Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa unaoifanya iwe chini ya Usimamizi wa Rais watua Bungeni

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Kupitia Bunge la 12 linaloendelea Jijini Dodoma, Serikali imepeleka Bungeni Muswada unaopendeleza Mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa.

Pamoja na Mambo mengine, Sheria inapendekezwa kufanyiwa marekebisho katika kifungu cha 13 ili kuweka utaratibu wa kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu, Naibu Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi na Maafisa wa Idara.

Inapendekezwa kifungu cha 16 kifanyiwe marekebisho ili kuzuia ufichuaji wa utambulisho wa watu wanaofanya kazi katika Idara au watu wengine wanaoshirikiana na Idara na kumpa Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya udhibiti wa watu hao. Lengo la marekebisho ni kuwalinda maafisa na watu hao kutokana na utendaii wao wa kazi za kiusalama.

Kifungu cha 19 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza kinga ya makosa ya jinai kwa Maafisa wa Idara tofauti na ilivyo sasa ambapo kinga imetolewa katika mashauri ya madai pekee dhidi ya Maafisa hao.

Lengo la marekebisho ni kuweka kinga dhidi ya makosa yanayoweza kutendeka wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa uaminifu.

Vifungu vya 16(3), 17(3), 20(2) na 23 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza viwango vya adhabu kwa makosa mbalimbali kutegemeana na uzito wa kosa. Lengo la marekebisho hayo ni kuhakikisha viwango hivyo vya adhabu vinaendana na mazingira ya sasa.

Muswada unapendekezwa kuongeza vifungu vipya vya 24, 25 na 26 vitakavyoweka masharti mbalimbali ikiwemo, udhibiti wa Maafisa kutoa taarifa pindi wanapostaafu au kumaliza vipindi vya ajira, kuzuia uingiaji katika maeneo ya Idara bila idhini na masharti kuhusu vitendo vya uvunjifu wa Sheria nje ya mipaka ya Nchi.

Inapendekezwa Jedwali lifanyiwe marekebisho kwa kuongeza kiapo cha Utii pamoja na kurekebisha kiapo cha utumishi na kiapo cha kutunza siri kwa lengo la kumarisha ulinzi wa taarifa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Idara.

Pia soma: Katavi: Tundu Lissu apinga Muswada wa Sheria ya Usalama wa Taifa kuwasilishwa bungeni, adai utaleta Ukiritimba

==========

ZAIDI (Kutoka kwenye nyaraka)

Muswada huu unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa, Sura ya 406. Lengo la marekebisho yanayopendekezwa ni kubadili masharti ya Sheria kuendana na mfumo wa utawala uliopo na taratibu za usimamizi wa Idara za Usalama kimataifa na kuweka masharti mbalimbali ya utekelezaji bora wa majukumu ya Idara.

Marekebisho yanakusudia kuboresha Sheria na kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake.

Muswada umegawanyika katika Sehemu Mbili. Sehemu ya Kwanza inahusu masharti ya awali ambayo yanajumuisha jina la Muswada na masharti kuhusu namna ambavyo vifungu mbalimbali vya Sheria
vimefanyiwa marekebisho.

Sehemu ya Pili ya Muswada inapendekeza marekebisho katika vifungu mbalimbali vya Sheria. Sheria inapendekeza kurekebishwa kwa ujumla kwa kubadili masharti yote kuhusu usimamizi wa Idara kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya Usalama wa Taifa na kuweka jukumu hilo kwa Rais.

Lengo la mapendekezo hayo ni kukidhi muundo uliopo sasa ambapo Idara ya Usalama wa Taifa inawajibika moja kwa moja kwa Rais pasipo kupitia kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya Usalama wa Taifa. Mapendekezo haya yamezingatia pia mfumo wa utendaji kazi wa idara za usalama duniani.

Kufuatia mabadiliko ya jumla yanayoweka usimamizi wa Idara chini ya Rais, inapendekezwa vifungu vya 11, 15, 18, 19(3) virekebishwe ili kuondoa mamlaka ya usimamizi wa Waziri wa Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa intelijensia na usalama.

Inapendekezwa kifungu cha 4 cha Sheria kifanyiwe marekebisho kwa kuipa Idara hadhi ya Chombo cha Ulinzi na Usalama na kuiweka chini ya usimamizi wa Rais. Lengo la marekebisho hayo ni kutambua jukumu ambalo Idara imekuwa ikitekeleza kama mojawapo ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini.

Inapendekezwa sheria ifanyiwe marekebisho katika kifungu cha 5 kwa lengo la kuipa Idara majukumu ya msingi na muhimu ya usalama inayoyatekeleza kwa sasa. Majukumu hayo ni pamoja na ulinzi binafsi wa Viongozi wa Ngazi za Juu wa Kitaifa na Kimataifa, ulinzi wa Vituo Muhimu, mamlaka ya upekuzi wa kiusalama wa Viongozi na udhibiti wa matishio ya kiusalama dhidi ya Jamhuri ya Muungano.

Kifungu kipya cha 5A kinapendekezwa kuongezwa ili kujumuisha wajibu wa Waziri katika Sheria. Lengo la marekebisho haya ni kuwezesha masuala ya kisera ya Idara yanayotekelezwa na Waziri.

Inapendekeza kifungu cha 6 cha Sheria kifanyiwe marekebisho ili kuweka sifa za uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu na kuweka masharti kuhusu nafasi hiyo baada ya utumishi. Lengo ni kupata mtendaji mwenye uwezo, sifa na weledi na kulinda maslahi ya kiusalama kwa watu ambao wamewahi kutumikia nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.

Ili kuboresha utendaji kazi wa Idara, inapendekezwa kuongeza vifungu 6A na 6B katika Sheria ili kuweka masharti kuhusu nafasi za Naibu Wakurugenzi Wakuu kwa Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na nafasi ya Wakurugenzi wengine katika Idara watakaoteuliwa na Rais. Pia inapendekezwa kuweka masharti kuhusu sifa za uteuzi katika nafasi hizo tajwa.

Ili kuboresha utendaji kazi wa Idara, inapendekezwa kifungu cha 7 cha Sheria kirekebishwe kwa kuweka masharti kuhusu vigezo vya ajira kwa Watumishi wa Idara. Vilevile, kifungu kinaweka sharti la matumizi ya silaha wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa lengo la kutambua matumizi ya silaha na kuweka utaratibu wa nidhamu ya umiliki na matumizi ya silaha hizo.

Inapendekezwa Kifungu cha 10 cha Sheria kifanyiwe marekebisho ili kumtambua Mkurugenzi Mkuu kama Mshauri Mkuu wa Rais na Serikali katika masuala ya usalama wa Taifa. Lengo ni kutambua wajibu wa Idara katika usimamizi na udhibiti wa Usalama wa Taifa. Vilevile, kwa kuwa Mkurugenzi Mkuu ndiye Mtendaji Mkuu wa Idara, Sheria inarekebishwa kwa kumpa Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya nidhamu kwa watumishi walio chini yake.

Kifungu cha 10A kinapendekezwa kuongezwa ili kuweka masharti yatakayo muwezesha Katibu Mkuu Kiongozi kuratibu na kuwa kiungo baina ya Rais na Idara katika utekelezaji wa masuala ya kisera na utumishi wa umma.

Sheria inapendekezwa kufanyiwa marekebisho katika kifungu cha 13 ili kuweka utaratibu wa kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu, Naibu Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi na Maafisa wa Idara.

Inapendekezwa kifungu cha 16 kifanyiwe marekebisho ili kuzuia ufichuaji wa utambulisho wa watu wanaofanya kazi katika Idara au watu wengine wanaoshirikiana na Idara na kumpa Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya udhibiti wa watu hao. Lengo la marekebisho ni kuwalinda maafisa na watu hao kutokana na utendaji wao wa kazi za kiusalama.

Vifungu vya 16(3), 17(3), 20(2) na 23 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza viwango vya adhabu kwa makosa mbalimbali kutegemeana na uzito wa kosa. Lengo la marekebisho hayo ni kuhakikisha viwango hivyo vya adhabu vinaendana na mazingira ya sasa. Muswada unapendekezwa kuongeza vifungu vipya vya 24, 25 na 26 vitakavyoweka masharti mbalimbali ikiwemo, udhibiti wa Maafisa kutoa taarifa pindi wanapostaafu au kumaliza vipindi vya ajira, kuzuia uingiaji katika maeneo ya Idara bila idhini na masharti kuhusu vitendo vya uvunjifu wa Sheria nje ya mipaka ya Nchi.

Inapendekezwa Jedwali lifanyiwe marekebisho kwa kuongeza kiapo cha Utii pamoja na kurekebisha kiapo cha utumishi na kiapo cha kutunza siri kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa taarifa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Idara.
 
Attachments

  • THE_TANZANIA_INTELLIGENCE_AND_SECURITY_SERVICE_AMENDMENT_BILL,_2023.pdf
    440 KB · Views: 31
Hapo pa Tiss kulinda mpaka watoto wa Spika hapana, mbona watu mnataka kuidhalilisha Sana Tiss.
Beside that tunashauri tuwe na chombo kitakachoshughulika na local intelligence na International Intelligence ziwe taasisi mbili tofauti.

