Uchaguzi 2020 Makosa ya Lissu yanaweza kutumiwa na CCM kumzidi kete kisiasa

Kosa moja ambalo Lissu anafanya hivi sasa ni kuaccumulate makosa mengi ya kisiasa ambayo CCM wanaweza kuyatumia dhidi yake.

Tangu arudi nchini Lissu ameshafanya makosa kadha wa kadha ambayo asipokuwa makini na akaendelea kuyafanya yataanza kumpungunzia mtaji wa kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.

Makosa yenyewe ni yafuatayo

1. Hazungumzii kwa kirefu ana ajenda gani ya maendeleo kwa wananchi, kitu kimoja ambacho amekielezea kwa ufanisi sana ni kuhusu suala la katiba mpya na umuhimu wake, lakini Lissu anapwaya sana kwenye kuelezea Issues zinazohusu ugali mezani mwa wananchi, Lissu kwa mfano hawezi kuzungumza zaidi ya dakika moja kuhusu mkulima na kilimo chake, mfanyakazi wa umma na maslahi yake, Elimu na namna ya kuiboresha, wavuvi na uvuvi wao, Wamachinga, miundo mbinu, Lissu haarticulate vizuri hizo issues. Lissu hazungumzii Ufisadi kabisa na kwamba ana mpango gani wa kukomesha rushwa, ufisadi na plan ipi aliyokuwa nayo juu ya Taifa ili kunufaika na rasilimali zake

2. Pili Suala la kuponda hali ya COVID-19 nchini na kudai ipo sana na kulizungumza bila ushahidi wa Data, na kuongea kitu ambacho yeye binafsi hatekelezi, inamuexpose kama mwanasiasa msema chochote ilimradi kusema lakini hasimamii anachokisema. Tangu Lissu aje, ameonekana kwenye mikusanyiko ya watu wengi, ndani ya vikao vya chama, kwenye mapokezi yake n. k, huko kote hajaweka social distance wala kuvaa barakoa, iweje leo atwambie kwenye TV ya Kenya kuwa Tanzania kuna Korona nyingi na kuwataka watu wavae barakoa na kuweka social distance?. Kitu kimoja ambacho Lissu lazima akielewe ni kwamba Magufuli pamoja na kuhandle issue ya Korona kwa tofauti sana, amejitahidi sana kuspin situation nchini ilivyo kwa kuvurugavuruga channel rasmi za taarifa kiasi kwamba leo ni vigumu kujua hali halisi ya Korona nchini, hata hivyo kitu kimoja kilicho obvious ni kwamba Magufuli ana ratings kubwa ajabu miongoni mwa wananchi kwa jinsi alivyohandle issue hii ya Korona japo jinsi alivyoihsndle siyo kisayansi. Kwa hiyo Lissu wakati anaongea haya ajue anaongea na Watanzania wa namna gani, Wengi hawawezi kumuunga mkono unless aje na data zisizoweza kutiliwa shaka hata kidogo. Ila hii ya kupinga bila data inawafanya wananchi wamuondolee credibility

3. Issue ya Wimbo wa Taifa pia haikuwa sahihi Lissu kuitolea comment. Ilitakiwa chama chenyewe ndo kiseme. Kama tulivyokwishajadili humu, Kuna makosa ya Kisiasa na makosa ya kisheria. Issue ya Wimbo wa Taifa ni Issue ya Kisiasa na Kijamii. Siyo lazima kila kanuni iandikwe kwenye vitabu vya sheria. Wananchi wanauheshimu wimbo wao wa Taifa, wimbo huo kwao unasymbolize Taifa moja na kwa wananchi wimbo huo upo juu ya vikundi vya watu kama vile vyama vya siasa n. k. Sasa kitendo cha kutetea kubadili matumizi ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama ndani yake kunatuma meseji kuwa hawa watu ni wapenda fujo, wasiofuata taratitibu.
Utetezi kuwa mbona UVCCM nao waliimba tofauti hausaidii, maana wananchi wanajua kuwa uongozi wa Juu wa vyama ndiyo wenye kuwakilisha misimamo halisi ya vyama na siyo hao watoto wa UVCCM. Kwa hiyo inapotokea viongozi wa Chadema wanafanya makosa kama haya, halafu Lissu anatetea, inatuma meseji kuwa huyu ni. mpenda vurugu, moenda malumbano, kwa hiyo wanamshusha hadhi

Nina mapendekezo yafuatayo kwa Lissu na Chadema

1. Lissu anza kuzungumzia issues, ili watu waone una substance zilizoshiba zile zinazohusu ugali wa wananchi zaidi

2.Kwenye kipindi hiki kuelekea uchaguzi, CHADEMA lazima mcoordinate anachozungumza Lissu kwenye Vyombo vya habari, fahamuni kuna vyombo vitajaribu kumframe ili kuzungumza vitu ambavyo atatoa boko halafu vitumike kisiasa dhidi yake na Chadema ili kuwadiscredit mbele ya wananchi.

3. Lissu, kuwa confident kama ulivyo ila kuwa humble zaidi, wananchi hawapendi arrogance, overconfidence

4. Lissu una mtaji wa huruma ya wananchi, itumie hiyo vizuri kukusaidia kwenye kampeni, Fahamu kwamba kila aliyesikitika na tukio lililokufika ni potential voter wako. Kila aliyetoa senti yake kwako ni potential voter wako, na kila sliyekuombea dua ni potential voter wako. Lakini cha kufanya, ni kuhakikisha watu wanakuona katika positive light

5. Ndani ya Chadema najua chama kipo kwenye paralyisis namna gani ya kumuweka Lisu kwenye msitari, hakijajua kitamuwekaje sawa ili acheze katika mistari ya hulka za taswira ya rais. Sasa inabidi watafute namna ya kuliweka sawa hilo jambo

Kiufupi CCM walikuwa kwenye shock namna ya kuhandle umaarufu wa Lissu, ila inavyoonekana wameanza kutoboa matobo kidogokidogo katika haiba ya Lissu, Chadema na Lissu wawe makini na stratergy hii ya CCM.

Lissu kwenye hoja hasa za kisheria, haki za binadamu na katiba hakuna ndani ya CCM anayemuweza, ila wenzie ni wajuzi sana wa siasa, wanajua namna ya kumanipulate mtu wa chini kabisa hata kwa propaganda ili awaunge mkono. Kwa hiyo Lissu inabidi anyanyue zaidi game yake kuliko ilivyo sasa.
Safari hii kutakuwa na mitego ya kila aina. Mnataka aanze na sera zake sasa hivi halafu mje muweke pingamizi kwamba ameanza kampeni mapema kabla ya muda uliowekwa na tume ya uchaguzi?
 
Lissu ni Lissu jana, leo, kesho na milele na milele.

ni huu u Lissu wake ndiyo haswa uliomfikisha kwenye hatua hii ya hata kukubalika kuwa presidential material and candidate. don't change him into what he's NOT.

watu watamwelewa Lissu very soon. anahitaji no more than 30 days kuwasomesha Watanzania wakamwelewa.

in fact, Lissu is miles better off compared to JPM kwenye maeneo mengi na Lissu ndiye ana jeuri inayohitajika kupambana katika mfumo ambao CCM wanatumia zaidi nguvu ya dola kuliko hoja.

let's enjoy the Lissu we know.
let's enjoy his fierce battling against a tyrant.
let's enjoy the ride!!

Endeleeni kumpoteza.
 
tutamchagua kwa kuongoza juhudi za kumuondoa huyu mtesi wetu ccm ndani ya nchi yetu
Kalagabao

Kama uwezi kuuza sera zenye kueleweka na kuwa mkombozi wq wananchi,basi ondoa zana ya MBELEKO, kama unaona ccm ina petty issues basi ulete BIG issues bila hivyo asitegemee huruma ya wananchi.

Siasa ni uuzaji wa sera za uhakika,sio huruma za wapiga kura.
 
Mkuu ndo maana nikakuambia wewe ni utopolo wa level hiyo hiyo,the reasons why LGAs was established ilikuwa ni ili zishughulike na hizo petty issues zinazowagusa wananchi ili central government ibaki Ina deal na major issues,Sasa Kama saizi ya Magu ni hizo petty issues huko kwenye urais anatafuta nini?
Nmekuuliz ishu za Lisu ambae wewe unahisi ndio mbadala wa Magufuli ni zipi?
 
Huyu jamaa ni muongo muongo sana vile alivyotuambiaga kuwa miga watatunyoa kwa chupa aiseee sijawahi kumuamini tena kifupi ni msanii msanii fulani hivi.
 
Mkuu kwa miaka 60 uchumi wetu na maendeleo yetu ysmedumazwa na CCM,Sasa badala ya kuhangaika kuong'oa kisababishi Cha matatizo yetu ya kiuchumi ninyi mnataka ashughulike na petty issues kama Magu?yaani aanze kuhangaika na stend,masoko na kupokea watalii siyo?
Ishu kubwa kubwa za Lisu ni zipi?
 
Lissu na Magufuli ni mapacha wa nje wasiolewana,sema mmoja ana dola mwingine inaitafuta dola.

Tuombe Mungu mwenye Dola awe mvumilivu.
Na wamefana mengi usipokuwa Magufuli Sasa kajirekebisha Sana na anafata ushauri wa wataalamu wake kipindi hichi Cha kampeni. Na magufuli akiendelea na hii maturity atafanya la maana clashes zitaisha automatic
 
Kosa moja ambalo Lissu anafanya hivi sasa ni kuaccumulate makosa mengi ya kisiasa ambayo CCM wanaweza kuyatumia dhidi yake.

Tangu arudi nchini Lissu ameshafanya makosa kadha wa kadha ambayo asipokuwa makini na akaendelea kuyafanya yataanza kumpungunzia mtaji wa kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.

Makosa yenyewe ni yafuatayo

1. Hazungumzii kwa kirefu ana ajenda gani ya maendeleo kwa wananchi, kitu kimoja ambacho amekielezea kwa ufanisi sana ni kuhusu suala la katiba mpya na umuhimu wake, lakini Lissu anapwaya sana kwenye kuelezea Issues zinazohusu ugali mezani mwa wananchi, Lissu kwa mfano hawezi kuzungumza zaidi ya dakika moja kuhusu mkulima na kilimo chake, mfanyakazi wa umma na maslahi yake, Elimu na namna ya kuiboresha, wavuvi na uvuvi wao, Wamachinga, miundo mbinu, Lissu haarticulate vizuri hizo issues. Lissu hazungumzii Ufisadi kabisa na kwamba ana mpango gani wa kukomesha rushwa, ufisadi na plan ipi aliyokuwa nayo juu ya Taifa ili kunufaika na rasilimali zake

2. Pili Suala la kuponda hali ya COVID-19 nchini na kudai ipo sana na kulizungumza bila ushahidi wa Data, na kuongea kitu ambacho yeye binafsi hatekelezi, inamuexpose kama mwanasiasa msema chochote ilimradi kusema lakini hasimamii anachokisema. Tangu Lissu aje, ameonekana kwenye mikusanyiko ya watu wengi, ndani ya vikao vya chama, kwenye mapokezi yake n. k, huko kote hajaweka social distance wala kuvaa barakoa, iweje leo atwambie kwenye TV ya Kenya kuwa Tanzania kuna Korona nyingi na kuwataka watu wavae barakoa na kuweka social distance?. Kitu kimoja ambacho Lissu lazima akielewe ni kwamba Magufuli pamoja na kuhandle issue ya Korona kwa tofauti sana, amejitahidi sana kuspin situation nchini ilivyo kwa kuvurugavuruga channel rasmi za taarifa kiasi kwamba leo ni vigumu kujua hali halisi ya Korona nchini, hata hivyo kitu kimoja kilicho obvious ni kwamba Magufuli ana ratings kubwa ajabu miongoni mwa wananchi kwa jinsi alivyohandle issue hii ya Korona japo jinsi alivyoihsndle siyo kisayansi. Kwa hiyo Lissu wakati anaongea haya ajue anaongea na Watanzania wa namna gani, Wengi hawawezi kumuunga mkono unless aje na data zisizoweza kutiliwa shaka hata kidogo. Ila hii ya kupinga bila data inawafanya wananchi wamuondolee credibility

3. Issue ya Wimbo wa Taifa pia haikuwa sahihi Lissu kuitolea comment. Ilitakiwa chama chenyewe ndo kiseme. Kama tulivyokwishajadili humu, Kuna makosa ya Kisiasa na makosa ya kisheria. Issue ya Wimbo wa Taifa ni Issue ya Kisiasa na Kijamii. Siyo lazima kila kanuni iandikwe kwenye vitabu vya sheria. Wananchi wanauheshimu wimbo wao wa Taifa, wimbo huo kwao unasymbolize Taifa moja na kwa wananchi wimbo huo upo juu ya vikundi vya watu kama vile vyama vya siasa n. k. Sasa kitendo cha kutetea kubadili matumizi ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama ndani yake kunatuma meseji kuwa hawa watu ni wapenda fujo, wasiofuata taratitibu.
Utetezi kuwa mbona UVCCM nao waliimba tofauti hausaidii, maana wananchi wanajua kuwa uongozi wa Juu wa vyama ndiyo wenye kuwakilisha misimamo halisi ya vyama na siyo hao watoto wa UVCCM. Kwa hiyo inapotokea viongozi wa Chadema wanafanya makosa kama haya, halafu Lissu anatetea, inatuma meseji kuwa huyu ni. mpenda vurugu, moenda malumbano, kwa hiyo wanamshusha hadhi

Nina mapendekezo yafuatayo kwa Lissu na Chadema

1. Lissu anza kuzungumzia issues, ili watu waone una substance zilizoshiba zile zinazohusu ugali wa wananchi zaidi

2.Kwenye kipindi hiki kuelekea uchaguzi, CHADEMA lazima mcoordinate anachozungumza Lissu kwenye Vyombo vya habari, fahamuni kuna vyombo vitajaribu kumframe ili kuzungumza vitu ambavyo atatoa boko halafu vitumike kisiasa dhidi yake na Chadema ili kuwadiscredit mbele ya wananchi.

3. Lissu, kuwa confident kama ulivyo ila kuwa humble zaidi, wananchi hawapendi arrogance, overconfidence

4. Lissu una mtaji wa huruma ya wananchi, itumie hiyo vizuri kukusaidia kwenye kampeni, Fahamu kwamba kila aliyesikitika na tukio lililokufika ni potential voter wako. Kila aliyetoa senti yake kwako ni potential voter wako, na kila sliyekuombea dua ni potential voter wako. Lakini cha kufanya, ni kuhakikisha watu wanakuona katika positive light

5. Ndani ya Chadema najua chama kipo kwenye paralyisis namna gani ya kumuweka Lisu kwenye msitari, hakijajua kitamuwekaje sawa ili acheze katika mistari ya hulka za taswira ya rais. Sasa inabidi watafute namna ya kuliweka sawa hilo jambo

Kiufupi CCM walikuwa kwenye shock namna ya kuhandle umaarufu wa Lissu, ila inavyoonekana wameanza kutoboa matobo kidogokidogo katika haiba ya Lissu, Chadema na Lissu wawe makini na stratergy hii ya CCM.

Lissu kwenye hoja hasa za kisheria, haki za binadamu na katiba hakuna ndani ya CCM anayemuweza, ila wenzie ni wajuzi sana wa siasa, wanajua namna ya kumanipulate mtu wa chini kabisa hata kwa propaganda ili awaunge mkono. Kwa hiyo Lissu inabidi anyanyue zaidi game yake kuliko ilivyo sasa.
Uwe na subra ,muda wa kampeni bado
 
Mkuu pole wewe na huyu anaeongelea petty issues mpo level moja,rais kuongelea vitu vidogo vidogo Kama stend na majengo ya masoko na hadi unaobwa bumu yanawekana tu kwa watu wenye uwezo mdogo otherwise nchi hii Ina Mambo mengi makubwa ya kufanywa na rais wakati hayo ya masoko na stend yakifanywa na wakurugenzi

Wewe mtumiaji wa airport hupigi kura, watumiaji wa stendi ndiyo wapiga kura na jinsi ya kuwapata na kuteka hisia zao ni kuongelea stendi yao, nyavu zao, majembe yao, visima vya maji, Bodaboda zao, mashamba yao n.k. Kwa mwenendo huu, Haki ya nani JPM atashinda kwa kishindo cha zaidi ya 80%
 
Nmekuuliz ishu za Lisu ambae wewe unahisi ndio mbadala wa Magufuli ni zipi?
1.kuitoa Ccm madarakani_ kwangu hii ni kubwa maana itafungua Mambo mengi na kuspeed up maendeleo ya nchi yetu na watu wake
2. Katiba mpya_ systems ni muhimu kwa maendeleo ya nchi kuliko matamko na kutembea na mabunda barabarani
3. International relationships na nchi nyingine- kufungua fursa za watanzania kwenye import and exports,kufanya kazi nje ya Tanzania etc
 
Yawezekana pia nje ya field yake hana alijualo!

Yawezekana hata kwenye taaluma yake tunaamini yupo sawa kwa vile wengi ni laymen tu ila anachemka vilevile.

Kwenye kila achoongea nje ya taaluma yake anaonesha he's not well informed mf anajua hakuna jogoo wa laki moja😁! Wakati viwanja vya sabasaba walikuwepo kuchi jogoo wa laki tano.

Ushauri: He's to say less than necessary!

"Powerful people impress and intimidate by saying less.

The more you say, the more likely you're to say something foolish"
 
Wewe mtumiaji wa airport hupigi kura, watumiaji wa stendi ndiyo wapiga kura na jinsi ya kuwapata na kuteka hisia zao ni kuongelea stendi yao, nyavu zao, majembe yao, visima vya maji, Bodaboda zao, mashamba yao n.k. Kwa mwenendo huu, Haki ya nani JPM atashinda kwa kishindo cha zaidi ya 80%
Hizo si issues za kuongelewa na rais,JK na BWM hawakuwahi ongelea hizi petty issues na still walipata kura,acheni utopolo Bwana
 
I second your point,uelewa na utendaji wa Magu vyote vipo below average ndo maana unamuona anahangaika na petty issues_ yaani rais unasimama mbele za watu unaanza kuonesha masoko na stend? Shame on him

..mimi nimeshangaa Jpm eti anasema wapinzani watabomoa madaraja na kuuza scraper, na meli zote zitapigwa mnada!!

..Shame on him!!
 
Kachanganyikiwa,mtu mwenye hadhi ya urais huwezi ongea utopolo wa aina ile
 
Naona watu wamekuwa mafundi wa kumshauri Lissu wakiogopa asikosee lakini sioni wakimshauri magombea wa CCM ambaye kwa hulka akiamua kupaisha anapaisha kweli.

Mgombea wa CCM ana rungu la dola mkononi, hilo ndo linampa jeuri ya kuharibu kisha likmsafisha. Sasa wapinzani hawana hiyo ndiyo maana inabodi waplay smarter
 
Hii ishu ya corona alioiongelea leo Lissu, CCM wakiitumia vizuri nikiboko kitamu sana kwa wamachinga na bodaboda.
Hakuna kitu Kama hicho.
Hii ishu itammaliza Magu zaidi kuliko unavyofikiria.
Lupima mapapi ,kutangaza korona imekwisha wakati Hakuna vipimo kuthibitisha Hilo Hilo Ni janga.
Umejuaje Kama korona imekwisha wakati huaminishwa vipimo?
Watu wako kimya tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom