Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,273
MAKOSA MAKUBWA YA MSWADA WA TISS.
SEHEMU YA 2.
Baada ya kuona makosa ya vifungu vya 5 na 16 namna vinavyopingana, na mapendekezo niliyoweka ili kuboresha mswada huu wa sheria ya Usalama wa Taifa Tanzania.
Sasa naomba leo tuchambue vifungu vingine ambavyo vina utata vikichwa vipite kama vilivyo itakuwa hatari kwa nchi. Mswada unasema, Kufuatia mabadiliko ya jumla yanayoweka usimamizi wa Idara chini ya Rais, inapendekezwa vifungu vya 11, 15, 18, 19(3) virekebishwe ili kuondoa mamlaka ya usimamizi wa Waziri wa Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa intelijensia na usalama.
Marekebisho haya ni hatari, Afrika na dunia ya leo y utandawazi ukimwacha mtu mmoja aamue na kudhibiti Sekta nyeti kama ya Ujasusi pekee yake ni hatari kwake binafsi na ni hatari kwa taifa. Hii ni room inayoweza kuipa TISS kumpindua Rais, hasa ikizingatiwa kuna kifungu cha 16 kinachoficha utambulisho wa Afisa wa TISS. Pili, afisa huyu ana kinga ya kisheria ya kutoshitakiwa kijinai kwamjibu wa kifungu cha 19 cha mswada huuhuu. Huu ni mtego mbaya kwa nafasi ya Rais, Vyombo hivi vinaongozwa na watu ambao wanatoka katika jamii zetu hizihizi na wanahisia hizihizi za kutaka madaraka. Sasa Rais anabebeshwa pekee yake uamuzi na udhibiti wa ida, ni hatari, iko siku tutapata Rais ambae sio Samia, atatumia meno haya kuangamiza taifa.
Mapendekezo yangu, vifungu vya 11, 15, 18, 19(3) virekebishwe Mamlaka yote ya TISS yawe chini ya Rais, lakini atasaidiwa/atashauriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mashauri ya Kigeni. Kwasababu ya hoja zifuatazo, Mswada huu haujawa katika mtazamo wa kiuchumi kama tulivyokuwa tukishauri, badala yake mabadiliko yanalenga udola zaidi. Hivyo Waziri wa Fedha na Mipango ataingia katika usimamizi wa Idara kama sehemu ya Sera mpa ya TISS ya kuongoza njia za uchumi wa nchi katika mtandao wa kifedha na uwekezaji, Ikizingatiwa tayari kuna kitengo cha Ujasusi wa kiuchumi kilichoundwa mwaka juzi pale Bank, Miradi ya uwekezaji wa ndani na nje yote ikiwemo sera ya uwekezaji na fedha viwe chini ya Waziri kwa mwamvuli wa TISS.
Waziri wa Sheria na Katiba anaingia kwaajili ya usimamizi wa sheria na katiba wakati wote wa uendeshaji na Oparesheni za TISS, atakuwa pia mshauri wa Rais katika mambo ya sheria na katiba. Waziri wa Mambo ya nje anaingia kwaajili ya maswala yote ya kijasusi nje ya mipaka ya nchi, na hasa katika diplomasia ya kimataifa na uwekezaji wa kigeni.
Hapo vifungu hivi vya mamlaka ya usimamizi wa TISS chini ya Rais vitakuwa vimetumia. NB: huko nyuma Mawaziri tajwa waliokuwa wanatambuliwa na sheria iliyopo walikuwa wapo kama kivuli tu, Kila kitu cha TISS iliamliwa na Rais, hata mswada huu umesema wazi kuwa wanarasmisha ule utaratibu wa awali ambao haukuwa rasmi. Kama Rais anamchagua Waziri Mkuu kwakushauriana na Makamu wa Rais, iweje jambo nyeti kama TISS Rais anapewa mamlaka ya pekee yake? Tukatae hili kwa nguvu zote!
Sehemu nyingine yenye utata ambayo inahitaji ifanyiwe marekebisho ya laazima ni kifungu cha 19 cha Mswaada huu kinachotoa kinga ya kijinai kwa maafisa wote wanapofanya uhalifu wawapo kazini. Hiki kifungu kina hatari nyingi sana, Lakini kuwa zaidi kina hatari kwa Umma, madhara ya utekaji wa raia na mauaji ya raia kwa miaka mitano iliyopita shutuma zote zilielekezwa kwa Idara ya Usalama wa Taifa kupitia genge lililoitwa watu wasiojulikana. Uhatari wa pili unahusu Mamlaka ya Rais kuwa hatarini ikiwa taasisi nzima maafisa wote wana kinga ya kijinai inatoa room ya kumpindua Rais kwa mwamvuli wa kinga hii. Ninafahamu, Mswada huu wa sheria ya Usalama wa Taifa ulianza kutungwa kipindi cha Magufuli 2019, nilidokezwa, Ulitungwa kwakuangalia mazingira ya wakati ule, na ulilenga dhana ya umagufulication, Rais Samia kaja kufanya maboresho kidogo tu, Rais Samia stuka, unabebeshwa dude hatari kwa usalama wako na wa nchi kwa ujumla. Rekebisheni
Duniani kote maafisa na wakuu wa idara nyeti kama ya Ujasusi huwa hawapewi kinga hata chembe, ili iwe rahisi kuwadhibiti kisheria pale wanapovuka mipaka yao ya kazi. Ndio maana unaweza kuona Mkurugenzi wa CIA au Mosad anafika mbele ya mahakamu kujibu tuhuma kadhaa zilizotokea katika utendaji wao. Ni juzi tu maafisa wa shirika la Ujasusi la Urusi walifikishwa katika mahakama moja mjini Moscow kwa makosa kadhaa ya usaliti katika vita huko Ukraine.
Mapendekezo yangu, Kinga kwa maofisa wa TISS iondolewe, badala yake kingi iwekwe kwenye kazi/Oparesheni na taarifa tu. Afisa kama mtu ashitakiwe tu kwamjibu wa taratibu za kijeshi kwakuwa tayari sheria kifungu cha kwanza kabisa kimeitambua TISS kama jeshi hivyo utaratibu wa kinidhamu wa Mahakama za kijeshi utumike kama kawaida.
Ikiwa kuna ulazima ambapo Kimsingi unajionyesha ni wa kisiasa zaidi kama ule aliopewa Spika, Jaji Mkuu nk, Basi kinga apewe Miurugenzi wa Usalama pekee na sio maafisa wote katika idara.
Kwa leo tuishie vifungu hivi... Tutaendelea wakati ujao
Na Yericko Nyerere