Pia mfumo wa ajira uwe wazi sio huu wa Sasa hivi kila DSO na; au RSO kuleta mtoto, mdogo au ndg yake na ama kupitia Uvccm wilaya.
 
Idara nyeti karne ya 21 inapaswa kujikita zaidi kwenye ujasusi Wenye tija kwa nchi sio masuala ya kuwekeana kinga hayana tija kwa taifa kama letu zaidi ya kutumika ndivyo isivyo maana wao pia ni binadamu tu kwanini wapewe kinga kama wakikosea mambo ya kijima kabisa haya karne ya sasa.
 
Muswada pia uzungumzie Mfumo wao wa ajira, na sie watoto wa kajamba nani? tuweze kuajiriwa ktk idara! ajira iwe wazi na ya kiushindani! isiwe ajira ya kinyemela! hiyo inaleta ubaguzi kwa watoto wa kimaskini ambao ni watoto wa wakulima kuwemo ndani ya Mfumo huo.
 
Mswada huu umekuja kipindi kibaya. Kwanza ni kipindi ambacho raia wanayo matumaini kuwa nchi yao inakwenda kufanya mabadiliko ya kukuza demokrasia, utawala wa sheria, haki za binadamu, uwajibakaji na uwazi. Pili mswada umeletwa wakati ambapo raia wanaendelea kusubiri majibu ya jinamizi la "watu wasiojulika" ambapo raia wamepotea katika mazingara yenye mwelekeo wa sababu za kisiasa. Pengine kabla ya kuleta mswada huu mamlaka zingejielekeza kwanza kurudisha imani ya raia kwa kutengua kitendawili cha "watu wasiojulikana". Vinginevyo, itakuwa vigumu kuwaaminisha baadhi ya raia kuwa lengo la mswada siyo pamoja na kuwalinda na kutoa kinga kwa matukio hayo ya watu kupotea, kutekwa na kuuawa.
 
Usalama wa taifa kuwa chini ya usimamizi wa rais haina afya kwa taifa. Tulimuona jiwe alivyotumia vibaya vyombo vya dola hata akatengeneza "wasiojulikana".

Kwa sheria hii tutajujq kumpata tena rais kichaa kama jiwe atakuja kuisumbua nchi kwa kutumia sheria hii.
 
Hapo wasiojulikana wanaenda kuhalalishwa kisheria.
 
Usalama wa taifa kuwa chini ya usimamizi wa rais haina afya kwa taifa. Tulimuona jiwe alivyotumia vibaya vyombo vya dola hata akatengeneza "wasiojulikana".

Kwa sheria hii tutajujq kumpata tena rais kichaa kama jiwe atakuja kuisumbua nchi kwa kutumia sheria hii.
Haya mambo ya Magufuli tuachane nayo. Miswaada na sheria zote zilizotungwa wakati wa Magufuli zilikuwa zinataka kumfanya Magufuli kama mungu
 
Marekebisho ni mazuri sana sana! Ila binafsi pamoja na upeo wangu mdogo wa mambo ya usalama nina mapendekezo haya;

1) Masharti ya manaibu wakurugenzi bara na Zanzibar yajadiliwe kwa kina, kuna mtego.
2) Mkurugenzi mkuu amepewa madaraka mazito kitu ambacho ni muhimu lakini kuwe na process makini za uteuzi wake ( mjadala wa kina).

Tukijichanganya, Rais na Mkurugenzi mkuu kutakuwa na ngoma nzito wakipishana. Hapa wasipoangalia vizuri naona yale yale ya kutenganisha kofia ya Urais na Mwenyekiti wa CCM. Kuna madaraka yanatoka kwa Rais na kubakia kwa DG.

Tuombe busara zitumike lakini maeneo mengi ya Marekebisho yataleta mapinduzi chanya kwa usalama wa Taifa!
 
Kupitia Bunge la 12 linaloendelea Jijini Dodoma, Serikali imepeleka Bungeni Muswada unaopendeleza Mabadiliko ya Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa.

Pamoja na Mambo mengine, Sheria inapendekezwa kufanyiwa marekebisho katika kifungu cha 13 ili kuweka utaratibu wa kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu, Naibu Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi na Maafisa wa Idara.

Inapendekezwa kifungu cha 16 kifanyiwe marekebisho ili kuzuia ufichuaji wa utambulisho wa watu wanaofanya kazi katika Idara au watu wengine wanaoshirikiana na Idara na kumpa Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya udhibiti wa watu hao. Lengo la marekebisho ni kuwalinda maafisa na watu hao kutokana na utendaii wao wa kazi za kiusalama.

Kifungu cha 19 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza kinga ya makosa ya jinai kwa Maafisa wa Idara tofauti na ilivyo sasa ambapo kinga imetolewa katika mashauri ya madai pekee dhidi ya Maafisa hao.

Lengo la marekebisho ni kuweka kinga dhidi ya makosa yanayoweza kutendeka wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa uaminifu.

Vifungu vya 16(3), 17(3), 20(2) na 23 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza viwango vya adhabu kwa makosa mbalimbali kutegemeana na uzito wa kosa. Lengo la marekebisho hayo ni kuhakikisha viwango hivyo vya adhabu vinaendana na mazingira ya sasa.

Muswada unapendekezwa kuongeza vifungu vipya vya 24, 25 na 26 vitakavyoweka masharti mbalimbali ikiwemo, udhibiti wa Maafisa kutoa taarifa pindi wanapostaafu au kumaliza vipindi vya ajira, kuzuia uingiaji katika maeneo ya Idara bila idhini na masharti kuhusu vitendo vya uvunjifu wa Sheria nje ya mipaka ya Nchi.

Inapendekezwa Jedwali lifanyiwe marekebisho kwa kuongeza kiapo cha Utii pamoja na kurekebisha kiapo cha utumishi na kiapo cha kutunza siri kwa lengo la kumarisha ulinzi wa taarifa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Idara.

Pia soma: Katavi: Tundu Lissu apinga Muswada wa Sheria ya Usalama wa Taifa kuwasilishwa bungeni, adai utaleta Ukiritimba

==========

ZAIDI (Kutoka kwenye nyaraka)

Muswada huu unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Idara ya Usalama wa Taifa, Sura ya 406. Lengo la marekebisho yanayopendekezwa ni kubadili masharti ya Sheria kuendana na mfumo wa utawala uliopo na taratibu za usimamizi wa Idara za Usalama kimataifa na kuweka masharti mbalimbali ya utekelezaji bora wa majukumu ya Idara.

Marekebisho yanakusudia kuboresha Sheria na kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake.

Muswada umegawanyika katika Sehemu Mbili. Sehemu ya Kwanza inahusu masharti ya awali ambayo yanajumuisha jina la Muswada na masharti kuhusu namna ambavyo vifungu mbalimbali vya Sheria
vimefanyiwa marekebisho.

Sehemu ya Pili ya Muswada inapendekeza marekebisho katika vifungu mbalimbali vya Sheria. Sheria inapendekeza kurekebishwa kwa ujumla kwa kubadili masharti yote kuhusu usimamizi wa Idara kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya Usalama wa Taifa na kuweka jukumu hilo kwa Rais.

Lengo la mapendekezo hayo ni kukidhi muundo uliopo sasa ambapo Idara ya Usalama wa Taifa inawajibika moja kwa moja kwa Rais pasipo kupitia kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya Usalama wa Taifa. Mapendekezo haya yamezingatia pia mfumo wa utendaji kazi wa idara za usalama duniani.

Kufuatia mabadiliko ya jumla yanayoweka usimamizi wa Idara chini ya Rais, inapendekezwa vifungu vya 11, 15, 18, 19(3) virekebishwe ili kuondoa mamlaka ya usimamizi wa Waziri wa Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa intelijensia na usalama.

Inapendekezwa kifungu cha 4 cha Sheria kifanyiwe marekebisho kwa kuipa Idara hadhi ya Chombo cha Ulinzi na Usalama na kuiweka chini ya usimamizi wa Rais. Lengo la marekebisho hayo ni kutambua jukumu ambalo Idara imekuwa ikitekeleza kama mojawapo ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini.

Inapendekezwa sheria ifanyiwe marekebisho katika kifungu cha 5 kwa lengo la kuipa Idara majukumu ya msingi na muhimu ya usalama inayoyatekeleza kwa sasa. Majukumu hayo ni pamoja na ulinzi binafsi wa Viongozi wa Ngazi za Juu wa Kitaifa na Kimataifa, ulinzi wa Vituo Muhimu, mamlaka ya upekuzi wa kiusalama wa Viongozi na udhibiti wa matishio ya kiusalama dhidi ya Jamhuri ya Muungano.

Kifungu kipya cha 5A kinapendekezwa kuongezwa ili kujumuisha wajibu wa Waziri katika Sheria. Lengo la marekebisho haya ni kuwezesha masuala ya kisera ya Idara yanayotekelezwa na Waziri.

Inapendekeza kifungu cha 6 cha Sheria kifanyiwe marekebisho ili kuweka sifa za uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu na kuweka masharti kuhusu nafasi hiyo baada ya utumishi. Lengo ni kupata mtendaji mwenye uwezo, sifa na weledi na kulinda maslahi ya kiusalama kwa watu ambao wamewahi kutumikia nafasi ya Mkurugenzi Mkuu.

Ili kuboresha utendaji kazi wa Idara, inapendekezwa kuongeza vifungu 6A na 6B katika Sheria ili kuweka masharti kuhusu nafasi za Naibu Wakurugenzi Wakuu kwa Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na nafasi ya Wakurugenzi wengine katika Idara watakaoteuliwa na Rais. Pia inapendekezwa kuweka masharti kuhusu sifa za uteuzi katika nafasi hizo tajwa.

Ili kuboresha utendaji kazi wa Idara, inapendekezwa kifungu cha 7 cha Sheria kirekebishwe kwa kuweka masharti kuhusu vigezo vya ajira kwa Watumishi wa Idara. Vilevile, kifungu kinaweka sharti la matumizi ya silaha wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa lengo la kutambua matumizi ya silaha na kuweka utaratibu wa nidhamu ya umiliki na matumizi ya silaha hizo.

Inapendekezwa Kifungu cha 10 cha Sheria kifanyiwe marekebisho ili kumtambua Mkurugenzi Mkuu kama Mshauri Mkuu wa Rais na Serikali katika masuala ya usalama wa Taifa. Lengo ni kutambua wajibu wa Idara katika usimamizi na udhibiti wa Usalama wa Taifa. Vilevile, kwa kuwa Mkurugenzi Mkuu ndiye Mtendaji Mkuu wa Idara, Sheria inarekebishwa kwa kumpa Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya nidhamu kwa watumishi walio chini yake.

Kifungu cha 10A kinapendekezwa kuongezwa ili kuweka masharti yatakayo muwezesha Katibu Mkuu Kiongozi kuratibu na kuwa kiungo baina ya Rais na Idara katika utekelezaji wa masuala ya kisera na utumishi wa umma.

Sheria inapendekezwa kufanyiwa marekebisho katika kifungu cha 13 ili kuweka utaratibu wa kuapishwa kwa Mkurugenzi Mkuu, Naibu Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi na Maafisa wa Idara.

Inapendekezwa kifungu cha 16 kifanyiwe marekebisho ili kuzuia ufichuaji wa utambulisho wa watu wanaofanya kazi katika Idara au watu wengine wanaoshirikiana na Idara na kumpa Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya udhibiti wa watu hao. Lengo la marekebisho ni kuwalinda maafisa na watu hao kutokana na utendaji wao wa kazi za kiusalama.

Kifungu cha 19 kinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza kinga ya makosa ya jinai kwa Maafisa wa Idara tofauti na ilivyo sasa ambapo kinga imetolewa katika mashauri ya madai pekee dhidi ya Maafisa hao.

Lengo la marekebisho ni kuweka kinga dhidi ya makosa yanayoweza kutendeka wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kwa uaminifu.

Vifungu vya 16(3), 17(3), 20(2) na 23 vinapendekezwa kurekebishwa ili kuongeza viwango vya adhabu kwa makosa mbalimbali kutegemeana na uzito wa kosa. Lengo la marekebisho hayo ni kuhakikisha viwango hivyo vya adhabu vinaendana na mazingira ya sasa. Muswada unapendekezwa kuongeza vifungu vipya vya 24, 25 na 26 vitakavyoweka masharti mbalimbali ikiwemo, udhibiti wa Maafisa kutoa taarifa pindi wanapostaafu au kumaliza vipindi vya ajira, kuzuia uingiaji katika maeneo ya Idara bila idhini na masharti kuhusu vitendo vya uvunjifu wa Sheria nje ya mipaka ya Nchi.

Inapendekezwa Jedwali lifanyiwe marekebisho kwa kuongeza kiapo cha Utii pamoja na kurekebisha kiapo cha utumishi na kiapo cha kutunza siri kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa taarifa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Idara.
Kama kelele zetu hazitasikika ni Bora Wapinzani wamlilie beberu USA na washirika wake maana ni hatari sana.
 
Haya ni maandalizi ya uchaguzi ujao, jamaa hawataki kutoka madarakani kwa kura. Kumbuka ni idara hii iliyoratibu wizi wa kura katika chaguzi ziliozopita. Mbowe maridhiano yako na Samia ni kiinimacho
 
Back
Top Bottom