Makosa makubwa tunayofanya wanaume katika mapenzi

Makosa makubwa tunayofanya wanaume katika mapenzi

Jamani mna hakika mume wake hamtumtumii pesa za matumizi? Huyu mwanamke na huyu mwanamme anayemkopesha pesa wote wanamakosa tena makubwa. Mwanamke MALAYA na MWANAUME kama sio POMOLE basi nae anatabia za kutembea na wake za watu. Utamkopeshaje mke wa mtu bila ridhaa ya MMEWE tenA ZAIDI YA MARA TATU halafu unakuja na lamb excuses ETI ITAKUWAJE USIMTUMIE MKEO PESA MIEZI MIWILI; unauhakika hamtumii?...Watakugegeda ukamsimulie mkeo...
 
QUOTE] Wewe ni mkware aliyekubuhu. Ungekuwa na nia njema na ndoa ya rafiki yako usingeleta jambo hili hapa jamvini badala yake ungetafuta mbinu ya kurescue situation ikiwa ni pamoja na kuonesha kuwa unachukizwa na hayo mawasiliano mapya ya huyo shemeji yako. Kuleta jambo linalomhusu rafiki yako kwenye public namna hii ni kumvua nguo. One thing you should know; mwosha naye huoshwa. Watch out, you are married! Kama ww unatumia ushawishi wa pesa kwa wake za watu kwann mke asifanyiwe vivo hivyo?[/QUOTE]

Nadhani hujamtendea haki mleta mada, Inawezekana hata jambo lenyewe halijamtokea yeye ,ila kwa kuwa ni vitu vinavyotokea kwenye jamii hakuna ubaya kujadiliwa, ni fundisho pia kwa wengine tunaosoma . Ninavyofahamu mtu huleta mada Jf akiwa anatafuta plan B au C. Kusema kuwa eti atategemea michango ya wadai humu sidhani kama ni sahihi. Si kweli pia kuwa jamaa amuanika mke wa mwenzake kwenye kadamnasi kama unavyodai ,nadhani ID za watu wengi humu si majina yao halisi. Au mwenzetu unamfahamu aliyejadiliwa?
Umaarufu wa JF unatokana na kujadili mada za ukweli na michango lukuki kutoka kwa kwa wadau .Na si vinginevyo.
 
Wewe ni mkware aliyekubuhu. Ungekuwa na nia njema na ndoa ya rafiki yako usingeleta jambo hili hapa jamvini badala yake ungetafuta mbinu ya kurescue situation ikiwa ni pamoja na kuonesha kuwa unachukizwa na hayo mawasiliano mapya ya huyo shemeji yako. Kuleta jambo linalomhusu rafiki yako kwenye public namna hii ni kumvua nguo. One thing you should know; mwosha naye huoshwa. Watch out, you are married! Kama ww unatumia ushawishi wa pesa kwa wake za watu kwann mke asifanyiwe vivo hivyo?

hope uememuelewa STABILIZER kwamba hatumii pesa kumvutia mke wa mtu,alimsaidia shemej yake kama shemej yake,na shemej ndo alitangaza shida,pia ameandika kuwa alipotumiwa sms alikasirika na hakupendezewa na hali ile,
isitoshe hajamtaja jina huyo swaiba wake na hata mimi na ww hatumjui mtoa mada,hakuna sababu za kuitana wakware
 
Last edited by a moderator:
Du hata katika vitabu iliandikwa Daud alipomkataa mke wa Mfalme yeye Malkia alilirarua vazi lake na kupiga yowe kuwa kabakwa kwani Daud alimkataa kulala naye
Sasa STABILIZER wewe ulimuongezea pesa za 40,000/= nini kwenda katika Msiba wao hapohapo muonee huruma hivyo hivyo kamsikilize kwani na yeye ni kiumbe huenda ameshaachana na jamaa yake kumSTABILIZER


sio daudi ndugu, ni YUSUPH! yulewa pharao! au na mie nachemka?
 
Alikuwa anakutaka akatumia style ya kukuomba pesa ili umtongoze,alaah.Hujasanda tu,we vipi bana.
 
Maisha bana...............wewe una uhakika gani huyo wa kwako unayemtimizia mahitaji ya kifedha hagegeduliwi na wengine aliko, mapenzi ya mbali ni uzushi
 
Ni funzo kubwa kwa wanaume, kama wewe sifurahii kitendo alichokifanya huyo mke wa jamaa na kwa maoni yangu hana excuse ya kufanya alichofanya; lakini kweli mumewe alipaswa kuwa responsible kwa familia yake. Why start a family kama huwezi kuiendesha?
Na kitendo cha kutegemea kipato cha mtu mmoja kwa maisha ya sasa sio nzuri kbs.
Wanawake wengine wana kiranga ata kama alikuwa anatumiwa pesa ukute alishampenda hiyo ilikuwa ni gia ya kuanzia chezea wanawake wa siku hizi balaaaaaa. Tabia ya mtu huwa haibadiliki hiyo ni tabia yake asikwambie mtu kesi hizo ni asilimia chache tu pia wanaume nao wamezidi kukimbia majukumu yao lol
 
NAWAPA KISA KIFUPI TUU AMBACHO KINANISIBU KWA SASA,

Mimi ni mwanaume, nimeoa ila kwa sasa mke wangu na mtoto wako mkoa mwingine na mimi mkoa mwingine kikazi.
Familia yangu naipenda sana na huwa nawapatia kila aina ya mahitaji mara ninapoambiwa kuna upungufu fulani wa mahitaji, hata kama sina hela niko tayari kukopa mahali lakini siyo mke wangu kwenda kukopa kwa watu. Kuna sababu kuu mbili za kutokuruhusu mwanya wa mke wangu kukopa: Moja, ni kuruhusu mwanya wa kutongozwa na hao watakaomkopesha (kama ni wanaume). Pili, inatengeneza umbea, majungu na unafiki usio na msingi especially akina mama.

Hivi karibuni kuna jamaa yangu tunafahamiana naye, naye yuko mbali na mkewe japo huja walau mara moja kwa mwezi au miezi miwili hivi, then hurudi kwenye biashara na kazi zake. Mke wake amekuwa akinisumbua sana mara kwa mara, huniomba nimkopeshe pesa. Wakati fulani nilimpa, akanirudishia. Mara ya pili akanikopa tena, muda wa kulipa ulipofika akaniambia kuwa Mr. amempigia simu kuwa bado hajapata hela, hivyo afanye atakaloweza kurekebisha mambo nyumbani. Akaniomba nimkopeshe tena, basi nikawa mpole tuu, nikaipotezea maana haikuwa hela kubwa (30,000).

Baada ya muda, akanisihi tena nimsaidie mama yake anaumwa anatakiwa aende kwao (Nauli 40,000/-) akanisihi kuwa Mr. atatuma hela wiki ijayo. Nikampa akaenda, alipofika huko dada yake akafariki ikawa ni msiba huku mama akiwa mgonjwa. Nikampa pole. Aliporudi sikudai ile 40,000/- nikijua alipatwa na matatizo, acha iwe msaada.

Baada ya wiki ananiambia Mr. anasema kuna mtu alikuwa anamdai laki 4, ametokomea na simu haipatikani. Akawa ananiuliza kuwa nimshauri afanyeje maana hata matumizi hana. Kisaikolojia ni kwamba alitaka nimsaidie tena, nikampa 10,000/-. Hiyo hali ikaendelea kidogo kidogo hivyo hivyo.

Siku moja alinitumia msg kuwa nimpigie kuna kitu anataka kuniambia. Nilipompigia alinishukuru kwa yote niliyomsaidia. Kwenye mazungumzo baadaye akaniambia njoo tulale, nikashtuka. Akaanza kunisemesha kwa sauti ya mahaba. Mwishowe uvumilivu ukamwishia, akapasua jipu. Anahitaji kuwa na mimi. Ameniambia hawezi kuvumilia tena, na amedhamiria liwalo na liwe lazima awe na mimi anipe tunda nilifaidi kama shukrani. Nilikata simu na tangu hapo nimejikuta kama vile nimelewa mawazo nimekuwa na hali ya kuchanganyikiwa kimawazo. ananitumia message za mapenzi kibao, japo mimi nimeamua kutokujibu message hizo.

Najua fika, mke wa mtu ni sumu. Lakini hoja yangu ni kuwa haya yote yasingetokea kama huyu mumewe angekuwa responsible na familia yake. Inakuwaje mtu akae miezi miwili mbali na familia yake na hatumi hela kwa visingizio vya kubanwa au kukosa hela? Sijui wadau, naombeni comment zenu hatua za kuchukua haraka at least to rescue the situation. Sisemi kuwa mimi nina hela sana, maana katika maisha kuna wakati wa kupata na kuna wakati wa kukosa, na inapotokea umekosa, wewe mwanaume fanya juu chini, bora ukope wewe mwanaume mtajuana na mdeni wako, lakini hawa wanawake ni viumbe dhaifu, ni rahisi kuingia majaribuni. Mimi sijamtongoza huyu dada na sijawahi kumtamkia mambo ya mapenzi lakini mwenyewe kalianzisha. Sasa mambo yakiharibika nani alaumiwe?

Naomba niwateteee wanaume kama ifuatavyo; mtakubalina na mimi kwamba, wanawake wote wakopaji siyo kwamba waume zao hawako responsible ni tabia tu ya kujiendekeza na kukopa kwa matumizi yake ambayo hayana maana, akiogopa kuyaweka wazi kwa mumewe. NI nani hapendi familia yake? Kama mtu una hela kwa nini usihudumie familia? Wapi imeandikwa kwamba mwanaume ndiyo mhudumiaji wa familia? Je na wale ambao hatuna wanaume tunahudumiwa na nani? Kabla ya kuolewa nani alikuwa anakuhudumia? Kama uliweza kujihudumia kabla ya ndoa kwa nini usisaidizane na mumeo kuhudumia famila pamoja?

Wanawake amkeni acheni kuwategea waume zenu sababu zisizo za msingi. Na wewe unajitia kukopesha wake wa wenzio acha hizo tabia. What if mkeo akikopeshwa??
 
sio daudi ndugu, ni YUSUPH! yulewa pharao! au na mie nachemka?
mtufulani wewe kiboko ni kweli kabisa YUSUPH yule ambaye nduguze walimtumbukiza kwemye shimo ndiye aliyeng'ang'aniwa na Mke wa Farao
DAUDI naye alikuwa na vituko kwani katika Kitabu wa 2Samweli sura ya 11 Daudi alimpenda mke wa mtu waliyekuwa akioga (Bethsheda Bint wa Eliabu mke wa Uria Mhiti) na kutuma watumishi wake wakamwite na saa hiyohiyo akalala naye na akashika mimba. Ingawa mungu hakupendezwa mtoto aliyezaliwa alikufa. MUNGU alikuja kuridhia uhusiano wao na Mke huyo wa mtu hadi wakazaa mtoto wa pili Solomoni (Mfalme Suleimani) aliyekuja kuwa mbabe na kuwa na wake wengi
Bado STABILIZER asimuogope huyo Mama amsaidie na ikiwezekana huyo jamaa aendelee hukohuko kama Daud alivyo amrisha Uria Mhiti atangulie uwanja wa vita ili auawe yeye abaki na Mke
MY TAKE wale wenye wivu samahanini msinishambulie
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom