Uchaguzi 2020 Makosa ya Lissu yanaweza kutumiwa na CCM kumzidi kete kisiasa

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,270
2,000
Kosa moja ambalo Lissu anafanya hivi sasa ni kuaccumulate makosa mengi ya kisiasa ambayo CCM wanaweza kuyatumia dhidi yake. Tangu arudi nchini Lissu ameshafanya makosa kadha wa kadha ambayo asipokuwa makini na akaendelea kuyafanya yataanza kumpungunzia mtaji wa kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.

Makosa yenyewe ni yafuatayo

1. Hazungumzii kwa kirefu ana ajenda gani ya maendeleo kwa wananchi, kitu kimoja ambacho amekielezea kwa ufanisi sana ni kuhusu suala la katiba mpya na umuhimu wake, lakini Lissu anapwaya sana kwenye kuelezea Issues zinazohusu ugali mezani mwa wananchi, Lissu kwa mfano hawezi kuzungumza zaidi ya dakika moja kuhusu mkulima na kilimo chake, mfanyakazi wa umma na maslahi yake, Elimu na namna ya kuiboresha, wavuvi na uvuvi wao, Wamachinga, miundo mbinu, Lissu haarticulate vizuri hizo issues. Lissu hazungumzii Ufisadi kabisa na kwamba ana mpango gani wa kukomesha rushwa, ufisadi na plan ipi aliyokuwa nayo juu ya Taifa ili kunufaika na rasilimali zake

2. Pili Suala la kuponda hali ya COVID-19 nchini na kudai ipo sana na kulizungumza bila ushahidi wa Data, na kuongea kitu ambacho yeye binafsi hatekelezi, inamuexpose kama mwanasiasa msema chochote ilimradi kusema lakini hasimamii anachokisema. Tangu Lissu aje, ameonekana kwenye mikusanyiko ya watu wengi, ndani ya vikao vya chama, kwenye mapokezi yake n. k, huko kote hajaweka social distance wala kuvaa barakoa, iweje leo atwambie kwenye TV ya Kenya kuwa Tanzania kuna Korona nyingi na kuwataka watu wavae barakoa na kuweka social distance?.

Kitu kimoja ambacho Lissu lazima akielewe ni kwamba Magufuli pamoja na kuhandle issue ya Korona kwa tofauti sana, amejitahidi sana kuspin situation nchini ilivyo kwa kuvurugavuruga channel rasmi za taarifa kiasi kwamba leo ni vigumu kujua hali halisi ya Korona nchini, hata hivyo kitu kimoja kilicho obvious ni kwamba Magufuli ana ratings kubwa ajabu miongoni mwa wananchi kwa jinsi alivyohandle issue hii ya Korona japo jinsi alivyoihsndle siyo kisayansi.

Kwa hiyo Lissu wakati anaongea haya ajue anaongea na Watanzania wa namna gani, Wengi hawawezi kumuunga mkono unless aje na data zisizoweza kutiliwa shaka hata kidogo. Ila hii ya kupinga bila data inawafanya wananchi wamuondolee credibility

3. Issue ya Wimbo wa Taifa pia haikuwa sahihi Lissu kuitolea comment. Ilitakiwa chama chenyewe ndo kiseme. Kama tulivyokwishajadili humu, Kuna makosa ya Kisiasa na makosa ya kisheria. Issue ya Wimbo wa Taifa ni Issue ya Kisiasa na Kijamii. Siyo lazima kila kanuni iandikwe kwenye vitabu vya sheria. Wananchi wanauheshimu wimbo wao wa Taifa, wimbo huo kwao unasymbolize Taifa moja na kwa wananchi wimbo huo upo juu ya vikundi vya watu kama vile vyama vya siasa n. k. Sasa kitendo cha kutetea kubadili matumizi ya wimbo wa Taifa na kuweka uvyama ndani yake kunatuma meseji kuwa hawa watu ni wapenda fujo, wasiofuata taratitibu.

Utetezi kuwa mbona UVCCM nao waliimba tofauti hausaidii, maana wananchi wanajua kuwa uongozi wa Juu wa vyama ndiyo wenye kuwakilisha misimamo halisi ya vyama na siyo hao watoto wa UVCCM. Kwa hiyo inapotokea viongozi wa Chadema wanafanya makosa kama haya, halafu Lissu anatetea, inatuma meseji kuwa huyu ni. mpenda vurugu, moenda malumbano, kwa hiyo wanamshusha hadhi

Nina mapendekezo yafuatayo kwa Lissu na Chadema


1. Lissu anza kuzungumzia issues, ili watu waone una substance zilizoshiba zile zinazohusu ugali wa wananchi zaidi

2.Kwenye kipindi hiki kuelekea uchaguzi, CHADEMA lazima mcoordinate anachozungumza Lissu kwenye Vyombo vya habari, fahamuni kuna vyombo vitajaribu kumframe ili kuzungumza vitu ambavyo atatoa boko halafu vitumike kisiasa dhidi yake na Chadema ili kuwadiscredit mbele ya wananchi.

3. Lissu, kuwa confident kama ulivyo ila kuwa humble zaidi, wananchi hawapendi arrogance, overconfidence

4. Lissu una mtaji wa huruma ya wananchi, itumie hiyo vizuri kukusaidia kwenye kampeni, Fahamu kwamba kila aliyesikitika na tukio lililokufika ni potential voter wako. Kila aliyetoa senti yake kwako ni potential voter wako, na kila sliyekuombea dua ni potential voter wako. Lakini cha kufanya, ni kuhakikisha watu wanakuona katika positive light

5. Ndani ya Chadema najua chama kipo kwenye paralyisis namna gani ya kumuweka Lisu kwenye msitari, hakijajua kitamuwekaje sawa ili acheze katika mistari ya hulka za taswira ya rais. Sasa inabidi watafute namna ya kuliweka sawa hilo jambo

Kiufupi CCM walikuwa kwenye shock namna ya kuhandle umaarufu wa Lissu, ila inavyoonekana wameanza kutoboa matobo kidogokidogo katika haiba ya Lissu, Chadema na Lissu wawe makini na stratergy hii ya CCM.

Lissu kwenye hoja hasa za kisheria, haki za binadamu na katiba hakuna ndani ya CCM anayemuweza, ila wenzie ni wajuzi sana wa siasa, wanajua namna ya kumanipulate mtu wa chini kabisa hata kwa propaganda ili awaunge mkono. Kwa hiyo Lissu inabidi anyanyue zaidi game yake kuliko ilivyo sasa.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,405
2,000
JamiiForums kuna nawazo mzuri sana kwa wanasiasa.

Hata hivyo,tatizo mojawapo ni kuwa,media hazitoa uzito katika kuripoti issue zingine anazozungumzia Lissu na mfano mzuri ni issue ya TRA na kodi kwa wafanyabiashara ambayo aliiongelea hivi karibuni.

Lissu pia majuzi ameongelea maswala ya wafanyakazi na ubora wa elimu yetu ila mitandaoni na kwenye media haya hayaripotiwa/hayaandikwa sana.

Issu nyingine ni wanaomuhoji nao wanachangia kumfanya kila wakati aongelee issue ya yeye kushambuliwa na maswala ya utawala wa Bora.

Lissu kwa sasa anatakiwa awe makini na wanaomuhoji na asikubali wamuelekeze kwenye hoja hizi za kila siku ambazo ameshazisema sana.

Lissu sasa atumie muda mwingi kuelezea matatizo yanayogusa wananchi moja kwa moja kama vile mishahara duni ya wafanyakazi, makato katili ya Bodi ya Mikopo,matatizo ya mafao kwa kastaafu, kero za maji,mfumuko wa bei ,mfano tatizo la bei ya sukari, watu kutekwa,PAYE kwa wafanyakazi,pembejeo kwa wakulima,n.k

Tatizo lingine ni kukosekana watu wa kuandika na kusambaza hotuba za Lissu mitandaoni na badala yake wanasamba zaidi clips na tweet za anayoyasema hivyo watu wanashindwa kupata hotuba zake kwa ukamilifu.

Athari za kutoipata hotuba kwa ukamilifu, ni watu wa propaganda wa chama fulani kuchukua sehemu fulani tu za hotuba kwa lengo la kupotosha huku wakiacha kwa makusudi sehemu ya hotuba inayoweza kujibu propaganda waliyoitengeneza kwa kutumia hotuba hiyo(wanachukua vipande tu wanavyoweza kuvifanyia propaganda)

Clips kusikiliza ni gharama, hivyo wengi kushindwa kusikiliza hotuba zake kwa kirefu kupitia mitandaoni.

Kampeni zikianza, tunaomba CHADEMA mzingatie huu ushauri.
 

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,540
2,000
Mimi binafsi naamini ukiiondoa CCM madarakani,utakuwa umesolve kila tatizo linalowakabiri watanzania,the only problem ninayoiona watanzania wengi tumeadhiriwa na viongozi uchwara aina ya kina Magu wanaoongelea petty issues kila Mara,Sasa Kama rais anaongelea masoko na stend, anaongelea vibarabara vya halmashauri,anaongelea vizahanati badala ya kuongelea national health systems ,Kuna nini tena hapo?
 

QUIGLEY

JF-Expert Member
May 23, 2015
27,680
2,000
Lisu asikilize wapiga kura na washauri wenye nia nzuri atashinda. Ushauri mzuri
Nimukuelewa kaka
Nikikutana na lissu nitamwambia
JamiiForums kuna nawazo mzuri sana kwa wanasiasa.

