Makosa ya Rushwa na adhabu zake kwa mujibu wa Sheria

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
132
500
Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11/2007 imeharamisha vitendo vya rushwa na sasa ni makosa ya jinai. Makosa hayo yameorodheshwa katika sehemu ya III ya sheria hii, hasa katika vifungu vya 15-39;

1) K/F 15 – kuomba, kushawishi, au kulazimisha kupewa rushwa, kutoa au kuahidi kutoa rushwa. (Faini Tshs- 500,000 – 1,000,000/= au kifungo cha miaka 3-5 au vyote kwa pamoja);

2) K/F 16 – kutoa au kupokea rushwa ili kupata mkataba wa kutoa huduma kwa idara ya umma au Shirika la Umma (faini Tshs 3,000,000/= au kifungo cha miaka 3-5 au vyote kwa pamoja);

3) K/F 17 – kutoa au kupokea ili kumpendelea mtoa rushwa au kufanikisha kupata Zabuni katika manunuzi wa mali au huduma katika idara ya serikali, shirika la umma au binafsi (Faini Tshs 15,000,000/= au kifungo cha miaka 7 au vyote kwa pamoja);

4) K/F 18 –Rushwa katika mikataba (faini Tshs 15m. au kifungo cha miaka 7 au vyote kwa pamoja);

5) K/F 20 –Rushwa katika ajira (Faini 5m. au kifungo cha miaka 3 au vyote kwa pamoja);

6) K/F 21 – kujihusisha na Rushwa kupitia mashirika ya kigeni (Faini 10M. au kifungo cha miaka 7 au vyote kwa pamoja)

7) K/F 22 –Kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya muajiri au kujipatia fedha kwa ufisadi (Faini 7m au kifungo cha miaka 5 au vyote kwa pamoja).

8) K/F 23 – Kujipatia faida au vitu vyovyote kutoka kwa mtu unayemshughulikia kikazi (mpokeaji ni mtoa maamuzi) [Faini 10m au kifungo miaka 7 au vyote kwa pamoja].

9) K/F 25 – Rushwa ya ngono (Faini 5m/kifungo cha miaka 3 au vyote kwa pamoja)

10) K/F 26(3) – Mtumishi wa umma kukataa kutoa maelezo au kutoa maelezo ya uongo kwa Afisa wa TAKUKURU kuhusiana na mali zake ni kosa la jinai (Faini 5m/kifungo cha miaka 3 au vyote kwa pamoja)

11) K/F 28 – Mtumishi wa umma au Taasisi binafsi anayefuja mali au kubadilisha umiliki wake na kuwa zake (faini 10m/kifungo cha miaka 2 au vyote kwa pamoja)

12) K/F 29 – Mtumishi wa umma anayebadilisha matumizi ya mali za umma/serikali kwa matumizi binafsi (Faini 2m/kifungo cha miaka 2 au vyote kwa pamoja)

13) K/F 30 – Mtu yeyote anayemsaidia mtu mwingine kutenda kosa la Rushwa kinyume cha sheria hii, naye pia atakuwa ametenda kosa la Rushwa (faini 2m/kifungo cha miaka 2 au vyote kwa pamoja)

14) K/F 31 – Mtu yeyote anayetumia vibaya mamlaka/madaraka aliyopewa na umma kwa manufaa yake binafsi au kwa manufaa ya mtu mwingine binafsi (Faini 5m/kifungo cha miaka 3 au vyote kwa pamoja)

15) K/F 32 – Kula njama kwa lengo la kula Rushwa.(Faini 5m/kifungo cha miaka 3 au vyote kwa pamoja)

16) K/F 33(1) – Kufanya ukuwadi wa mamlaka kwa mtu mwenye cheo au madaraka kwa lengo la kumpendelea mtu mwingine na yeye kujipatia faida fulani (Trading influence). (faini 3m/kifungo cha miaka 2 au vyote kwa pamoja)

17) K/F 33(2) – Mtu yeyote anayetumia kuwadi wa mamlaka kushawishi kwa mtu mwenye cheo au madaraka kwa lengo la kumpendelea ili kujipatia faida binafsi dhidi ya mtu mwingine naye pia atakuwa ametenda kosa la jinai. (faini 3m/kifungo cha miaka 2 au vyote kwa pamoja)

18) K/F 34(1) – Kubadilisha au kuhamisha au kuuza mali iliyopatikana kwa njia ya Rushwa.(Faini 10m/kifungo cha miaka 7 au vyote kwa pamoja)

19) K/F 34(2) – Kukaidi kutekeleza NOTISI ya mwanasheria ya
(3) - Kumzuia kubadili au kuuza au kuhamisha au
(4) - Kukubali kumiliki Mali iliyopatikana kwa rushwa
(Faini 10m/kifungo cha miaka 7 au vyote kwa pamoja)

20) K/F 36 – Kujitambulisha kama Afisa wa TAKUKURU wakati sio kweli.(Faini 2m/kifungo cha miaka 2 au vyote kwa pamoja)

21) K/F 37 – Kutoa siri ya uchunguzi bila idhini ya kufanya hivyo. (Faini 100,000/= au kifungo cha mwaka 1 au vyote kwa pamoja)

22) K/F 52(2) – Kumtishia mtu aliyetoa taarifa za kufanyika au kuwepo mpango wa kufanyika vitendo vya rushwa (Faini 500,000/= au kifungo cha mwaka 1 au vyote kwa pamoja)
 

Rwazi1

JF-Expert Member
May 3, 2013
662
500
K/F 25 – Rushwa ya ngono (Faini 5m/kifungo cha miaka 3 au vyote kwa pamoja)
Nafanya mbinu gan ili anayetaka kunihonga ngono akamatwe yeye.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom