabu yanayofanyika.

Badala yake, propaganda za kitoto sana zitatoka CCM kuwazubaisha wananchi..., hiyo ni sababu mojawapo inayofanya waTanzania walaumiwe, kumbe hawapati taarifa mbadala wanazoweza kuzipima na kulinganisha.
 
Paskali katika ubora wako.
Thanks, ubarikiwe,
Mimi ni mkweli na ukiwa mkweli too much katika jamii inayofurahia hadaa, unaonekana ni an enemy of the people.

Tumeichagua CCM kwa kura nyingi kutokana na kuikubali ilani yake. Miongoni mwa hoja kwenye ilani ile ni pamoja na kukamilisha mchakato wa katiba mpya, lakini after spending billions kwenye katiba, leo anaibuka mtu na kusema "katiba sio kipaumbele chetu":na anashangiliwa!.

Ilani ikasema mtoto wa kike akipata ujauzito shuleni, ataendelea na masomo, akaibuka mtu akasena serikali yake haitasomesha wapenda ngono! Kama sio kwa msaada wa watu wa Marekani, hili pia lingepita!

Kwenye ilani kuna energy strategic plan ya miaka 5, priority 1 ni umeme wa gesi ndio umeme wa uhakika, lakini sasa tunarudi kutegemea umeme wa maji ya mvua inayoletwa na Mungu, na kwa vile baadhi yetu wa Kanda ile sii mchezo!, mfano Mkama Rumanyika alikuwa ana i command mvua.
Hivyo tutaendelea kui command mvua, bwawa litajaa wakati wote.

Gesi tutaendeleza taratibu, ni yetu huko ardhini ilipo haihami nchumbiji, inatusubiria!.

P
 
Go Magufuli
IMG_20200124_145425.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom