Makosa na Msamaha katika mapenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makosa na Msamaha katika mapenzi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 16, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 16, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Katika mapenzi watu hukoseana na wakati mwingine hata kuchukizana na kukasirikiana. Na kuna wakati makosa hayo huzaa hadi vurugu na hata kusababisha matumizi ya nguvu (violence) na katika matukio mengine makosa hayo hufikia kukatishia maisha.

  Makosa yapo mengi kuanzia madogomadogo kama mtu kuwa msahaulifu, kufanya kitu ambacho kinasababisha usumbufu n.k na yapo makosa makubwa kama kwenda nje ya mahusiano na kuzaa nje ya ndoa..

  Makosa hayo yote huita mwitikio kwa pande zote mbili, kuna mwitikio wa uchungu, kisasi, hasira, wivu na hata kinyongo cha muda mrefu. Na wakati mwingine haya yote yanadumu siku baada ya siku, mwezi baada ya mwezi na hata miaka. Hivyo makosa haya ya mapenzi yanaweza kusababisha madhara ya kihisia, kisaikolojia na hata kimaumbile kwa yule ambaye amakutwa nayo.

  Na kutokana na hayo kuna mambo ambayo watu hufikia mahali na kusema kuwa makosa fulani hayasameheki na kuwa mtu wake akifanya kosa x basi hawezi kumsamehe kamwe..

  (itaendelea)...
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Approach ni ishu sana katika mlolongo mzima wa mkosaji katika kuomba msamaha.

  Mimi nasema hakuna kosa lisilosameheka...Mbona ni watu kibao mtaani tunawajua wanawasamehe wake/waume zao kwa makosa ambayo wengine walishaapa kwamba hawatasamehe?
  Inategemeana na mtenda na mtendwa pamoja, mioyo yao ikoje.

  Kosa moja linamuudhi mtu x kidogo tu, na anasamehe, wakati kosa hilohilo linamgharimu mtu y kutoa talaka au kutoa uhai wa mkosaji.

  Tunatofautiana sana katika kuhimili uvumilivu na subira pindi tukosewapo!
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Ukipata mwanamke asie samehe
  utajuta kumfaham......
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Na mwanaume je?
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Ukimpata mwanaume asiyesamehe na mwenye visirani utajuuuuuuuuuta kwa nini ulisema yes I do !
   
 6. Sydney

  Sydney Senior Member

  #6
  Mar 17, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wapendwa mimi nadhani mwanaume siku zote ndio huwa mgumu sana kusamehe, yaani anaumia rohoni na kutamani hata kutoa roho ya mtu, Mimi nafahamu wanandoa fulani kabla ya kuoana past ya mwanamke ilikuwa chafu kidogo, lakini hakumwambia mwenzie pengine kwa kuhofoa kutemwa labda kwakuwa alimpenda sana, lakini hadi wasiochelewa na wenye visa na mkewe wakaanza kumsemea kwa mumewe, mume hadi leo hajasamehe kwa kile anachokiita ati mkewe hakuwa mkweli kwake, na tayari wana miaka minne ya ndoa yao kwa sasa na watoto. Lakini mwanamke kuna wakati aligundua uhusiano wa mumewe na msichana wa zamani kabla ya wao kuwa kitu kimoja, mume aliomba kusamehewa na alisamehewa, ingawa si kwa urahisi lakini ALISAMEHEWA, lakini hiki cha sasa cha huyu bibie,.. mume anashindwa kusamehe, ndoa imekuwa ndoano, sijui wataishia wapi. Point yangu ni kuwa mwanaume siku zote ni mgumu sana katika kusamehe!
   
 7. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwenye swala la kuombwa msamaha au kuomba, inategemea ni nani anakuomba msamaha hapo hatuangalii ni kosa gani, tunaangalia anayeomba, unaweza kukuta ni mtu wako wa maana sana amekukosea kumkosa hutaki na unaamini ankupenda ameteleza tu kumsamehe ni rahisi. Ila inatofautiana kwa mtu na mtu
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Pamoja na ugumu wa kusamehe, ili tuishi maisha yasiyo na presha, ni lazima tujifunze kusamehe. Hakuna jinsi maana sisi kama binadamu hatuwezi kuacha kukosa. Imagine, itabidi uamue kusihi na malaika kama hutataka kusamehe
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hawa ndo wabaya zaidi.....
  kila wakati reference kwenye lile kosa basi maisha yanakuwa magumu kupindukia na mwisho wa siku unaweza kubwaga manyanga kuepusha mengi zaidi

  ngumu sana kuwa na mwanume mwenye gubu/mwanamke mwenye gubu
  kama umeamua kusamehe samehe yaishe sio leo umesamehe na kesho unaanza ku-refer ulokwisha sema umesamehe......
   
 10. bht

  bht JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  furaha ya kusamehe ni kubwa mno kuliko hata ya kuombwa msamaha....

  ukikaa ni kinyongo moyo huwa mzito mno na daima hutapata furaha tofauti na unaposamehe.....
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mimi nashida na kimaumbile kivipi mtu anaweza kuathirika kimaumbile,unamaanisha kwa kupigwa?
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hapana yaani kutokana na kutokusamehe mwili utaanza kuonesha udhaifu na hata magonjwa mbalimbali yanaweza kuukumba. Kwa sababu kuna uhusiano usiotenganishwa kati ya afya ya akili (mental health) na afya ya mwili (physical health)..
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Mar 20, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nashukuru.Mwandishi wewe,Dakatari wewe,Mwanasaikolojia wewe.Haya hongera bwana.
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Kusamehe kunahitaji Moyo mkubwa na pia kuomba radhi nako kunahitaji mtu msyaarabu.

  Kimsingi ustaaarabu na kuheshimiana ndiko kwenye kuleta suluhu,suluhu huleta maridhiano na hayo ndiyo yatakayozaa msamaha
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,670
  Likes Received: 82,493
  Trophy Points: 280
  Na ukimpata ambaye anayesamehe utafurahi sana kumfahamu.
   
Loading...