Tatizo mojawapo ni kuwa,media hazitoa uzito katika kuripoti issue zingine anazozungumzia Lissu na mfano mzuri ni issue ya TRA na kodi kwa wafanyabiashara.

Lissu pia ameongelea masala ya wafanyakazi na ubora wa walimu yetu ila mitandaoni na kwenye media haya hayaripotiwa/hayaandikwa sana.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,270
2,000
Mimi binafsi naamini ukiiondoa ccm madarakani,utakuwa umesolve kila tatizo linalowakabiri watanzania,the only problem ninaloliona watanzania wengi tumeadhiriwa na viongozi uchwara aina ya kina Magu wanaongelea petty issues kila Mara,Sasa Kama rais anaondelea masoko na stend, anaongelea vibarabara vya halmashauri,anaongelea vizahanati badala ya kuongelea national health systems ,Kuna nini tena hapo?
Yes, Magufuli hana achievements zozote za maana ndiyo maana anazungumzia habari ndogo ndogo
Enzi za JK ilikuwa ni nadra sana kumsikia akizungumzia masoko na stendi japo awamu yake ilijenga hivyo vitu kwa wingi ajabu, hata hivyo vitu hivyo vilikuwa kwenye hadhi ya halmashauri huko, siyo Ikulu
 

dndagula

Senior Member
Jul 24, 2016
142
250
Lissu anazungumza kama mwanaharakati na kimapambano zaidi siyo kama mwanasiasa makini kuelekea kipindi cha kampeni. Hii ni sawa ns mechi ya mpira kosa moja linakugarimu He must be carefully with the game being more crafty vinginevyo atapata shida na kuwa hafifu kati ya viongozi wote wangombea hususani anaposema yeye anapambana na mfumo tu bila kueleza kwa watu wa kawaida anajipya lipi la mkate wa wanyonge na raslimali zao. Huyu ataonekana kituko hizi ni siasa za kampeni tunataka hoja tena za kisera na mashiko vinginevyo anasindikiza mechi. Kwanza mimi hapati kura yangu mpaka ajibu tuhuma ya kutumwa na mabeberu kuiuza nchi kwao.
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
11,723
2,000
Lissu ni Lissu jana, leo, kesho na milele na milele.

ni huu u Lissu wake ndiyo haswa uliomfikisha kwenye hatua hii ya hata kukubalika kuwa presidential material and candidate. don't change him into what he's NOT.

watu watamwelewa Lissu very soon. anahitaji no more than 30 days kuwasomesha Watanzania wakamwelewa.

in fact, Lissu is miles better off compared to JPM kwenye maeneo mengi tu na Lissu ndiye ana jeuri inayohitajika kupambana katika mfumo ambao CCM wanatumia zaidi nguvu ya dola kuliko hoja.

let's enjoy the Lissu we know.
let's enjoy his fierce battling against a tyrant.
let's enjoy the ride!!
 

4 7mbatizaji

JF-Expert Member
Dec 8, 2019
638
1,000
Lissu mkuu huu ni mtego wanataka uanze zungumzia mambo ya ilani wakuwekee pingamizi kwamba umeanza kupiga kampeni mapema nakushauri usidhubutu hata kidogo maana kunadi ilani za vyama ni kwenye majukwaa na mda bado ukifika mda wake ndo uweke ngoma uwanjani kwa sasa zungumza mambo mengine maana zipo siku 60 za kunadi ilani za vyama na mda bado wala kipindi hiki kabla ya tarehe usika ya kufungua kampen usidhubutu na najua walitambua hilo watu sio wazuri wanakutafuta uingie kwenye kumi na nane wakupige pingamizi
 

Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,540
2,000
Lissu ni Lissu jana, leo, kesho na milele na milele.

ni huu u Lissu wake ndiyo haswa uliomfikisha kwenye hatua hii ya hata kukubalika kuwa presidential material and candidate. don't change him into what he's NOT.

watu watamwelewa Lissu very soon. anahitaji no more than 30 days kuwasomesha Watanzania wakamwelewa.

in fact, Lissu is miles better off compared to JPM kwenye maeneo mengi na Lissu ndiye ana jeuri inayohitajika kupambana katika mfumo ambao CCM wanatumia zaidi nguvu ya dola kuliko hoja.

let's enjoy the Lissu we know.
let's enjoy his fierce battling against a tyrant.
let's enjoy the ride!!
I second your point,uelewa na utendaji wa Magu vyote vipo below average ndo maana unamuona anahangaika na petty issues_ yaani rais unasimama mbele za watu unaanza kuonesha masoko na stend? Shame on him
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
11,723
2,000
I second your point,uelewa na utendaji wa Magu vyote vipo below average ndo maana unamuona anahangaika na petty issues_ yaani rais inasimama mbele za watu unaanza kuonesha masoko na stend? Shame on him
absolutely!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom